..je, Mramba ana uwezo wa kuithibitishia mahakama kwamba Raisi Mkapa ndiye aliyemtuma kufanya madudu aliyoyafanya?
Pasco,
..utaratibu ni kwamba client humlipa contractor baada ya project consultant kukagua na kuhakiki kazi iliyofanyika.
..hata mimi naona ni vigumu kuwatia Liyumba na Kweka hatiani unless walikiuka maelekezo ya project consultant.
Kitendo cha Mramba kusema ni maekezo toka juu, anamaanisha ni Cabinet na ndio rais na serikali nzima. Maamuzi yoyote ya cabinet yanabeba sura ya collective resiponsibilities, hata kama ni Mramba aliyapigia debe kwenye Cabinet, yakishapita na kutoka, siyo ya Mramba tena, ni ya Rais na serikali yote, huwezi kumsulubu Mramba kwa uamuzi wa Cabinet. Nasisitiza hii kesi hamna kitu
Nikija kwa kina Liyumba na Kweka, plant yote ni defective inakwenda kinyume cha haki za binaadamu kwa kuwashitaki Liyumba na Kweka for the whole cost of Twin Towers.
Kwa mujibu wa charge sheet, inaonekana thamani iliyotumika yote imeonekana kama ni hasara, kitu ambacho sio cha kweli. Majengo yapo na kulikuwa na thamani ya awali iliyokubaliwa na kazi ikaanza, gharama zikazidi kupanda na kupanda mpaka zikafikia hapo zilipofika.
Kesi ya ukweli mbele ya haki, ingewezekana baada ya
Value for money audit ya kilichopo ili kuestablish the true value, baada ya kujua thamani halisi, ndipo unachukua fedha iliyotumika na kuitoa thamani halisi, the diference ndio hasara iliyosababishwa na Marehemu Balali!.
Hasira za serikali ya Kikwete kwa madudu yaliyofanywa na Marehemu Balali ndio imepelekea kumfikisha Liyumba who was only the signatory na Kweka, msimamizi wa mradi.
Haiingii akilini hata kidogo eti yote yahusuyo Twin Tower yalifanywa na Liyumba bila baraka ya Bodi ya BOT!. Hebu angalie structure ya BOT ni ya ajabu sana, hakuna cha bodi wala cha nini, Gavana ndio kila kitu. Ndiye Mtendaji Mkuu wa BOT, ndiye msemaji pekee wa BOT na ndiye Mwenyekiti wa hiyo bodi zuga ya BOT!. Kila kikao sitting ni 2-5m kila mjumbe, nani atakohoa mbele ya Gavana?!.
Ulikuwa ni 'Wizi Mtupu!,na sasa ni kesi zuga japo watu wasio na hatia wanaozea selo!.