Faida ya kusafiri peke yako kwenda sehemu ngeni

GoldDhahabu

JF-Expert Member
Apr 29, 2023
4,695
6,398
Ni vizuri kuwa na mwenyeji unapoenda kwa mara ya kwanza sehemu ambayo hujawahi kufika, lakini kuna faida kubwa zaidi endapo utaenda peke yako.

Kwa mfano, kama hujawahi kwenda Kenya, usisumbuke kumtafuta mtu wa kwenda naye unapotaka kwenda kwa mara ya
kwanza. Badala yake, ulizia kila kitu unachopaswa kufahamu kuhusu Kenya na safari kwa ujumla kabla ya kuanza safari.

Miongoni mwa vitu vya kufahamu ni utamaduni wa watu wa nchi husika, nyaraka unazohitajika kuwa nazo, hali ya kiusalama kwa wageni na jinsi ya kuchukua tahadhari, usafiri wa kukufikisha unakoenda, malazi, mahali kulipo na ofisi za ubalozi wa nchi yako, jinsi utakavyofanya mawasiliano na "nyumbani" kukitokea ulazima huo, n.k. Ukishayafahamu hayo yote, ujue kuwa sasa upo tayari kwa safari.

Miongoni mwa faida za kusafiri peke yako ni pamoja na:
1. Kukuongezea hali ya kujiamini
Utalazimika "kujitegemea" kwa kuwa haupo na wa "kumtegemea".

Mwisho wa safari utagundua kuwa hata wewe unaweza pasipo kuwategemea wengine kukushika mkono.

2. Kukuongezea umakini
Muda wote ukiwa safarini unajua kuwa ukilikoroga utalinywa mwenyewe, kwa hiyo umakini lazima uwepo.

Hizo ni miongoni mwa faida. Karibu uongeze zingine.
 
Hata kama mwoga itakuwa Siri Yako maana hakuna ulieongozana nae!
 
Sure kwa sasa Google map inarahisisha sana mimi ata siulizi mtu nawasha tu mtandao najiongeza. Labda niwe vijijini kusikokuwa na mtandao
 
Back
Top Bottom