KUMEKUCHA, Mramba amtaja Mkapa! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

KUMEKUCHA, Mramba amtaja Mkapa!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Halisi, Apr 17, 2009.

 1. Halisi

  Halisi JF-Expert Member

  #1
  Apr 17, 2009
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 2,810
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  JAmani katika utetezi wake leo mahakamani, Basil Mramba amekiri kuwa yeye ndiye aliyeidhinisha malipo kwa Alex Steward Government Business Corporation ya dola milioni moja kwa kufuata maelekezo ya IKULU ya Benjamin Mkapa.

  Hakumtaja Mkapa lakini alisema alipata maelekezo ya IKULU. Huenda alikuwa na maana ya Baraza la Mawaziri, ambalo baadhi ya viongozi wa sasa walikuwa wajumbe!!! Hapo iko kazi. KUMEKUCHA

  Mramba na wenzake jana walikuwa wakisomewa maelezo ya awali ya kesi hiyo iliyoko chini ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Kisutu, Hezron Mwankenja.

  Wenzake Daniel Yona na Gray Mgonja, walikana baadhi ya maelezo waliyosomewa wakati Mramba alikiri sehemu kubwa.
   
 2. A

  Asha Abdala JF-Expert Member

  #2
  Apr 17, 2009
  Joined: Mar 21, 2007
  Messages: 1,134
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Eeh eheeeee. Mi nilisema hapa, ni mambo yao hao Chama Cha Mafisadi, watu wakanitusi sana kwa kuita chama cha mafisadi. Sasa jina chama cha mafisadi linatumika mpaka magazetini. Na hata mahakama nayo itathibitisha kuwa hiki ni Chama Cha Mafisadi

  Asha
   
 3. Kaduguda

  Kaduguda JF-Expert Member

  #3
  Apr 17, 2009
  Joined: Aug 1, 2008
  Messages: 671
  Likes Received: 281
  Trophy Points: 80

  Pameiva mwaka huu haushi lazima mdomo wa mtu fulani ufunguke tu! Na tutasikia mengi, na wala sintashangaa hata mkuu wa kijiji akitajwa peupe. Maana kama yalitoka ikulu au kwa maana ya baraza la mawaziri mkulu naye si alikuwemo ndani ya hilo baraza? Ngoja tuendelee kutega masikio na kukodoa macho kweny hii sinema. Na huo ndo mwanzo, mengi yaja!
   
 4. Azimio Jipya

  Azimio Jipya JF-Expert Member

  #4
  Apr 17, 2009
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 3,370
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  So far? Soo goood!!!!!

  Wait to here more!
   
 5. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #5
  Apr 17, 2009
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,611
  Likes Received: 3,913
  Trophy Points: 280
  lazima watapindisha tu,watanzani mara zote tnafurahi habari kama hizi, hata kesho Mkap akienda mahakamani na akakubali kuwa aliifisadi nchi tutashangilia sana, achilia mbali akiachiwa huru na kutorudisha mali zetu! wamegundua tuko hivi, watasema kila kitu!

  OUR ULTIMATE GOAL, IS FOR THESE PEOPLE TO RETURNS OUR MONEY, TO GO TO JAIL, AND TO BE HANGED IF POSSIBLE . LET US DO NOT CARE WHAT THEY SAY! everyone knows CCM wote mafisadi, Mramba hata siku MOJA HATA MUANGUSHA MKAPA, SO AS MKAPA HATAMUANGUSHA KIKWETE!

  If really Mkapa could go to jail, then we do not have government! Kikwete must lead the parade!
   
 6. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #6
  Apr 17, 2009
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,601
  Likes Received: 18,631
  Trophy Points: 280
  Nilisema hizi kesi, ni kesi si kesi ili mradi kuurudisha umaarufu wa mpenda sifa. Ukipenda sana kusifiwa, utakuwa tayari kufanya lolote ili mradi nyimbo za mapambio ziendelee kurindima.

  Niliposema serikali has a very weak case against them in the eyes of law, watu walinisakama sana. Nasubiri kesi ianze nithibitishe maneno yangu.

  Hata ile kesi ya BOT, akipatikana mwanasheria makini, atathibitisha we have defective law systeam inayokiuka haki za binaadamu.

  Masikini Liyumba na Mzee wetu wa Kanisa, Mzee Kweka, wanawaonea bure!. Time will tell ninachoshukuru, hii kesi itafanya badhi ya bad laws kuwa scraped from the book of laws!.
   
 7. c

  cesc Senior Member

  #7
  Apr 17, 2009
  Joined: Nov 25, 2008
  Messages: 156
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  mmmhh!!!..hapa kazi ipo..kwanzaaa ndo muvi limeanza..kuna maadui na mastering...lets wait and watch..but it'l b very very interesting
   
 8. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #8
  Apr 17, 2009
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,320
  Likes Received: 5,611
  Trophy Points: 280
  Watamnyamazisha sasa hivi kwa ahadi .......kuwa hizi ni za kisiasa tu....asiropoke maana ni hatari kwa chama na serikali.........yake iliyo madarakani...hiyo ndio dawa yao sasa...watajane wote tuone kama serikali itkivuliwa nguo itafanyaje?
   
 9. rmashauri

  rmashauri JF-Expert Member

  #9
  Apr 17, 2009
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 3,008
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Huu ni mwelekeo mzuri wa hii kesi. Hope hakimu hatapindisha pindisha mambo ili siri zaidi zipatikane tujue huo uozo uliojikita ndani ya CCM na mtandao wake wa wizi na kutojali wananchi wake hata kama watakula nyasi shauri yao. Wakati wa kufanya mabadiliko umefika, CCM nao wapumzike ili watakaokuja wajue kuwa watanzania si mabwege tena na wanataka kuona maendeleo na rasilimali tulizo nazo zinainufaisha nchi si kuibiwa na wageni
   
 10. J

  JokaKuu Platinum Member

  #10
  Apr 17, 2009
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,815
  Likes Received: 5,146
  Trophy Points: 280
  ..je, Mramba ana uwezo wa kuithibitishia mahakama kwamba Raisi Mkapa ndiye aliyemtuma kufanya madudu aliyoyafanya?

  Pasco,

  ..utaratibu ni kwamba client humlipa contractor baada ya project consultant kukagua na kuhakiki kazi iliyofanyika.

  ..hata mimi naona ni vigumu kuwatia Liyumba na Kweka hatiani unless walikiuka maelekezo ya project consultant.
   
 11. Eeka Mangi

  Eeka Mangi JF-Expert Member

  #11
  Apr 17, 2009
  Joined: Jul 27, 2008
  Messages: 3,182
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Tatizo ni watu tunashangilia bila kuelewa. Hapa hamna nini wala nini. Hawa jamaa wanajua technical know how. Wanajua wanachokifanya hawa. Na believe me or not nothing is going to happen here. Tusubiri
   
 12. Dilunga

  Dilunga JF-Expert Member

  #12
  Apr 17, 2009
  Joined: Apr 8, 2009
  Messages: 679
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0

  Sasa mbona umesema kwenye kichwa cha thread kwamba kamtaja Mkapa?

  Hivi mbona Watanzania tumezoea kuongopeana?
   
 13. A

  Alpha JF-Expert Member

  #13
  Apr 17, 2009
  Joined: Aug 30, 2007
  Messages: 614
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  This is Nonsense, How is this good in anyway.

  It's the classic "i was just following orders" defence. It's been used hundreds of times. from the Nazi's concentration camps to Pol Pots killing fields.

  Mkapa has his own case to answer (weather he ever actually gets there is another story). It's pretty obvious that the defense's tactic will be to put the blame on Mkapa's state house knowing very well that that Mkapa is immune from prosecution for this type of crime. Mkapa could very well have agreed to this little arrangement to save his buddies skin.

  If Mramba is allowed to launch such a defense this will all become a huge joke, smoke and mirrors. Mramba should stop trying to lay the blame on other people and take responsibilty.
   
 14. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #14
  Apr 17, 2009
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,188
  Trophy Points: 280
  Ni kweli tumekuwa kama wagonjwa na serikali ya CCM baada ya kutambua hilo imekuja na mpango wa kutoa dozi. Homa inapotupanda serikali hutoa dawa ya aspirin na sisi hupata nafuu na kuanza tena kushangilia. Kwa Richmond tulipewa dozi ya kuundwa kwa kamati ya Mwakyembe na tuliweza kupata nafuu kwa kujiuzulu kwa EL, Karamagi na Msabaha. Kwa EPA tukaandikiwa tena dawa ya kamati ya Mwanyika, Mwema na Hosea na tukaweza kupata nafuu kwa Patel na wenzake kufikishwa mahakamani. Kwa minara ya Benki Kuu tumeweza kupata nafuu kwa Liyumba na Kweka kulala Keko. Sasa imekuwa kawaida ya wananchi kuandikiwa dozi na serikali, bunge na mahakama, zote za CCM, na sisi kama fisi kucheka na kushangilia !!

  Lini sisi wananchi tutaweza kuamka na kutambua kuwa hizi dawa zinatoa tu nafuu na gonjwa liko pale pale. Mwakyembe, Kilango, Kimaro, Sendeka na wengine, ni waandikaji wa dawa zisizotibu - ni kama waganga wasanii ambao hukodishwa hali inapokuwa mbaya. These are like actors on stage who are full of sound and fury but at the end of the day signify absolutely nothing. Wananikumbusha ule usemi wa ukiona vyaelea, vimeundwa na wenyewe - CCM. Hivi leo watuhumiwa wote wakimnyooshea mkono Mkapa ndipo iweje ? Baada ya mkutano wa CCM wa Butiama, nilitegemea wananchi wangeweza kuielewa hili genge la mafisadi lakini wapi - ndani ya CCM kuna walinzi, washambuliaji, waunganishaji wote chini ya mlinzi mkuu - katiba.
  Adui mkubwa wa CCM ni haki na usawa !!​
   
 15. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #15
  Apr 17, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,918
  Likes Received: 83,442
  Trophy Points: 280
  Sakata la Alex Steward: Mramba aitaja Ikulu

  Friday, 17 April 2009 16:34


  Na Grace Michael

  Majira

  ALIYEKUWA Waziri mwandamizi katika Serikali ya awamu ya tatu Bw. Basil Mramba amekiri kutoa vibali vya msamaha wa kodi katika Kampuni ya Alex Steward (Assayers) kutokana na kuridhiwa na Ikulu.

  Mbali na hiyo pia amekana kusababisha hasara kwa Serikali ya Tanzania ya sh. bilioni 11.7 na kusema kuwa hasara hiyo ilisabishwa na mkataba mbovu uliokuwa umeingiwa kwa maridhiano hayo.

  Hayo yalisemwa jana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam mbele ya Hakimu Mkazi Bw. Hezron Mwankenja kupitia wakili wa mshitakiwa huyo, Bw. Herbert Nyange wakati wa usikilizwaji wa awali wa kesi hiyo.

  "Mteja wangu hajaingiza hasara ya mabilioni hayo bali ni mkataba mbovu uliokuwa umeingiwa lakini pia asingeweza kufanya hayo bila ya Ikulu kuridhia na kwa kuwasaidia wapelelezi wakaangalie Hansard ya Bunge ya mwaka 2004," alisema Bw. Nyange.

  Hatua ya kusema hivyo ilitokana na upande wa mashitaka kusoma maelezo yote ya awali ya kesi hiyo ambapo washitakiwa walitakiwa kueleza ni mambo gani wanayokiri na yapi wanayoyakana.

  Kwa upande wa Bw. Mramba alikiri kushika nyadhifa ya juu katika Serikali ya Awamu ya Tatu kama Waziri wa Fedha lakini pia kuandika barua kwa mshitakiwa wa pili, Bw. Daniel Yona aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini kwamba shughuli ya kuingiza Kampuni hiyo ililetwa wakati bajeti ya 2003/04 ikiwa imefungwa hivyo inawezekana kufanyika katika bajeti ya nyongeza.

  Mbali na hiyo pia, Bw. Mramba alikubaliana na kuandika barua namba TYC/M/30/2 ikitoa maelezo kwa Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kuwa ailipe dola za Marekani milioni moja kama fedha za awali katika Kampuni Alex Steward.

  Kwa upande wa mshitakiwa wa pili, Bw. Yona alikubaliana na vipengele vya majina yake na kushika wadhifa wa juu serikalini lakini alipingana na maelezo ya kuandika barua ambayo, Bw. Mramba alikiri kuandika kwake kuhusiana na fedha kupatikana kwenye bajeti ya nyongeza.

  Hata hivyo mshitakiwa wa tatu ambaye alikuwa ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Uchumi, Bw. Gray Mgonja alikanusha maelezo yote na kukubaliana na wadhifa aliokuwa nao.

