Bowie
JF-Expert Member
- Sep 17, 2016
- 4,373
- 6,084
Baada ya Idara ya maji katika miji ya Bukoba, Tabora na Musoma kusitisha kutoa huduma kwa wananchi za maji baada ya Idara hiyo ya maji kushindwa kulipa Tanesco bili za umeme ni dalili tosha kwa serikali ya awamu ya tano ina hali mbaya ya kifedha, kwa ujumla hali ni mbaya katika mahospitali ya miji hiyo.
Tanesco napo hali ni mbaya kifedha mpaka imefikia hatua kwa wafanyabiashara wanaotoa huduma kwa shirika hilo hilo kusimamisha kutoa huduma baada ya shirika hilo kushindwa kuwalipa madeni yao. wastaafu wengi hawajalipwa mafao zao ni hii imewaletea kuwa na hali ngumu ya maisha na kuanza kuishi maisha ya kuombaomba.
Ni wakati muafaka wa wabunge wa kikao kinachokuja kuungana ili kuiokoa Tanzania katika hali tuliyonayo hatutaki ahadi nyingi zisizokuwa za msingi kama hiyo bajeti ya trillion 31 wakati huku kwa wananchi hali ni mbaya sana kwa wananchi kufikia hatua hata huduma za muhimu kama maji inaanza kukosekana. Hivi kweli leo Serikali ya awamu ya 5 inawaza kuwa na ndege kumi na reli ya kisasa wakati maji wala madawa hospitali hakuna. Jana nimekisitika sana na kitendo cha aibu kwa kamati kuu ya CCM kukutana Ikulu na kujadili masuala ya majina ya wagombea ubunge badala ya kujadili masuala yanayohusu hali halisi ya nchi kiuchumi.