Kuna anayewafahamu vizuri ForePlan Clinic ya Dr. Mwaka?

Neno Doctor ni neno la kizungu kwa kiswhili maana yake ni ni mganga sasa wewe usishangae Dr mwaka kuita Doctor? mbona Viongozi wenu wa nchi munawaita Ma-Doctor? Je nao pia wamesomea huo U-Daktari shuleni? au munawapa vyeo amabavyo haviwahusu? Wewe ulitaka Dr Mwaka ajiite Jina la Mganga Mwaka? ndio ungeona lingemfaa kuita jina hilo kuliko kutumia jina la kizungu yaani Doctor? Acha hivyo kama una bifu na Dr Mwaka bora sema ili mradi Dr Mwaka havunji sheria zanchi muache awatibie watu. Mbona mimi ninawatibu wateja wa Dr mwaka na wanapona wakati mimi sio Dr?

Ni kama hutofautishi kati daktari wa tiba (tabibu) na daktari wa falsafa!! Doctorate in Philosophy (PhD)
 
Yap Hata babu wa loliondo aliuaga umaskini kwa ubunifu huo na bado wapo wataalam kibao wakusafisha nyota mtaani na wateja wanapata so be creative be millionaire
 
UFAFANUZI.
1/Dr.Mwaka ni mtaalamu wa kutibu binadamu kwa kutumia miti shamba, ni utaalamu aliosomea nje ya nchi na kufuzu(Serikali ya Tanzania inamtambua hivyo na anavyo vyeti katika fani hiyo)

2/Kwa jinsi nilivyomfatilia kupitia vipindi vyake kwenye Tv na nilipowauliza wataalamu wa Afya kuhusu yale anayoongelea Dr.Mwaka, kiujumla Dr.Mwaka anaifahamu vizuri Sayansi ya mwili wa Binadamu, anafahamu vizuri tiba mbalimbali za kihospitali na anazijua tafiti za tiba kwa kina(Jamaa ni intellectual kabisa)

3/Dr.Mwaka yuko sahihi kabisa kutumia Kipaji chake na utaalamu wake wa kutibu watu na kujipatia fedha na mali anazozitaka. Ni haki yake kwa sababu anafuata sheria, analipa kodi na anatumia uhuru wake.

4/Hakuna shida yoyote kwa Dr.Mwaka kutumia koti jeupe au kujiita Daktari, kwa sababu neno Daktari lina maana ya Mganga, na koti jeupe mtu yoyote anaweza kuvaa pasipo kujali utaalamu alionao. Mpishi, Muuza nyama, Mfanyakazi wa Mochwari, Muuza duka la dawa, Mfanyakazi wa kiwandani, Muuza juice nk. Wote huwa wanavaa makoti meupe mara nyingi.

5/Watu wengi wanaokwenda kwa Dr.Mwaka mara nyingi wanakuwa tayari wamewahi kufika katika Hospitali zingine kwa kupimwa au kutibiwa lakini mwisho wa siku hawakupona, hivyo wakiwa wamekata tamaa ya kupona ndio wanaamua kwenda kwa Dr.Mwaka, sasa kwa hali hiyo kuna kitu gani cha kumlaumu Dr.Mwaka?

Sisi hatuna pesa za kwenda India na dokta Mwaka ni tabibu wa matatizo kibao yanayo shindikana kwenye hospital zao naimani sana na tiba asilia kuliko za hospital wenyewe wanauwezo wa kutibia magonjwa ya kufanyiwa oparation kwa dawa za kunywa tu na unakuwa sawa tezi dume hospital ni mpaka oparation lakini kwa wazee wa tiba asilia ni dozi tu ya miti shamba unakaa poa na oparation zao zinasumbua kila siku unauzuria klinic wakati kwa tabibu jj mwaka ni miti shamba unakuwa mzima milele
 
Sijui kama ni kweli au LA. Mimi na mke wangu tulioana na tulikaa miezi 8 bila wife kushika mimba, wife alikuwa anapata maumivu makali sasa siku za hezi mpaka homa so madokta walitushauri azae ili tatizo liishe lakini hakushika mimba. Tulikuwa tunamsikia huyu Dr kwenye TV basi tukafunga safari mpaka kwake. Hatukumkuta yeye ila tuliwakuta wasaidizi wake, wife alipimwa na kukutwa na tatizo la kuto kubalance kwa hormone na kuwa na viuzibezibe kwenye mirija ya uzazi vinavyopelekea mayai yake kuwa weak na kutokuwa na mpangilio maalumu wa hedhi na yenye maumivu. Aliambiwa ni ngumu yeye kupata mimba bila matibabu. Alipewa dawa aina 12 akazitumie kwa miezi 10 ila pindi akihisi tu dalili za mimba asimame kutumia dawa Mara moja. Alitumia zile dawa kwa masharti aliyipewa kwa miezi 3 tu mimba ikanasa. Aliacha kutumia zile dawa, mimba ikakua, akajifungua na sasa mtoto ana mwaka mmoja. Tafakuri yangu, inawezeka dawa za Dr mwaka zimesaidia au ni mpango wa mwenyezi mungu au yote mawili kwa pamoja. All in all namwachia muumba.
Sijui ka ni kweli au la ila dr kasharuka mita mia
 
Dr.Mwaka ni tapeli la karne ya sasa,ni mganga wa kienyeji na wala hajawahi kusomea udaktari.Kazi yake ni kukariri kama kasuku masomo ya uganga na kuyatoa redioni au kwenye runinga.Kama ni kweli ni daktari aweke cv yake hapa.Eti ana mashine ya kugundua magonjwa yote kwa kushika tu na mkono.Hivyo ni viroja vya karne.Pathology,Biochemistry amejifunzia wapi na saa ngapi? Serkali naona inamchelewesha kumshughulikia.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom