Polisi wampe ulinzi mke wa Dr. Mwaka. Sakata la ndoa yao lina vita ya kiuchumi ambayo inaweza kupelekea mauaji

dmkali

JF-Expert Member
Nov 17, 2014
11,284
21,403
Sitapenda kuchimba sana kwenye mgogoro wa ndoa

Lakini naomba kusema machache kwenye sura ya usalama wa kila mmoja kwenye mgogoro huo!

Ukitazama kwa juu juu unaweza kushangaa kwanini mambo yao ya ndoani yameifikia jamii.

Lakini ukitafakali sana unagundua sakata lao ni sawa na moto, ulianza kama moto mdogo ndani ya nyumba yao lakini ulishindikana kuzimwa kwa faya extuingusher, hivyo moto umekuwa mkubwa moshi umetanda kiasi cha kuhitaji msaada wa jamii na zimamoto!

Hivyo serikali ikichelewa kutoa msaada wa haraka itakuwa kama zimamoto iliyochelewa! Hakutakuwa na kuokoa kila kitu kitapukutika!

VITA YA KIUCHUMI NI MBAYA SANA
Queen (mke wa Dr Mwaka) anaonekana kuhitaji taratibu zote za haki zifuatwe katika sakata lao la ndoa! Lakini anayokutana nayo kwenye kesi yake huenda kama siyo Rushwa basi yanavurugwa na mfumo dume!

Kwa maelezo yake mwenyewe anakutana na majibu ya jeuri, vitisho katika mamlaka yake ya haki ya ndoa! (Swali kwanini wamtishe? Kwa nini wamjibu jeuri mteja katika shauri la haki?

utakubaliana na mimi kwamba Kama siyo rushwa basi ni mfumo dume!
Ambapo kama Tabia hii haijakomeshwa iko siku taifa litaingizwa kwenye migogoro ya kijinsia! (Tusifike huko)

KWANINI HAYO YOTE?
Kwa taswira ya mmoja mmoja hakuna anayemhitaji mwenzake kindoa! Lakini kwasababu za kiuchumi ndicho kinacholeta marumbano hayo!.

TUKIANZA NA DR. MWAKA!

Huyu MWAKA ni mfanyabiashara, kazi yake kubwa inayompa wateja wengi ni kusuluhisha migogoro ya ndoa na tiba kwenye masuala ya uzazi (ndoa)!.

faida ya kazi hii ndiyo inayomlisha, ndiyo iliyompatia wake zake wengine!

Kwa mfano!
Endapo Ahadi ya wateja wa Dr. MWAKA kumuona kwa ajili ya ushauri wa kindoa walilipia (laki tatu ~Hadi tano) inamaana kwa siku anaweza kuwa anaingiza zaidi ya (2mil hadi 5mil) bila shaka itakuwa ni pesa nyingi kwa mwezi na mwaka!

Ukiachilia mbali kazi ya ushauri, Imani ya mauzo ya dawa zake kutibu ndoa za wengine ni kubwa!

Hivyo ukijumlisha tiba na mauzo ya dawa utaona ni pesa nyingi kiasi gani
.
kwa lugha rahisi ni kwamba kumuua Dr. Mwaka kibiashara ni KUONDOA IMANI KWA WATEJA!

Hivyo kwa gharama yoyote iwe mvua iwe jua TALAKA YA NDOA HII Haiwezi kuwa rahisi kama wengi walivyotarajia!.

Kumpoteza mke wake kwa talaka ni shambulio kubwa sana la kibiashara ya mwaka pamoja na mapato pia inahatalisha ndoa zake zingine!

Swali ni je hayo yote dr. Mwaka hakuyajua mapema?

majibu ni mepesi tu "Kiburi cha pesa, Dharau na mfumo dume"
hivyo ndivyo vinavyoweza kuwa vimechangia!

Sakata hili ni sawa na bundi kuhamia kwa mganga! Analia usiku kucha, na mganga badala ya kupiga manyanga kwa tiba badala yake anatoa silaha kumpiga bundi ili kumnyamazisha kufumba wateja wake wasimkimbie!

Katika vita hii Dr mwaka anaweza kufanya tukio baya sana ili kulinda biashara yake na wake zake!

Usalama wa Queen upo mashakani kama polisi hawatampa ulinzi kuanzia sasa!

Mambo yao ya kisheria na haki yatizamwe haraka kwa usalama wao!

Mgogoro wa nyumba ni sehemu ndogo sana wa maslahi ya Dr.mwaka!

Maslahi makubwa ya anayolinda Mwaka ni biashara yake na wake zake wanaobaki wasimkimbie!

Ikumbukwe pia mwaka anamikopo benki ambayo marejesho yanategemea biashara hiyo!

Updates
TUME YA HAKI ZA BINADAM ikiongozwa na kamishina wamefika kwa mke wa mwaka ili kuona namna ya usalama wa mwanamke umeguswa! Na wamebaini kuna HOJA ya msingi ambayo inahitaji msaada!

Hivyo uwezekano wa mwaka kufanya ukatili ili kuifumba jamii ni mkubwa mno endapo shauri lao kama halitasikilizwa mapema! Na itangazwe wazi!
 
Acha kiherehere, wampe ulinzi kwa umuhimu gani alionao. Watu kuoana na kuachana ni kawaida na wapo kibao, sasa polisi italinda kila walioachana?!!
Ninadhani mleta mada amepata msukumo wa kutoa ushauri huo kutokana na mvutano uliopo.
Mvutano huo umejumuisha mpaka mashabiki sasa kwamtazamo wa mleta mada ameona upepo huo utamtoa mtu roho
 
Huyo Mwaka kazingua sana..yule mama kwa maelezo ya jana...anahitaji kusepa tu..lkn pia kwa ajili alivyokua anaongea..yuko tayari kutulia kama atabembelezwa...shida huyo Mwaka ni kama hajui anataka nini, anampiga pini kila idara bila direction yoyote
 
Huyo Mwaka kazingua sana..yule mama kwa maelezo ya jana...anahitaji kusepa tu..lkn pia kwa ajili alivyokua anaongea..yuko tayari kutulia kama atabembelezwa...shida huyo Mwaka ni kama hajui anataka nini, anampiga pini kila idara bila direction yoyote

Sent from my SM-A205F using JamiiForums mobile app
Mnajifanyaga wabobezi kwenye maswala ya ndoa kumbe vilaza wakubwa!

Hakuna lolote. Ujinga tu.
 
Back
Top Bottom