Kuna anayewafahamu vizuri ForePlan Clinic ya Dr. Mwaka?

Kwanza ujuwe ni nini maana ya mtu kujiita doctor? kisha hapo utakapo juwa ndipo utasema zaidi.......

Dktr ni profession. ...in medical field ukimaliza masomo ya udaktari kuna viapo...huyu ni mwizi yeye ni mganga wa mitishamba ...kwnn ajitangaze kama gyncllogiste?????
 
Hii n kwa maslahi ya taifa...kuna watu wamesomeshwa n taifa hili n wanajua hayo yafanywayo sio sawa ,huyu jamaa ni tapeli kulitumia jina la dr kwa matumizi yasiyo sahihi hatuwezi fumbia macho....unachukulia piwa kwa vile wewe huzai ..ila kwa wanawake hii ni serius issue

Mkuu watu wana utashi tofauti. Huwezi chagulia mtu pakwenda kupata tiba na kuna magonjwa yameshindikana hata huko hospital, binafsi sio mdau wa hizi tiba asilia ila naamini kuna watu wanapata tiba japo wengi wanaibiwa.

Wanawake wagumba Ni very desperate huwa wanajaribu chochote kile na watu kama mwaka wanatumia fursa hiyo, Lakini serikali inatambua uwepo wa tiba mbadala na inatoa leseni. Acha watu waenda at their own risk

Unayo point katika matumizi ya title Dr. Nadhani sio sahihi kwa yeye kujiita Dr
 
Nilikuwa nafatilia kuhusu huyu anayejiita dr mwaka...kumbe hajasomea n mganga wa kizushi wa mitishamba...mimi nilidhani ni gyncologistie the way anavyojitangaza,inatia hasira sana medicine inachukuliwa kirahisi rahisi tu...

Acha mambo ya kimbea mtoto wa kike....ukishaona mtu amefanikiwa basi wew povu linakutoka maisha yako kuwa magumu sio sababu ya wew kukaza mishipa kutaka kuwaharibia wengine maisha yao waliofanikiwa...jitume sio kutokwa povu kwenye mafanikio ya wengine
 
Dktr ni profession. ...in medical field ukimaliza masomo ya udaktari kuna viapo...huyu ni mwizi yeye ni mganga wa mitishamba ...kwnn ajitangaze kama gyncllogiste?????
Neno Doctor ni neno la kizungu kwa kiswhili maana yake ni ni mganga sasa wewe usishangae Dr mwaka kuita Doctor? mbona Viongozi wenu wa nchi munawaita Ma-Doctor? Je nao pia wamesomea huo U-Daktari shuleni? au munawapa vyeo amabavyo haviwahusu? Wewe ulitaka Dr Mwaka ajiite Jina la Mganga Mwaka? ndio ungeona lingemfaa kuita jina hilo kuliko kutumia jina la kizungu yaani Doctor? Acha hivyo kama una bifu na Dr Mwaka bora sema ili mradi Dr Mwaka havunji sheria zanchi muache awatibie watu. Mbona mimi ninawatibu wateja wa Dr mwaka na wanapona wakati mimi sio Dr?
 
Hivi anadai anatibu wanawake wagumba tu au magonjwa mbalimbali
 
Mzizi mkavu, hawa wanaojiita dr na wakati hawana degree ni kosa tena anakwenda mbali zaidi n kujitangaza anatibu ugumba...yani st?rilit? huo n uwongo hii ni profession..ina ethics zake ...kaoata wapi dheria ya kumfanyia mgonjwa examen gyncocologique ...mana hii inahusisha kumvua nguo mwanamama kwa ajiri y check up,tena anavaa koti la kidaktari kuwahadaa watu...mana asiyejua akiona kavaa koti anajua ni proffession doctor kumbe sio...hilo ndo ttzo langu..serikali iwawekee mipaka hawa watu

Mimi huwa sikubaliani sana na waganga wa mitishamba. Lakini si kwa sababu wanavaa makoti am kujiita kama unavyolalamika.

Utabibu siyo kuvaa makoti ishengom. n awala siyo kujjita jina au kupata degree. Utabibu ni uwezo wa kutibu wagonjwa na kuwafanya warejee katika afya yao sahihi.

Nilitegemea ungesema juu ya utendaji wake wa kazi kwamba anayosema anayafanya hafanyi. Ungetuambia kwa research kwamba umebaini hana uwezo wa kusaidia tusema matatizo ya uzazi ila anaongopa. nk nk. Au ungetuambia anayofanya ni scientifically disapproved AU ina madhara makubwa kwa mgonjwa kwa namna moja ama nyingine, au ungesema hafuati ethicks za tiba kwa abc.

Lakini ukisema anavaa makoti, anajitngaza, bila sababu za msingi, unaonyesha wivu wa kijinga. Matangazo ya makoti yanakuathiri nini wewe kwenye taaluma yako ama wateja wake?

Pengine labda kama hujui, tiba mbadala imepanda kasi baada ya hao unaowaita medical dr kuprove failures. Wemebaki na hayo makoti, na mashine za kupimia watu shingoni lakini hakuna tiba. Mtu yuko diabetic na wanajua halafu wanamtundikia drip za glucose. Hao ndio wanamwuliza mgonjwa anataka aandikiwe dawa gani wakati yeye hata anachosumbuliwa nacho hakijui zaidi ya maumivu; Hao wanaoitwa mgonjwa kazidiwa wodini wanasema "nisubiri nitakuja" halfu wanatoroka au kusema subiri dr wa zamu ijayo yeye muda wake umekwisha. Hao hao wanaotaka wapewe rushwa ili mgonjwa apate huduma za karibu n.k. Hao wanao prescribe wrong medicines and dose kwa wagonjwa wanaend up kufa, hao wanaoona wagonjwa ni tatizo badala ya ajira.

