Kuna anguko kubwa sana la kujua kuandika sentensi na herufi sahihi za maneno miongoni mwetu Watanzania

Jamani hali ni mbaya sana, watu wanajua kuhesabu lakini kusoma na kuandika ni utapia kichwa, utapia ujinga unaangamiza taifa nyakati za sasa katika uga wa mawasiliano kwa njia ya maandishi, sms, chats etc.

Sijui labda ni mimi tu naliona hili. Uandishi mbovu na makosa ya herufi sahihi kwenye maneno.

Mungu aingilie kati hili anguko, naogopa sana tuko tuendako.

Ni hayo tu.

Wadiz
"Sijui labda ni mimi tu naliona hili." Hakuna Kiswahili sanifu kama hiki Tanzania
 
Sisi tutakwenda Kenya kuwafundisha kuongea wao watakuja Tanzania kutufundisha kuandika.
Kama shule ya msingi hukujifunza kuandika na kuongea vizuri hata ukiwa na PhD utaendelea kupuyanga.
Ni vyema walimu wa Primary nao wafundishwe kuongea na kuandika kwa ufasaha ili kuokoa kizazi kijacho.
Nasema kizazi kijacho kwakuwa hiki tayari Kiko shimoni.
Irabu na silabi zinachanganywa kama zege.
 
Screenshot_20231022_164103_Samsung Internet.jpg
 
Inaongozwa na Inaenezwa zaidi na hizi local TV na Radio kuna watu ukiwasikiliza kwa radio ama TV unajiuliza huyu mtu alivutwa na kamba kufanya hii kazi,alihongwa au alibebwa mwenye kituo ni ndugu yake?jamani kuna radio huku mbinga inaitwa Ruvuma FM kipundi Chao cha sa nne cha michezo kile mama weee kuna kilaza kimoja hicho maaaweeeee jamani malazi maradhi hajui kutofautisha z.. na dh..l
 
Jamani hali ni mbaya sana, watu wanajua kuhesabu lakini kusoma na kuandika ni utapia kichwa, utapia ujinga unaangamiza taifa nyakati za sasa katika uga wa mawasiliano kwa njia ya maandishi, sms, chats etc.

Sijui labda ni mimi tu naliona hili. Uandishi mbovu na makosa ya herufi sahihi kwenye maneno.

Mungu aingilie kati hili anguko, naogopa sana tuko tuendako.

Ni hayo tu.

Wadiz
Kwakweli ni kubwa sana kiasi cha kutia mashaka kuwa, huenda baada ya miaka kadhaa lugha ya kiswahili ikapotea kama zinavyopotea kwa kasi lugha za baadhi ya makabila.
Imekuwa ni changamoto sana kutofautisha matumizi ya "r" na "l", pia changamoto ya matumizi sahihi ya maneno yanayotaka kufanana kiuandishi lakini yanatofautiana muktadha kama vile "mahali" na "mahari".
Pia unakuta Mhitimu wa elimu ya juu au Chuo kikuu kabisa badala ya kuandika "Habari?", yeye anaandika "abari", au "habali".
Tena kuna ugonjwa umeibuka wa matumizi ya herufi "h" mahali pasipo stahili na kuacha kuitumia panapo stahili; Unakuta mtu anakuandikia "Abari ya hasubuhi?" au mwingine anasema "humeamkaje?".
Kwakweli jitihada za makusudi kabisa zinahitajika kufanyika ili kuinusuru hii lugha.
 
Wewe unashida. Mtu akijifunza lugha zaidi ya moja anaweza kuingia kwenye tatizo la kuchanganya lugha sikumbuki wanaitaje kuna neno maalumu la hao watu.
Basi wewe akili yako haiko sawa, mjomba mimi nimejifunza Kiarabu naongea na kusoma kiasi maandishi yale, niliwahi kujifunza Kifaransa, Kiingereza kwangu sio shida hata kidogo ila hakuna siku nikakosea kutumia herufi zitakiwazo pahala sahihi labda iwe ni typing errors tu na sio mistake hiyo
 
Uwe unasoma na kuelewa. Usijibu tu kujifanya wewe ndio unajua. Wewe unadhani sisi ndio hatujui hizo lugha ulizotaja. Kuna mahubiri gani msikitini ramewahi tolewa bila mhubiri kuchanganya lugha ?
Halafu unavyosema wewe huchanganyi lugha nani amekupima na kuthibitisha kuwa unaongea lugha fasaha?
Tafuta mada ielezee kwa dk 20 halafu iweke hapa tukupime kwa vitendo.
 
Back
Top Bottom