Kuna Dalili ya Serikali Kufilisika

Kuna Dalili ya Serikali Kufilisika

IMF katika taarifa yake kuhusu TZ inasema by July mwaka huu most likely Nchi hii itakuwa imefilisika rasmi.
Nasema tena tatizo hapa ni Ngosha anaendekeza one man show, kila kitu ni yeye na hashauriki. Viongozi wote kuanzia Chief secretary , PM, mawaziri, wakurugenzi wa wizara, hawana maamuzi mpaka Ngosha atoe directives. Hakuna kitu kama hii iliwahi fanikiwa kokote duniani.
Kuna swali la kujiuliza hapa who is his "Mastermind"? ; Je ni Bashite , Kagame au wote? Au nani? Lazima kuna watu atakuwa anawaamini Kwa ushauri. Tukiwajua tutakuwa tumekata mzizi wa fitina. Maana tumeambiwa hata ushauri wa viongozi wastaaf haupokei.
Weka hiyo ripoti hapa
 
Mamlaka za Maji na kufilisika kwa Serikali kuna mahusiano gani? Acha uchochezi
 
Baada ya Idara ya maji katika miji ya Bukoba, Tabora na Musoma kusitisha kutoa huduma kwa wananchi za maji baada ya Idara hiyo ya maji kushindwa kulipa Tanesco bili za umeme ni dalili tosha kwa serikali ya awamu ya tano ina hali mbaya ya kifedha, kwa ujumla hali ni mbaya katika mahospitali ya miji hiyo.
Tanesco napo hali ni mbaya kifedha mpaka imefikia hatua kwa wafanyabiashara wanaotoa huduma kwa shirika hilo hilo kusimamisha kutoa huduma baada ya shirika hilo kushindwa kuwalipa madeni yao. wastaafu wengi hawajalipwa mafao zao ni hii imewaletea kuwa na hali ngumu ya maisha na kuanza kuishi maisha ya kuombaomba.
Ni wakati muafaka wa wabunge wa kikao kinachokuja kuungana ili kuiokoa Tanzania katika hali tuliyonayo hatutaki ahadi nyingi zisizokuwa za msingi kama hiyo bajeti ya trillion 31 wakati huku kwa wananchi hali ni mbaya sana kwa wananchi kufikia hatua hata huduma za muhimu kama maji inaanza kukosekana. Hivi kweli leo Serikali ya awamu ya 5 inawaza kuwa na ndege kumi na reli ya kisasa wakati maji wala madawa hospitali hakuna. Jana nimekisitika sana na kitendo cha aibu kwa kamati kuu ya CCM kukutana Ikulu na kujadili masuala ya majina ya wagombea ubunge badala ya kujadili masuala yanayohusu hali halisi ya nchi kiuchumi.
Idara za maji zinadai Taasis nyingi za serikali malimbikizo ya ankara za maji; zikilipwa zina uwezo mkubwa tuu wa kuilipa Tanesco
 
Idara ya maji ni mali ya serikali na Tanesco ni mali ya serikali inakuwaje zidaiane .?
Watanzania wanalipa kodi nyingi sana ni wajibu wa serikali kutoa huduma hii bure.
 
0c1d09409ccfd6661f99721bd6f3c6ce.jpg
Majanga
 
Mamlaka za Maji na kufilisika kwa Serikali kuna mahusiano gani? Acha uchochezi
Mkiambiwa ukweli ni uchochezi, mnatakiwa kuondoa fikra za enzi za zidumu fikra za mwenyekiti. Kama serikali haijafilisika kwanini miji hiyo hakuna maji ?
 
kama mtu anajiagizia na kugawa pesa anapojisikia yeye unategemea nini?
 
Tatizo Mkuu ni huyu mtu mmoja ambaye kawajaza woga watendaji wake kiasi cha kushindwa kumwambia kwamba anakoipeleka nchi siko. Hivi baraza lote la Mawaziri likiamua kumvaa huyu dikteta uchwara kwamba nchi inayumba awasikilize washauri wake na aachane na udikteta atafukuza wangapi!? Hivi wastaafu Mawaziri Wakuu na Marais wakijipanga kwenda kuongea naye Ikulu kuhusu nchi kwenda mrama atawafanya nini!?

Kwanini mtu mmoja aachiwe kuiyumbusha nchi kiasi hiki na wale walio karibu yake waamue kukaa kimya kwa kumuogopa!?
Dahh unasubiria embe chini ya mchungwa soo whaaatt hata wakimwambia ndo afanyeje kama hela hazipo ni hazipo akachapishe au achimbe ardhini hakuna jipya ni kupiga perereee tuu wacha kilichopo kitumike hakitoshi jibane kuishi na uwezo uliopo kuna familia wanakula mlo mmoja jiulize kwanini ni kula kwa kile walichonacho sasa afanyeje na amekuta hazina hamna hela... acheni ushambenga na ushiranga
 
KIPINDI KILE ANAJENGA MABARABARA ALIKUWA HAJUI KIKWETE HELA ANATOA WAPI, KAZI YAKE ILIKUWA KUKREMU KILOMETERS BILA KUJUA KUPATA HELA INABIDI UTOKE NJE.

ATOKE AKASEMEZANE NA WAKOLONI TUPATE HELA YA BAJETI.

KWASASA NG'OMBE ANAYEKAMULIWA ANATOA DAMU SI MAZIWA TENA.
 
