Kuna anayewafahamu vizuri ForePlan Clinic ya Dr. Mwaka?

Udaktari ni nini?

Daktari (ma) ni neno la asili ya Kilatini lililoingia Kiswahili kwa kupitia
Kiingereza . Hutumiwa na maana mbili:


1) Mtaalamu aliyepata mafunzo maalum kwenye chuo kikuu ya kutibu
maradhi au wagonjwa. Mtu wenye ujuzi wa kutibu wanaitwa pia mganga (wa) , tabibu (ma) .

2) Kwa kufuata tabia za lugha nyingine
dakta(ri) hutumiwa pia kama jina la heshima la mtu aliyepata shahada ya juu kabisa.
 
Mkuu Tabby, nimechukua tu sehemu uliyoongelea weakness za professional Mds umeandika ukweli mtupu maana bila hayo mapungufu watu wasingekimbialia kikombe cha babu au hao wengine, THUM UP ila hayo mengine ya kum-attack muanzisha thread kama hayakustahili maana yanapunguza nguvu ya hoja uliyoielezea kwa kina juu ya mapungufu ya Mds

Lengo halikuwa kum attack hasa. Nilitaka aone jinsi alivyojenga hoja yake juu ya msingi mwepesi wa makoti na miaka ya kusota shuleni ambayo ili reflect wivu na au hadi mtu ateseke kama alivyoteseka yeye.

Nimemwambia somewhere alitakiwa ajenge competitive grounds kama ethics za kazi, competence, athari za hizo practices kuliko kukazania makoti na miaka ya kusota as if ndiyo vigezo vya kudeliver.
 
Mkuu kuna tofauti kati ya dr wa kutibu watu na dr phd,wote wanaitwa dr. Kikwete ni phd,kina mengi na wengine.

Phd unaweza kutunukiwa kwa heshima kama ilivyo kwa kikwete au ukaseomea kama ilivyo kwa dr mwakiembe.

Dr wa kutibu watu lazima uende shule miaka kadhaa.

Sema tatizo siku hizi kujiita dokta hapa kwetu imekua kama fasheni,waganga wa kienyeji nao ni dokta na wengine profesa kama maji marefu.


Kuhoji yule jamaa wa msoga na weupe wake kasoma wapi, nilikuwa namwelekeza kwenye ufahamu kwamba Neno Dr halimaanishi ni medical Dr. tu na halimaanishi kama alivyosema kwamba lazima mtu akasome. Alitakiwa kutofautisha.
Lakini kikubwa, kumshambulia huyo Mwaka kwa misingi ya kuvaa makoti, kujitangaza hakuna maana kwa sababu koti siyo medication wala medical skills. Mtu anayechukulia koti kwamba ni la Drs na mwingine haruhusiwi kuvaa, ninaona hata huo udaktari haujui.
 
UFAFANUZI.
1/Dr.Mwaka ni mtaalamu wa kutibu binadamu kwa kutumia miti shamba, ni utaalamu aliosomea nje ya nchi na kufuzu(Serikali ya Tanzania inamtambua hivyo na anavyo vyeti katika fani hiyo)

2/Kwa jinsi nilivyomfatilia kupitia vipindi vyake kwenye Tv na nilipowauliza wataalamu wa Afya kuhusu yale anayoongelea Dr.Mwaka, kiujumla Dr.Mwaka anaifahamu vizuri Sayansi ya mwili wa Binadamu, anafahamu vizuri tiba mbalimbali za kihospitali na anazijua tafiti za tiba kwa kina(Jamaa ni intellectual kabisa)

3/Dr.Mwaka yuko sahihi kabisa kutumia Kipaji chake na utaalamu wake wa kutibu watu na kujipatia fedha na mali anazozitaka. Ni haki yake kwa sababu anafuata sheria, analipa kodi na anatumia uhuru wake.

4/Hakuna shida yoyote kwa Dr.Mwaka kutumia koti jeupe au kujiita Daktari, kwa sababu neno Daktari lina maana ya Mganga, na koti jeupe mtu yoyote anaweza kuvaa pasipo kujali utaalamu alionao. Mpishi, Muuza nyama, Mfanyakazi wa Mochwari, Muuza duka la dawa, Mfanyakazi wa kiwandani, Muuza juice nk. Wote huwa wanavaa makoti meupe mara nyingi.

