Hukuzaliwa kuja kuokolewa na mtu

2 of Amerikaz most wanted

JF-Expert Member
Jan 13, 2023
1,328
3,692
Hakuna mtu yeyote anaye zaliwa(ku-exsist on this Earth) hapa Duniani ili aje kuokolewa ama kusaidiwa na mtu yeyote, Upo hapa Duniani ama tuite upo Katika huu ulimwengu wa tatu ili ukuze Ufahamu wako/consciousness, haujazaliwa Kuja kuokolewa na Bwana Yesu ama Kuja kufuata mafunzo ya Muhammadi , mwokozi wa maisha yako ni wewe mwenyewe , kila kinachokutokea Katika maisha haya kimesababishwa na wewe mwenyewe eidha kwa Kujua ama kwa kutokujua Ila ni wewe mwenyewe usimtafute mchawi

WEWE ni Nguvu/energy
WEWE ni Ufahamu/consciousness
WEWE ni mtu yule wa ndani
WEWE ni Roho/spirity
WEWE Huna mwanzo wala mwisho/you never die
WEWE ni Sehemu ya Ile Nguvu kuu/the source Yani MUNGU/muumba wa vyote

👉Ila... Jitafute Ujipate through Meditation/Tahajudi

Naendelea kusisitiza na kukukumbusha kuwa upo umuhimu wa dhati kabisa wa kuzitambua kanuni za kiulimwengu ijapokuwa uzijue , usizijue zenyewe zipo tu zinatenda kazi zake kulingana na hii miili yetu inavyoishi Katika huu ulimwengu wa utashi wa chini(3D) usipozijua hizi kanuni na kuzifuata basi utapata taabu Saba na hatimaye hata kujihisi umerogwa, Huna bahati, una nuksi na hata kutupa lawama kwa wazazi wako kuwa hawakukuandalia mazingira Bora kwa mustakabali wa future yako, na hapo ndipo unapozidi kujididimiza zaidi kwani kulaumu ni KUTUMA nguvu Hasi za mtetemo na mrudio(frequence & vibration) ambazo zinakurudia wewe mwenyewe kimatokeo

Usimlaumu mtu yeyote, pale unapoanza kujitambua kwa % hiyo hiyo uliyonayo kwa sasa sibudi kuanza upya hapo nisawa na Kuzaliwa upya kwani unaanza kuzitambua rangi halisi za hii dunia, anza maisha mapya hujachelewa Cha msingi Anza kuziishi kanuni hizo

◾ Anza kutambua kuwa wewe umeunganishwa na kila kitu Katika ulimwengu huu(ACHA ubinafsi) ondosha EGO/Egonism mfanyie MTU kile unachopenda kufanyiwa, kuwa na huruma

Nini maana ya huruma?
Huruma ni Hali ya mtu , kuyabeba, kuyahisi na kuyaishi maumivu, machungu, huzuni, shida na taabu anazozipitia MTU mwingine kwa kuchukua hatua madhubuti dhidi yake

◾ Tambua kuwa mawazo yetu, fikra zetu zote zipo Katika msafara mviringo, hupiga na husafiri , ukitaka kitu chochote kiweke Katika mawazo kwa muda mrefu hatimaye kitakuja kwako

◾ KUWA mtu wa kuchukua hatua ya dhati Katika jambo unalotaka kulifanya , jitume ili ulipate mfano ukitaka kwenda jela tenda mabaya utakwenda na ukitaka mafanikio basi jitume na uwe na nidhamu Katika fedha na mwaminifu kwa wengine

◾ ACHA malalamiko ukitaka Kujua upo Katika Hali gani basi mtazame jirani yako , tazama wenye shida kukuzidi, Kisha ishukuru Asili then songa mbele, fahamu ulimwengu unakupa mitihani ili kukuza Ufahamu wako, mitihani ni kipimo Cha akili

◾ Chochote ukitendacho utalipwa mara dufu, ukitenda wema utalipwa wema maradufu na ukitenda ubaya utalipwa ubaya mara dufu iwe unajua ama hujui kwani kanuni ya karma haijui Kama hujui, hivyo kuwa mwema, waza MEMA na tenda MEMA Katika jamii, mara zote karma hukaribiana na sheria ya malipo(the law of compensation, sheria ya6)

◾ Siri kubwa IPO hapa Katika maisha yako Zingatia vitu vitatu Hitaji(ask),Amini(believe) na pokea(receive) Yani kuwa na hitaji la kitu Fulani liwe dhahiri unahitaji kitu hicho, Amini kuwa kitu hicho kipo Katika mchakato, kipo njiani kukufikia(believe) Kisha Amini kishakufikia(receive) Yani Kama unataka nyumba Anza kuitembelea nyumba yako, ingia ndani, kaa sebureni tazama Runinga, kagua nyumba yako ukiwa na furaha, kwani siku nyumba hiyo utaijenga na kuishi ukiwa na furaha hiyohiyo

◾ Siku zote shinda negativity, shinda utashi wa chini epuka mawazo Hasi na huwezi kupiga hatua ingine Kama hutoishinda hiyo hatua ya utashi wa chini /lower self , mawazo mabaya pambana uyashinde kabla hayajakuletea matokeo mabaya Yani matatizo

◾ Usiogope vikwazo na majaribu, kupingwa Katika jamii ni kawaida kwani tambua kilakitu hapa duniani kina pande mbili za kiumeni na kikeni Yaani Chanya na Hasi Yani ukinzani , hutopendwa na kilamtu au kuchukiwa ama kuungwa mkono na kila mtu, wezi, vibaka, waaminifu, wakweli kwa waongo wote tunaishinao na kamwe hawataisha hivyo usimchukie MTU anayekuchukia kwani nikawaida watu hao kuwepo

◾ Katika maisha Kuna kupanda na kushuka kutokana na sababu za kadhaa wa kadhaa kwa Kujua ama kutokujua lakini ulimwengu hautakuruhusu kusonga mbele mpaka uhakikishe vikwazo vyote umevimaliza ndio usonge mbele, kwa lugha nyepesi tunasema Ujitakase kabla ya kuhitaji(ask) jambo jingine kwani ulimwengu hautokuruhusu kupiga hatua ya pili wakati ya awali inahitilafu.

Nihitimishe kwa kuomba walimu mbalimbali na wanao tufuatilia , huu sio muda wa malalamiko , sio muda wa kunyooshea vidole wazungu,waarabu sijui ni washenzi walifanya hivi na vile kwa Kuleta Dini zao , huu ni muda wa kujiokoa kuelimishana ni kwa namnagani tunaweza kutatua changamoto zetu kupitia Ukiroho wa kweli, kutuma malalamiko ni kujiongezea negativity Kisha kuturudia wenyewe Yes! nisawa wametufunga fikra zetu kwa kuficha ukweli kwa miaka Mingi,lakini hiyo sio sababu ya kuwachukia Bali wakwepe Toka kwenye mitego yao tu, Zingatia sheria namba moja [the law of Divine Oneness] inatueleza kuwa sisi sote ni kitu kimoja Yani sote tumeunganishwa Kwa pamoja.

Imeandikwa na
Naligia Mninoi... ✍️

FB_IMG_17010623688760233.jpg
 
Ulichozungumza ni fact but changamoto ipo kwa wanadumu wenzetu.. inawezekana hata mimi ni changamoto kwa mtu fulani but tujipe moyo, nakuwa positivist
 
Back
Top Bottom