Maxence Melo
JF Founder
- Feb 10, 2006
- 4,230
- 13,415
Wakuu, kilichotakiwa kufanyika kilifanyika kwa ufanisi (kuimarisha usalama wa data) lakini tulichokumbana nacho njiani kimepelekea maumivu makubwa!
Database yetu ni kubwa kuliko tulivyotarajia, - 30GB hivyo kufanya backup ikabakia salama ilikuwa ni bahati nasibu. Baada ya kufanya marekebisho muhimu na kutaka kuirejesha JF hewani mnamo saa 9 za usiku (kwa muda wa Tanzania) database ilionekana iko corrupted, tulijaribu kila namna tuwezayo kuirejesha sawa lakini ilikuwa ngumu SANA kufanyika vile.
Tumeshirikiana na wataalam wengine toka Marekani kwa malipo makubwa tu, lakini nao wakakiri kushindwa!
Tunasikitika kuwa tumepoteza hoja zote kuanzia saa 7 kamili usiku wa kuamkia tarehe 13 mpaka saa 4 kamili usiku wa tarehe 13 (takribani masaa 21) kwani tulilazimika kurejesha database ambayo ilikuwepo ikiwa safi na mijadala ya mpaka saa 7 kamili usiku wa kuamkia tarehe 13. Muda wote ninaotaja ni kwa nyakati za Tanzania.
Aidha, wote waliojisajili katika kipindi hicho TUMEWAPOTEZA na tunawaomba sana samahani kwani pamoja na jitihada zetu za kuhakikisha hakipotei kitu mambo yameenda tofauti kabisa na matarajio yetu.
Kwa niaba ya wenzangu, tunapenda kuomba radhi kwa usumbufu uliojitokeza kwa kupoteza data hizo na tunafanya jitihada kuona kama kuna ambacho kinaweza kufanikisha kurejesha data hizo ili tuziongeze kwenye database yetu.
Topic ninazoweza kukumbuka kuwa zilikuwa zimeanzishwa na zilikuwa na wasomaji wakubwa ni: Hii ndiyo Richmond ya Kikwete (aloianzisha Mwanakijiji) na ya Water Front Project iliyoanzishwa na Invisible.
Kuna nyingine zaidi lakini siwezi kukumbuka kila kitu. Naomba muda kidogo nilale (walau saa 1) nikirejea nitajibu maswali tutayoulizwa (kama yatakuwepo).
Ahsanteni,
Maxence