Kitendo cha kutamka tu kwamba "JamiiForums ni cross section" ya Watanzania" kinaonyesha wazi kabisa kwamba uko patently out of touch. vibaya mno. Absolutely out of touch.
Watanzania hawana, achilia mbali internet, au computer, na umeme, au kujua matumizi ya computer, au hata kuisogelea au kuiona hiyo computer, ni kwamba hawajui kusoma na kuandika. Abysmally out of touch.
Wewe unaona ni sawa kwa mtu kupotosha taarifa kwa sababu wewe una luxury ya point-and-click ya kusoma kilichomo ndani. Wenzako inabidi wanunue gazeti kuona kama hicho kichwa cha habari ni cha kweli au uongo.
Unaniuliza kama nimefanya survey kujua kama wasomaji huwa wanapotoshwa na hivyo vichwa vya habari au la. Duuuh. Hujui kwamba nchi mwako hili ni tatizo. Huna habari. Huna sensitivity. Again, irreperably out of touch. Wahariri wa magazeti wananiambia, kuhusu swala hili, kwamba vichwa vya habari "vina kazi yake," vinaandikwa hivyo kwa makusudi. Tafsiri (kama uko out of touch kunyaka hapo), wanasema, gotta eat, somebody gotta lie!
Halisi amekosea kusema Mramba amemtaja Mkapa wakati anakiri ndani ya habari kwamba "hakumtaja Mkapa." Sasa kama hakumtaja, kwa nini kwenye kichwa cha thread useme kamtaja? Kuweni wakweli. Na huwezi kusema ni vibaya kumuita mtu mwongo wakati ni wazi hakusema kweli. Na utetezi anaokuja nao ni kwamba eti hata gazeti la Tanzania Daima limeandika hivyo hivyo. Tabloid la Tanzania Daima ndio mwongozo wako?