Idara ya maji ni mali ya serikali na Tanesco ni mali ya serikali inakuwaje zidaiane .?
Watanzania wanalipa kodi nyingi sana ni wajibu wa serikali kutoa huduma hii bure.
NOOOOOOOO. Hizi huduma za maji na umeme tunalipia kiasi kufidia gharama za uendeshaji; inapotokea sisi wateja tunatumia hizo huduma halafu hatulipi kwa wakati ndiposa hizo taasisi hushindwa na zenyezwe kulipia gharama zake za uendeshaji. Bahati mbaya sana wateja wabovu (wasiolipia huduma kwenye taasis za serikali) ni taasisi za serikali
 
Tunyooshe tunyooshe anco magu-mpaka watanzania akili ziwakae sawa
Nyerere alisema makabila makubwa sio ya kuwapa nchi -watu hawakuelewa maana yake bado lowassa akasema bwana yule amekuwa chini yangu mm ninamfahamu bora angekuwa mwingine watu hawaoni wala hawasikii
Mara tunataka raisi mkali-mara tunataka rais dicteta hay sasa Mungu kawapa kama mlivyohitaji.
 
Baada ya Idara ya maji katika miji ya Bukoba, Tabora na Musoma kusitisha kutoa huduma kwa wananchi za maji baada ya Idara hiyo ya maji kushindwa kulipa Tanesco bili za umeme ni dalili tosha kwa serikali ya awamu ya tano ina hali mbaya ya kifedha, kwa ujumla hali ni mbaya katika mahospitali ya miji hiyo.
Tanesco napo hali ni mbaya kifedha mpaka imefikia hatua kwa wafanyabiashara wanaotoa huduma kwa shirika hilo hilo kusimamisha kutoa huduma baada ya shirika hilo kushindwa kuwalipa madeni yao. wastaafu wengi hawajalipwa mafao zao ni hii imewaletea kuwa na hali ngumu ya maisha na kuanza kuishi maisha ya kuombaomba.
Ni wakati muafaka wa wabunge wa kikao kinachokuja kuungana ili kuiokoa Tanzania katika hali tuliyonayo hatutaki ahadi nyingi zisizokuwa za msingi kama hiyo bajeti ya trillion 31 wakati huku kwa wananchi hali ni mbaya sana kwa wananchi kufikia hatua hata huduma za muhimu kama maji inaanza kukosekana. Hivi kweli leo Serikali ya awamu ya 5 inawaza kuwa na ndege kumi na reli ya kisasa wakati maji wala madawa hospitali hakuna. Jana nimekisitika sana na kitendo cha aibu kwa kamati kuu ya CCM kukutana Ikulu na kujadili masuala ya majina ya wagombea ubunge badala ya kujadili masuala yanayohusu hali halisi ya nchi kiuchumi.
Mbona hata uliyoyataja ni maendeleo na sio kana kwamba nchi inafilisika. Hiv broo mnafikiria nini mpaka mnapost hivi au ndio mihemuko ya kisiasa tu. Acheni bwana tabia hii jaman. Mbona mambo ya kuongelea ni mengi na yapo na sio kupotosha huku. Kwan wewe upo huko kagera na umeshuhudia jambo kama hili linafanyika na watu wanakufa kwa kukosa hayo maji au nchi imefirsika kweli??
 
IMF katika taarifa yake kuhusu TZ inasema by July mwaka huu most likely Nchi hii itakuwa imefilisika rasmi.
Nasema tena tatizo hapa ni Ngosha anaendekeza one man show, kila kitu ni yeye na hashauriki. Viongozi wote kuanzia Chief secretary , PM, mawaziri, wakurugenzi wa wizara, hawana maamuzi mpaka Ngosha atoe directives. Hakuna kitu kama hii iliwahi fanikiwa kokote duniani.
Kuna swali la kujiuliza hapa who is his "Mastermind"? ; Je ni Bashite , Kagame au wote? Au nani? Lazima kuna watu atakuwa anawaamini Kwa ushauri. Tukiwajua tutakuwa tumekata mzizi wa fitina. Maana tumeambiwa hata ushauri wa viongozi wastaaf haupokei.
"Mimi ni raisi nnae jiamini" " mimi huyu wakunipangia ukijaribu ndo utakua umepoteza kabisa " unategemea nini hapo mwafwaaaaaaaaaaaa " magufuli is not my president "
 
Fedha zote zikikusanywa popote zinapelekwa serikali kuu,kisha ndio wanaomba kwa ajili ya matumizi yao,sasa zinazopelekwa huko ni kidogo na hazitoshi,usishangae ukienda hata polisi au mahakamani ukaambiwa hatuna karatasi nenda nje katoe coppy,hii ndio Tanzania mpya ya viwanda
 
Sasa kama halmashauri hazipati OC unategemea walipe bili za MAJI na umeme kwa mishahara yao!
Ni ajabu sana japo ni kweli! TANESCO kuamriwa kuwakatia umeme wateja ambao hawakupewa pesa walizoomba kwa kazi hiyo kwa ukamilifu!
 
Tatizo Mkuu ni huyu mtu mmoja ambaye kawajaza woga watendaji wake kiasi cha kushindwa kumwambia kwamba anakoipeleka nchi siko. Hivi baraza lote la Mawaziri likiamua kumvaa huyu dikteta uchwara kwamba nchi inayumba awasikilize washauri wake na aachane na udikteta atafukuza wangapi!? Hivi wastaafu Mawaziri Wakuu na Marais wakijipanga kwenda kuongea naye Ikulu kuhusu nchi kwenda mrama atawafanya nini!?

Kwanini mtu mmoja aachiwe kuiyumbusha nchi kiasi hiki na wale walio karibu yake waamue kukaa kimya kwa kumuogopa!?
atavunja baraza ana ile kauli kuanza upya sio ujinga
 
Back
Top Bottom