Mkuu Phillemon Mikael,
Sehemu kubwa ya maelezo yako umelenga hoja mahususi, lakini sehemu kidogo uliyoteleza, inahamisha mjadala muhimu wa kauli ya Mramba mahakamani akiongozwa na wakili wake.
magazeti yameandika hii habari kuuza ..ukisoma ndani hakuna mahali alipotajwa mkapa bali imetajwa ikulu...ambayo ni taasisi ...inayojumuisha BARAZA LA MAWAZIRI..ambao wanaaapa [kwa namna yeyote kutooa siri za baraza la mawaziri]...na wanasimama kwenye [collective responsibility].........kikwete ,shein ,pinda ...et al walikuwapo kwenye baraza la mawaziri.....ndio maana tunasema hizi kesi ni za kisiasa....hasa zaidi zikichochewa na chuki ya kikwete kwa mkapa......LAKINI KESI ZA NAMNA HII HUISHIA SERKALI KUSHINDWA....KWANI HAZINA MSINGI IMARA!!!....sasa ameshataja baraza la mawaziri..whats next????
Magazeti ni kweli yanaandika kuuza, lakini si yote yanaandika uongo na katika hili magazeti yameandika ukweli. KWa Waziri wa Fedha kusema Ikulu, hawezi kuwa anamaanisha wale walinzi wa mlangoni ama mhudumu wa Ikulu, lazima ana maana ya kuwa ni aliyemteua ndiye anaweza kumpa amri. Uandishi tasfiri unakubalika na ukiondoa hisia zako utaamini hayo.
kama si chuki za kikwete kwa mkapa ..yote yanafanyika kwa baraka zake ....mbona hakuwakamata lowassa,karamagi na ibrahim....ambao ushahidi wao waala si wa kumungunya mungunya?????????
Si ni Kikwete aliyesema "mwacheni mzee wa watu apumzike" ? Si ni Mkapa aliyemwachia JK urais na baadaye Uenyekiti wa CCM? Si ni wasaidizi wengi wa Mkapa wameendelea na JK akiwamo Makamu wa Rais, Dk. Shein? Sasa hizo chuki hapo hazipo na kama zipo hazina uhusiano wowote na kauli ya Mramba kwa kuwa Mramba na Mkapa wana mahusiano ya kikazi na kifamilia kwa muda mrefu na usije shangaa Mkapa amemwambia Mramba asema hayo ili kuokoka. Mramba ndiye anayesema unayoyasema kwamba kesi zao ni za kisiasa na wanakomolewa na Kikwete, sasa hawezi kutumwa na Kikwete amtaje Mkapa.
si ndio yeye alikuwa watu wake kwa maelekezo yake walikuwa wakisimamia mkapa atukanwe kila siku magazetini?????.....then alipoona kumbe kazi ngumu akliwa songea ...akajibaraguza kwa kusema ..anaomba waandishi wamuache mkapa??
Majibu ya juu yanatosha kukwambia kwamba kwa hoja iliyopo mbele ya Mramba kuitaja Ikulu ya Mkapa, hakuna hoja kwa kuwa Mramba hawezi kutumwa na KIkwete kumtaja Mkapa.
visasi tu!!!... leo hii vinapelekea hadi chama cheti imara kama ccm kinageuzwa cha kidini.....umeona wapi ratio za uongozi chamani zimefikia unrealistic representation of the members or country demographic population kiasi huki??...LEO HII KAMATI KUU ASILIMIA 80% SITAFUNI MANENO ...NI WAISLAMU ...WHAT IS THIS MOCKERY???
SAFU ZA VIONGOZI ASILIMIA ZAIDI YA 80%....TAZAMA HADI KWENYE JUMUIA .....ZA CHAMA ........SIJAANGALIA VEMA HALMASHAURI KUU PALE...LAKINI HII HAITUPELEKI PAZURI KAMA TAIFA????...LAZIMA UONGOZI UWEKE RATIO ZETU SAWA UWAKILISHI KIDINI ,KABILA .....HATUNA KAWAIDA YA KUUONGEA WAZI...LAKINI SI WA KUUDHARAU...!....AU MNATAKA TUKIKIE KAMA KWENYA KUANZA KUDAI NAFASI ZA UTEUZI WAZI KIDINI,KIKANDA AU KIKABILA..KIJINSIA??
Hapa ndipo unapopotoka zaidi na unaungana na wale walioandika barua ya wasomaji katika gazeti la Mtanzania wakisema kwamba Umoja wa Wanawake umejaa Waislamu, na Sophia Simba ameteua Waislamu wenzake kasoro Mkiristo mmoja tu, Lucy Mayenga. Kwa mfano mdogo huo wa Wanawake, kwanza Sophia Simba si Muislamu na Lucy Mayenga si Mkiristo. Na hiyo tu inaondoa hoja ya udini kwa kuwa kwanza majina Si dini. Tuna Augustine Ramadhani, Askofu John Ramadhani ambao ni Wakiristu safi, tunao kina Gideon ambao ni Waislamu safi na kadhalika.
Lakini kama unazungumzia Kamati Kuu, rudi katika Kamati Kuu iliyopita na uangalie majina. Angalia wakati wa Mkapa na wakati wa MWinyi then urudi ujenga hoja upya. Uende na Zanzibar ujenga hoja pia.
MAANA KENYA NDIO WAMEFIKA HAPO...HAWAMPI RAIS FURSA KUTEUA KIUTASHI ..AKIJIUZULU KIONGOZI ..KAMA ALITOKA NYANZA ...KESHO YAKE WAZEE WA NYANZA WANAENDA IKULU NA MAJINA YA VIJANA WANAOWATAKA MMOJA WAO NA KUMPA RAIS ....NA INABIDI ATEKELEZE..! WAMEFIKA HAPO BAADA YA WANASIASA KU ABUSE ...FURSA YAO YA KUPANGA SAFU ZA UONGOZI KWA USAWA!![/B]
[/QUOTE]
Hoja za juu zimepunguza nguvu ya hoja yako hapo juu.