UFAFANUZI.
1/Dr.Mwaka ni mtaalamu wa kutibu binadamu kwa kutumia miti shamba, ni utaalamu aliosomea nje ya nchi na kufuzu(Serikali ya Tanzania inamtambua hivyo na anavyo vyeti katika fani hiyo)
2/Kwa jinsi nilivyomfatilia kupitia vipindi vyake kwenye Tv na nilipowauliza wataalamu wa Afya kuhusu yale anayoongelea Dr.Mwaka, kiujumla Dr.Mwaka anaifahamu vizuri Sayansi ya mwili wa Binadamu, anafahamu vizuri tiba mbalimbali za kihospitali na anazijua tafiti za tiba kwa kina(Jamaa ni intellectual kabisa)
3/Dr.Mwaka yuko sahihi kabisa kutumia Kipaji chake na utaalamu wake wa kutibu watu na kujipatia fedha na mali anazozitaka. Ni haki yake kwa sababu anafuata sheria, analipa kodi na anatumia uhuru wake.
4/Hakuna shida yoyote kwa Dr.Mwaka kutumia koti jeupe au kujiita Daktari, kwa sababu neno Daktari lina maana ya Mganga, na koti jeupe mtu yoyote anaweza kuvaa pasipo kujali utaalamu alionao. Mpishi, Muuza nyama, Mfanyakazi wa Mochwari, Muuza duka la dawa, Mfanyakazi wa kiwandani, Muuza juice nk. Wote huwa wanavaa makoti meupe mara nyingi.
5/Watu wengi wanaokwenda kwa Dr.Mwaka mara nyingi wanakuwa tayari wamewahi kufika katika Hospitali zingine kwa kupimwa au kutibiwa lakini mwisho wa siku hawakupona, hivyo wakiwa wamekata tamaa ya kupona ndio wanaamua kwenda kwa Dr.Mwaka, sasa kwa hali hiyo kuna kitu gani cha kumlaumu Dr.Mwaka?