Kumiliki laini zaidi ya moja ni ushamba uliokithiri

Kumiliki laini zaidi ya moja ni ushamba uliokithiri

Kesho yake unashangaa kuona namba ngeni inaingia kwa simu (Airtel), kwa sisi wenye vipengele hapa mjini huwa hatupokei namba ngeni kirahisi rahisi. Baada ya 40 missed calls unaamua kumpokelea, kumbe ni Athumani Majaba, halafu analaumu eti hupokei simu
Binafsi ukinipa namba A, halafu ukaja kunipigia na namba B
sipokei hiyo simu labda utume sms au wasap.
 
Nchi hii ngumu sana. Mtu ana line 10 lakini ukimpigia simu hapatikani number zote.
 
Mtoa mada, unafahamu hii mitandao inatoa huduma ya kukopesha? Sasa huwezi kupokelea miamala laini yenye deni, jariby kuwa muelewa kwa hilo🏃
 
Watu wa namna hii wanaudhi sana kama sio kusikitisha. Unakutana na mtu ana namba ya kila mtandao. Day one kakupa let say namba yake ya Voda, wakati anarudisha message unashangaa namba nyingine (Yas), unavumilia, unasave

Kesho yake unashangaa kuona namba ngeni inaingia kwa simu (Airtel), kwa sisi wenye vipengele hapa mjini huwa hatupokei namba ngeni kirahisi rahisi. Baada ya 40 missed calls unaamua kumpokelea, kumbe ni Athumani Majaba, halafu analaumu eti hupokei simu

Kwenye miamala anakutumia namba let say ya Halotel "Utaskia Tuma Humu", majibu ya kuonesha kuwa muamala umefika yanakuja kwa laini ya TTCL

Huo ni uzamwamwa! Nowdays serikali imethibiti utofauti wa huduma za mawasiliano ya mitandao ya simu. Kwa kifupi hakuna mtandao bora kumzidi mwingine, zote ni sawa, MB 245 za Yas ni kwa Tsh. 500 vivyo hivyo kwa mitandao mingine yote, au dizaini hii ya watu ndo wale wanaodanganyika kwa spika za dj maki za "Jipatie laini ya chuo" kwa chuo gani ulichosomea? Shwain

Hakuna kitu kinachonikera na kuchafua simu yangu kama kusave majina Juma Voda, Juma 2, Juma 3, J4 nikiwa na maana ya mtu mmoja
Wengine tunazo kibao wacha tuwe kama ulivyosema kwa faida zetu.
1. Natumia kwa matumizi kuperuzi tu haingii simu yoyote
2. Kwa maswala yangu ya mawasiano ya kawaida
3. Matumizi ya biashara ipo pale ofisini kwa huduma za kiofisi
 
Yeah kibongobongo huwezi kutimiza kila kitu kwa kutegemea kampuni moja lazima utakwama,kiufupi hata akaunti za benki unatakiwa uwe nazo zaidi ya 2 ili kufanya operations zako kiuhakika.
Imagine unataka kumtumia mtu muhamala chap unaambiwa mtandao uko chini kwa hiyo ungoje hadi kesho,So imekaa vipi hiyo kwa mfano mtu mishe zake ni za chaka na amekuja town mara moja kwa ajili ya kutuma pesa kwa hiyo alipie lodge alale hadi kesho yake kwa sababu ya kusubiria mtandao wa kampuni fulani urudi,haimake sense wakati laini ya simu inauzwa buku tu ya nini tujitese.
 
Pamoja na kwamba siungi mkono kuwa na malaini mengi ila kwa mazingira ya kwetu, kuwa na laini mbili naona sio mbaya
Mfano: Kuna mtandao mmoja huku kwetu Ikifika jioni 19h00 hadi 21h00 Internet haifungui kitu....
sasa kama ndio huo unao peke yake na unakazi za kufanya utafanyaje?
 
Itakuwa mishe zako ni kariakoo na kwenda kulala kimara ndio maana,ungekuwa unahusle kama sisi wengine huko vijijini walau usingepata nishati ya kuandika huu uzi.
 
Ukiona ivo wewe ndo mshamba.....mimi nnazo laini4....Airtel na Tigo zipo kwenye kiswaswadu kwa ajili ya kupiga na kutuma msg.....Voda na Halotel ni kwa ajili ya data tu na ziko kwenye simu kubwa....ukiwa na laini nyingi unaenjoy maisha
 
Eneo ninaloishi halotel wako vizuri sana kwenye meseji na kupiga. Ila data haishiki. Voda wapo vizuri kwenye data. Ila kupiga simu changamoto. Utalazimika tu kua nazo zote
 
Back
Top Bottom