  Maelezo waliyokana ni kupokea barua kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ikisisitiza kampuni hiyo ilipe kodi kulingana na sheria ya nchi.

  Maelezo hayo yalidai kuwa Bw. Mgonja alimshauri Bw. Mramba kuendelea na zoezi la
  kusaini notisi za msamaha wa kodi kwa kampuni hiyo.

  Baada ya kumaliza kusomwa kwa maelezo hayo upande wa mashitaka uliiambia mahakama kuwa unatarajia kuita jumla ya mashahidi 13 na vielelezo mbalimbali kuhusiana na kesi hiyo.

  Upande wa utetezi uliwasilisha ombi kuhusiana na Bw. Mramba kuruhusiwa kuhudhuria kikao cha Bunge mpaka Mei mosi mwaka huu ambapo mahakama ilikubaliana na ombi hilo. Kesi hiyo itaanza kuunguruma mahakamani hapo Mei 18 mwaka huu.

  Awali washitakiwa hao walifikishwa mahakamani hapo wakidaiwa kutumia vibaya ofisi zao kwa kuidhinisha vibali mbalimbali vya msamaha wa kodi na hatimaye kuisababishia hasara Serikali ya Tanzania jumla ya sh. bilioni 11.7.
   
 16. P

  Petu Hapa JF-Expert Member

  #16
  Apr 17, 2009
  Joined: Jan 2, 2008
  Messages: 714
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Yote sawa, kunyongana siungi mkono.
   
 17. M

  Mwikimbi JF-Expert Member

  #17
  Apr 17, 2009
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,745
  Likes Received: 109
  Trophy Points: 160
  iam a professional quantity surveyor, and i worked with various clients, nashangazwa na hii kesi ya akina liumba

  kuna architect, quantity surveyor na strutural engineer, kazi zote hizo ni kumshauri client kuhusu malopo, ubora wa kazi nk

  sasa hawa akina liumba wanaangukia wapi? yuko wapi web uronu yule quantity surveyor wa kimataifa aliye kuwa akiwashauri benki kuu kuhusu cost implication na of coz alilipwa fee yake almost 2bn?
   
 18. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #18
  Apr 17, 2009
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0

  rmashauri: Na wengine waliopost replies hadi sasa mnakosea lengo hapa ni nini. Ni kwamba Mramba anafikiria kesha save kwani atashikilia maagizo ya Ikulu yalikuwa ya mdomo, siyo ya maandishi, hivyo Mkapa itabidi aitwe mahakamani kutoa ushahidi. Kwa maana nyingine Mramba alikuwa akipokea amri tu.

  Itajengwa hoja kwamba Mkapa hawezi kuitwa mahakamani hadi eti aondolewe kinga, na chombo cha kufanya hivyo ni Bunge, ambalo Wabunge wengi ni wa CCM ambao kwa sababu ambazo hazitaingia akilini, watapinga Mkapa kuondolewa kinga. Kwa maana nyingine, ukiondoa wachache, Wabunge wengi wa CCM wanaona ufisadi ni kitu sawa tu, kinyume kabisa na wanavyoona wapiga kura wao! Hayo ni mambo ya CCM!

  Hata hivyo hili la Mramba kupokea amri kutoka juu halina nguvu sana kama upande wa mashitaka utasimama kidete na kuweza kutaja precedents kadha.

  Kwa mfano, baada ya Vita vya Pili vya dunia, majenerali wa Hitler walikamatwa na kushitakiwa na utetezi wao kwamba walikuwa wanapokea amri tu toka kwa Hitler ulitupiliwa mbali na mahakama maalum zilizokuwa zinasikiliza kesi zao. Bila shaka zipo precednts nyingine zisiziohusiana na masuala ya kivita.... lazima zipo.

  Na suala la 'kinga' kwa Mkapa linatokana na tafsiri potofu tu za vifungu vya sheria na Katiba na mawakili wazuri wanaweza kulisimamia vizuri mahakamani na kulitupilia mbali.
   
 19. bm21

  bm21 JF-Expert Member

  #19
  Apr 17, 2009
  Joined: May 12, 2008
  Messages: 774
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  That's it Man
   
 20. M

  Mwikimbi JF-Expert Member

  #20
  Apr 17, 2009
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,745
  Likes Received: 109
  Trophy Points: 160
  Nurujamii sijakusikia siku nyingi, mseminari liumba unadhani anayo kesi ya kujibu?
   
Loading...