Wangeonyesha competitiveness kwa uhai wa wagonjwa, bila shaka watu wasingehangaika na tiba mbadala. Huji ni kwa kiasi gani imesaidia watu kipindi chote ambacho hakuna serikali. Ninamshauri regulator kuwawekea mazingira mazuri zaidi ya kazi na kuwapa support inayotakiwa ili huduma zao ziwe bora zaidi ili Watanzania wasife kwa kutegemea makoti.

WIVU WAKO WA KIJINGA USIOKUWA NA HATA SCIENTIFIC REASONS BAKI NAO KWENU.

TENA UMENIUDHI KWA SABABU KAMA VILE NAKUONA ULIVYOVIMBA ETI KWA KUWA NAYE ANAVAA MAKOTI MEUPE. UPUMBAVU. MASUALA YA KITAALAM HAYABISHANWI KIPROPAGANDA ishengom. Ukitenda mema hutapata kibali?
 
Last edited by a moderator:

Mbona umetumia nguvu nyingi sana Mkuu kujibu hoja simple tu hii?
 
Last edited by a moderator:
Wazungu wameharibu akili za wengi kwa kukariri bila kufikiri. Simfahamu huyu anayeongelewa wala siwezi kutoa maoni yangu kama anaweza au la. Nitachangia kufuta ujinga wa kudhani kuitwa Dr. Lazima upitie shule zenye mfumo wa wazungu. Nitatoa mifano miwili tu. Hakuna hospitality yeyote inaweza kutibu jino zaidi ya kung'oa au kuziba. Waafrika nje ya mfumo wa wazungu wanatibu hata leo. Mkoa wa Tanga leo hii kuna watu wanaunganisha mifupa iliyovunjika na hospitali zikawaandikia kuikata maana hawawezi kuiunga. Jukwaa hili nina uhakika lina wapo wanaoweza kukiri haya.Hawa waitweje?
 
Hapa kuna watu kweli vichwa vyao vigumu ishengom amekuja na hoja ya maana kwanini aitwe doctor? Wakati yeye ni mganga wa kienyeji. Kuwa doctor lazima usomee kwa miaka 4 hadi 8. Lakini mganga wa jadi unapata maelezo ya kienyeji enyeji tu.
 
Hawa waganga wa kienyeji wanakwenda na wakati walizoea kubandika matangazo yao barabarani sasa wamekuja na hii style ya TV ili kuwashawishi watu kwa ukalibu zaidi mie nazani wako kibiashara zaidi.
 
Mbona umetumia nguvu nyingi sana Mkuu kujibu hoja simple tu hii?

Anaudhi mkuu. Kwanza alidhani ni professional medical dr. Baaday akagundua hana degree ya medical. Halafu badala ya kuhoji competence, anahoji vyeti, anahoji makoti, na matangazo. Halafu anagandamiza as if makoti ndiyo utaalam. Kaniudhi.
 
Hapa kuna watu kweli vichwa vyao vigumu ishengom amekuja na hoja ya maana kwanini aitwe doctor? Wakati yeye ni mganga wa kienyeji. Kuwa doctor lazima usomee kwa miaka 4 hadi 8. Lakini mganga wa jadi unapata maelezo ya kienyeji enyeji tu.

Doctor kikwete amesoma miaka mingapi ili aitwe dr?

Pengine hoja yake ingeleta sense kama angesema kuwe na jina lingine kutofautisha kundi lake na hili. Lakini yeye ameanza ku nullify kwamba kwa nini anajitangaza kutibu ugumba wakati hajasomea. Je kama anatibu ugumba waliokaa vyouni miaka 4 wemeshindwa aitweje? Awe boss wako wa report kwake? Anagombania makoti eti kwa nini anayavaa na kujitangaza. Watu wa maabara wanaovaa makoti nao ni madaktari? Wanaovaa kitchen coats nyeupe nao ni madaktari? Koti ndilo linampa mtu udaktari?

Amechngany sana madesa na picha ilyoonekna na wivu wa kijinga usio kuwa na sababu. Anasahau kwamba hospitali sasa haziina dawa, kuna urasimu na unyanyasaji wa kutisha na tiba mbadala ndiyo inasaidia watu. Badala ya kupendekeza kitengo kiboreshwe ili kupunguz hata matumizi ya foreign currency ku import madawa na kuboresha uwezo wa kutumia mimea yetu kwa tiba sahihi na hata ku export, yeye analeta wivu wa kipumbavu eti makoti. Ujinga mtupu!
 
Dr. Mwaka ameanza majuzi tu mmesha mwona lakni watu kama Maji marefu mnajifanya hamuwaoni kisa ni waziri mtarajiwa
 
Nadhani watu wanachanganya honorary doctorate, medical doctor na doctor of philosophy. Yeyote kati ya hao anatumia title ya Dr. Sasa sijui huyu Mwaka ana uDr upi kati ya hizo ila kama hana hata aina moja basi ni straight forward hafai kutumia title ya Dr. Tusipindishe maneno
 
Kilichomponza ni ile issue ya kudhamini wimbo wa diamond. ..

Ila kihalali ajiite mganga. ..jina la Dr. Awaachie wenzake.

Pia serikali isimamie afya za watu wake.
 
Back
Top Bottom