Kuna faida gani ya furaha au huzuni yako kumfikia mtu mwingine asiyehusika?

dmkali

JF-Expert Member
Nov 17, 2014
11,284
21,403
Natamani sana somo la ustaarabu lianze kufundishwa Shule za msingi huenda inaweza kusaidia!

Natamani sana watu wajifunze kufurahi au kuhuzunika pasipo kuathiri wengine!

Hapa ninamaanisha watu watambue umhimu wa kufanya mambo yao, ikabaki ya kwao pasipo kuathiri watu wengine bila sababu!

Nasema hivi kwasababu Afrika jambo halinogi kuwa jambo hadi limkwaze mwingine!

Mfano!
  • Mtu ana gari binafsi anapata faida gani kwa mfano kufungulia mziki mkubwa huku kashusha kioo?
  • Mtu ana matako makubwa kwa mfano, havai chupi ayabane na anapita mbele za watu kusudi.
  • Mtu ana chumba chake lakini anaamua kufungulia sauti kubwa.
  • Mtu ana shughuli binasi anaamua kuziba njia.
  • Mtu anafanya mapenzi binafsi lakini anapiga kelele hadi mtaa wa pili tena mchana.
  • Mtu anasali usiku lakini anatumia spika na maiki kana kwamba shetani ni huyo jirani yake!
  • Mtu anakunywa pombe lakini anatamba mtaa mzima.
Kwani hayo hayawezi kufanyika pasipo kukera wengine?
 
Hahaha, nimecheka hapo mtu anasali usiku kwa kutumia spika na mic kama shetani ndo huyo jirani.
 
Mara nyingi Ni Ulimbukeni na Misifa ndio Inawasumbua wengi wao Elimu zao ndogo sana ukiwachunguza wanaona maisha hayaendi bila kuhusisha watu wengine Mi huwa nawadharau kwa kiwango lami.
.Wengine hawajui kutongoza eti wakifungulia mziki anataka mpaka Ester wa nyumba ya saba kule amsikie amkubalie.
.wengine wezi wakiwa faragha mikelele ili poyoyo lake limwongezee dau na yanaongeza kweli.
.Hao wanaosali ndio kabisa mpaka sokoni watu biashara imekuwa ngumu hujauza wanakuja na maspika yao kama Promosheni za Tigo yaani wale nahisi wanavutaga na mibange sio mikelele ile.
 
Unalosema ni kweli kabisa mkuu, (kasoro hapo kwenye makalio makubwa, legeza kidogo mzee mwenzangu, fahari ya macho ni kutazama).
Well, kwa kiasi kikubwa ni ulimbukeni, elimu ndogo na lack of exposure. Wabongo tuna safari ndefu sana mpaka kustaarabika
 
Back
Top Bottom