Peter Mwaihola
JF-Expert Member
- Jun 23, 2022
- 227
- 333
Hakuna wakati mgumu anao upitia mwanadamu kama ule wakati wa kumpoteza mtu wa karibu au ndugu yake.
Wengine hudiriki hata kujikana wao wenyewe kuwa hawawezi kuishi pasipo wapendwa wao waliofariki huchukua maamuzi magumu kwa kujiua wakiamini kuwa watakutana nao katika maisha baada ya kifo.
Lakini je kuna maisha baada ya kifo? hili ni swali pia ni fumbo ambalo wanasayansi wengi wameshindwa kulifanyia utafiti kwakuwa ili ujue kuwa kuna uzima baada ya kifo lazima ufe, na ukifa huwezi kurudi duniani kuja kutoa ushuhuda.
Wataalamu mbalimbali wa masuala ya utamaduni wanaeleza kuwa huenda kuna maisha baada ya kifo kwa kuhusianisha matukio ya mizimu ya kale na ndoto mbalimbali ambazo uhusisha binadamu walio hai pamoja na mizimu.
Ushahidi huu wa kitamaduni bado hauwezi kuwa na mashiko bado utata unabaki palepale.
Kundi la tatu ni kundi la watu wenye mlengo wa Imani ya dini za kileo hasa dini ya kikristo ambao huamini kuwa baada ya kifo kuna uzima wa milele kupitia ufufuo wa kimungu.
Kwa kutumia mifano mbalimbali kutoka ndani ya kitabu cha biblia kwa kunukuu ya maandiko, kama inavyosomeka kwenye kitabu cha matendo, 24;15 ambapo inaahidiwa kuwa kutaakuwa na ufufuo.
Pia biblia inaeleza jinsi Yesu Kristo alivyoweza kuwaponya na kuwafufua watu mbalimbali kama Lazaro aliyekaa kaburini yapata siku 4.
Kuna faida gani kuamini kuwa kuna uzima baada ya kifo?.
Kwa kawaida imani juu ya maisha baada ya kifo ina faida kubwa hasa kwa wale walio na uzima kabla ya siku yao haijafika.
Kupata faraja pindi wapendwa wanapokufa, kwa kuwa mtu anae amini kuwa kuna uzima baada ya kifo anaamini kwamba atakuja kuonana na wapendwa wake wakati wa ufufuo.
Kuacha kuogopa kufa, ni dhahiri kuwa iwapo mtu anaamini kuwa kuna uzima baada ya kifo ataacha kuogopa kufa kwakuwa anaamini ataishi tena baada ya ufufuo.
Kuwa na matumaini la kukutana na wapendwa wako waliokufa kutakuongezea ujasiri na kujiamini zaidi.
Si hivyo tu bali kuamini kuwa kuna uzima baada ya kifo kunamfanya mtu kutengeneza njia yake iliyo njema ili auone huo uzima wa milele, kama ilivyoahidiwa kwenye vitabu vya dini kuwa watakao uona huo uzima ni wale tu watenda mema, watenda maovu wote wataangamia katika moto wa jehanamu.
Peter Mwaihola ni Mwandishi wa Habari na Mchambuzi wa Masuala ya Kijamii na kisiasa.
View attachment 2421041