5/Watu wengi wanaokwenda kwa Dr.Mwaka mara nyingi wanakuwa tayari wamewahi kufika katika Hospitali zingine kwa kupimwa au kutibiwa lakini mwisho wa siku hawakupona, hivyo wakiwa wamekata tamaa ya kupona ndio wanaamua kwenda kwa Dr.Mwaka, sasa kwa hali hiyo kuna kitu gani cha kumlaumu Dr.Mwaka?
 
Usichoke kuwaelimisha. Wengi hawajui mpaka ukae mwaka bila ujauzito ndipo inachukuliwa kuna tatizo.

Halafu viuzibeuzibe kwenye mirija ndivyo husababisha mayai kuwa weak?????? Hii mpya ya Mwaka......
Na maumivu ya tumbo wakati wa hedhi ni kawaida unless aseme maumivu ya mkewe ni ya kupitiliza au ana endometriosis etc etc


Tatizo la mitandao ya kijamii ndio hili. Every Tom, Dick and Hurry anajifanya mjuaji.

Haya endeeleeni kudanganyana na mayai yasiyo na nguvu na vipimo vya hormones vya vichochoroni. Story za dawa ya mirija iliyoziba ndio mnazofurahia.

Sikio la kufa halisikii dawa...
Anyway alianza Mama Terri akazikomba akasepa...

Akaja dr Ndodi akachukua akasepa

Babu wa loliondo alikusanya akasepa

Sasa wakati wa Mwaka kuzikomba
 
Usichoke kuwaelimisha. Wengi hawajui mpaka ukae mwaka bila ujauzito ndipo inachukuliwa kuna tatizo.

Halafu viuzibeuzibe kwenye mirija ndivyo husababisha mayai kuwa weak?????? Hii mpya ya Mwaka......
Na maumivu ya tumbo wakati wa hedhi ni kawaida unless aseme maumivu ya mkewe ni ya kupitiliza au ana endometriosis etc etc



Anyway alianza Mama Terri akazikomba akasepa...

Akaja dr Ndodi akachukua akasepa

Babu wa loliondo alikusanya akasepa

Sasa wakati wa Mwaka kuzikomba


Dr Badili Tabia utaanza lini uzikombe tuje kukopa?
 
Jamani naomba kujua,

Hivi Dokta mwaka yeye anatibu akina dada zetu na wanawake tu? Nauliza hivi kwa kuwa kila nimsikiapo either Redioni or katika Runinga (TV) yeye huzungumzia tu magonjwa yanayowasibu dada, wake na mama zetu.....Mara Utamsikia sijui fibroid, mara matiti kuuma, hujakaa sawa utasikia sijui kukoma kwa hedhi, hujapumua vizuri utasikia miscarriages, hujapumzika vizuri mara unasikia sijui uvimbe sehemu ya kizazi na ukisema ukae utafakari anakuja tena sijui na mirija ya uzazi na kadhalika.

Swali langu hivi huyu Dokta Mwaka yeye hospitali yake Foreplan Herbal Clinic inatibu tu jinsia ya kike? Ina maana sisi wa kiumeni hatuna matatizo? Sisi yetu nadhani anaweza kuona ni machache ila nadhani wanaume wengi ndiyo tuna matatizo ya kufa mtu!

Naomba kuwasilisha, Jumapili njema.

Watu rahisi kuwashika na wepesi kufata doctor ni wanawake.. Watu wanaplan zao aisee..
 
Watu wengi wana maradhi mbalimbali.Mfano mzuri ni jinsi watu walivyokuwa wanamiminika Loliondo kutafuta tiba wakati mahospitali yapo wakati Loliondo ilikuwa ni tiba feki tu.Na wagonjwa wengi walipoteza maisha baida ya kunywa kikombe cha babu kwa sababu waliacha dawa zao za VVU ,kisukari nk.
Sasa anapotokea mtu akaona huduma za tiba ni fursa ya kujipatia utajiri wa haraka haraka kwa kwa kutumia udhaifu wa wenye magonjwa inakuwa si sahihi.
Dr Mwaka ni mzungumzaji sana na anakuwa anazungumza ili kuvuta wagonjwa waende kwake.Mimi naona tiba mbadala ni tiba inayokubalika iwapo mgobjwa karidhia ila watu wapewe angalizo kabla ya kujiingiza huko kuhusu faida na hasara.
 
Dr mwaka katoka nduki kamkimbia Naibu waziri wa afya alipodhuru ktk clinic yake

Ovaaa
 
Back
Top Bottom