Kuna haja ya kumuomba Hayati Dkt. Magufuli msamaha; kama taifa kuna sehemu tumekosea sana

Abraham Lincolnn

JF-Expert Member
Apr 12, 2018
2,423
4,093
Habari wakuu,

Kuna baadhi ya watu maarufu na wasiokuwa maarufu kwa muda mrefu sasa wamekuwa wakionyesha chuki za wazi dhidi ya awamu ya tano pamoja na viongozi wake. Mbaya zaidi walifika hatua ya kutaka kusahaulisha 'Legacy' na kazi kubwa sana iliyofanywa na awamu ya tano.

Kwa siku kadhaa wakosoaji hao wameshuhudia wimbi kubwa la ujambazi, ubadhirifu, uzembe kwa baadhi ya viongozi, hali ya uchumi kuzidi kudorora, Matumizi mabaya ya rasilimali za umma, hakuna miradi mipya iliyoibuliwa zaidi ya kukamilisha ile ya awamu ya tano na mengineyo mengi ndani ya muda mfupi.

Hakuna uongozi usiokuwa na mapungufu lakini ni wazi kwamba uongozi wa awamu ya tano ulifanya mambo makubwa sana yaliyowagusa Watanzania wa hali zote. Mapungufu ya awamu ya tano yalikuwa na nafuu kuliko mapungufu ya awamu yoyote ile na haya yanaanza kujidhihirisha pia katika awamu hii. Asilimia 100 ya waliokuwa wanapinga juhudi za awamu ya tano japo hawapo tayari kukubaliana na ukweli lakini wengi mioyoni mwao wanajutia na wanatubu baada ya kuanza kujionea utofauti ila wanaogopa kukiri na kuomba msamaha.

Kwa haya machache tunayo kila sababu kama taifa kuwaombea msamaha kwa Mungu na kwa jamii wale wote waliokosoa awamu ya tano kwa nia mbaya ili kuondosha laana ambayo kama taifa itaweza kuipata.
 
1623791357221.png
 
YES.

Kwa mfano familia ya Azory Gwanda inaweza kuomba msamaha kwani ndugu yao alisababisha wasiojulikana wamteke.

Au Tundu Lissu anaweza kuomba msamaha kwa kusababisha wasiojulikana wampige risasi ktk eneo linalolindwa na serikali.

Au Sugu aombe msamaha kwa kusababisha akamatwe na polisi na mahakama imfunge kwa makosa ya kusingiziwa.
 
Azory Gwanda ni nani ukilinganisha na maisha ya watanzania milioni 60?? Sugu na hao wengine wanaumuhimu kuliko wanawake wajawazito wanaokufa kwa kukosa huduma bora za afya huko vijijini?

..ukiwajumlisha azory gwanda, sugu, na wengine, ndio unapata watz milioni 60 walioko mijini na vijijini.

..pia kati ya hao milioni 60 wako waliompenda na kumtegemea Azory Gwanda, Sugu, ...hivyo hisia na maoni yao lazima yathaminiwe.

..Serikali na mamlaka za KIDIKTETA huanza mdogo-mdogo kutoa watu kafara kwa madai kwamba hawana thamani kulinganisha na walio wengi, lakini mwisho wake watu wengi zaidi haishia kupata mateso kama siyo kuuwawa au kupotea.

..MAISHA YA KILA MTANZANIA YANA THAMANI.
 
Kumuomba msamaha?

Stop kidding acha masihara kabida Ndugu.

Jiulize tu, huyu mtu angeendelea kuwa hai ina maana Sabaya angekua bado ni DC na angekua anafanya ufedhuli wake..si ndio??
Huo ni mfano mmoja tu kuonyesha huyo mtu alikuwa hafai na alikuwa toxic kabisa.

UHIMIDIWE na UTUKUZWE Ee BABA MUNGU uliyeketi juu, TUNAKUSHUKURU SANA kwa kulifyekelea mbali hili Nyangumi Meko..
Amina.
 
Kama kichwa cha mada kingetumia neno:

"Kumwombea" badala ya "kumwomba" na kusha yote baada ya dash (-) ukayafuta, ungekuwa umejitendea haki sana kwa sababu nyingi zikiwamo hizi mbili:

1. Baadhi ya madhehebu huamini kwenye kuwaombea marehemu.
2. Ni ukweli unaona fahamika kuwa awamu ile imeleta machungu yasiyomithilika kwa watu, ndugu na jamaa wengi:

Kuwataja Ben, Azory, Lissu, watu kwenye viroba, nk walioonjeshwa pepo bila kupenda, kutoshe kukuitisha kuwaomba mods kufanya marekebisho husika hapo kwenye kichwa cha juu.
 
Azory Gwanda ni nani ukilinganisha na maisha ya watanzania milioni 60?? Sugu na hao wengine wanaumuhimu kuliko wanawake wajawazito wanaokufa kwa kukosa huduma bora za afya huko vijijini?
Kwani hizo huruma za afya walizipata swami ya tano?? Rejea takwimu za Vifo vya mama na mtoto kwa kipindi hicho acha kuropoka na kadegree kako ka kudesa kama unako
 
12 Reactions
Reply
Back
Top Bottom