Kumbukumbu zangu: Majasusi wa KGB walivyowafanya magaidi wa Hezbollah waliowateka wanadiplomasia wao wanne

GodstarTZ

Member
Jan 29, 2020
8
25
.687460/

Picha za video za hivi karibuni zilizokuwa zikionesha jinsi wanahabari wa kimarekani bwana James Foley pamoja na Steven sotloff wakikatwa vichwa na magaidi wa ISIS inanikumbusha stori ambayo ilitokea nchini Lebanon mnamo mwaka 1985.

Mnamo mwezi wa tisa, tarehe 30, mwaka 1985, kundi la watu wenye silaha lilifanikiwa kuwateka nyara wanadiplomasia wanne wa Urusi pamoja na wafanyakazi wa ubalozi wa Urusi nchini Lebanon (Arkady Katkov, Valery Myrikov, Oleg Spirin pamoja na Nikolai Svirsky) katika mji mkuu wa Beirut.

Wakati wa tukio zima la utekaji nyara huo nje kabisa ya majengo ya ubalozi huo, bwana Katkov alijeruhiwa sehemu ya mguu wake wa kushoto.

Watekaji nyara hao walijiita ni "Jeshi la Khaled Al-Walid" pamoja na "Islamic Liberation Organization" (ILO). Kulingana na taarifa za idara ya ujasusi wa nje ya Urusi, kanali Yuri Perfilyev, ambaye kwa wakatu huo ndiye aliyekuwa shushushu mkazi (resident spy ama station chief) wa KGB nchini Lebanon, tukio zima la utekaji nyara lilipangwa na kuratibiwa kwa umakini mkubwa na jasusi katili sana wa magaidi wa Hezbollah bwana Imad Mugniyeh kama kujibu mapigo ya wanamgambo wanaoungwa mkono na serikali ya Syria katika mji wa Tripoli uliopo humo nchini Lebanon. Baada ya kuchukua mateka, magaidi hao wa kishiha wakaitaka kwa nguvu zote serikali ya Urusi kuilazimisha Syria kuacha mara moja kufanya mashambulizi ya kijeshi katika mji wa Tripoli na kuufunga haraka sana ubalozi wake uliopo mjini Beirut.

Ili kudhihirisha ya kwamba hawakuwa na masihara katika kutaka matakwa yao kutekelezwa, ndani ya siku mbili tu, gaidi mkuu Mugniyeh akamuua bila huruma mwanadiplomasia wa Urusi aliyekuwa amejeruhiwa bwana Katkov kwa kummiminia risasi za kutosha kwa SMG na kisha kuutupa mwili wake kwenye dampo la takataka hapo hapo jijini Beirut.

KGB station chief bwana Perfilyev kisha akaamua kukutana na bwana mkubwa Ayatollah Muhammad Fadlallah, kiongozi wa kidini wa washiha waishio nchini Lebanon kisha akamwambia;

"Taifa kubwa kamwe haliwezi kusubiri milele. Tutaacha kusubiri na kutazama na kuamua kuchukua hatua kali zitakazokuwa na madhara yasiyotabirika (mkwara huu......)

Baada ya kuona ayatollah Fadlallah bado tupo kimya, KGB station chief akazungumza kwa ukali sana safari hii akimwambia;

" Hatuzungumzii tu kuhusu watu wa Beirut. Ninazungumza kuhusu miji ya Tehran na Qom ambao ni mji mtakatifu wa washiha pamoja na makazi ya Ayatollah Khomeini, ambayo haipo mbali na mpaka wa Urusi.

Qom ipo karibu sana na Russia na makosa yanaweza kujitokeza na kombora linarusha kwa bahati mbaya. Makosa ya kiufundi yanaweza kutokea kwa bahati mbaya sana na tunaomba Mungu aepushie mbali janga hili"

snowden-russia-fsb
Ayatollah Fadlallah ambaye alionekana anatetemeka sana kutokana na mkwara ule wa boss wa KGB akajibu baada ya kukaa kimya kwa muda mrefu akisema "ninafikiri mambo yote yataenda sawa sawia"

Baadaye mshauri wa karibu wa Ayatollah Fadlallah bwana Hassan akamwambia KGB boss ya kwamba hakuna mtu aliyewahi kuongea na kiongozi wetu mkuu wa dini kwa ukali wa namna hiyo.

Kutumia mbinu ya kutishia kushambulia moja kati ya miji kitakatifu sana ya watu wa dhehebu la shiha ilikuwa ni moja tu kati ya mikakati lukuki ya Urusi katika kutaka kuwakomboa diplomats wake, ila baada ya ukimya kuzidi kushika kasi KGB wakaamua kutoa somo la milele kwa magaidi wote wa kiarabu pale mashariki ya kati. Wanaume wa KGB walifanya ushenzi huu mpaka leo wanaogopwa sana na waarabu;

KGB walimteka mtu waliyejua fika alikuwa ni ndugu wa karibu saaaaana na kiongozi mashuhuri wa Hezbollah. Walimkata vipandevipande vya nyama, kisha wakaweza nyama zile kwenye mfuko na kisha kuvituma kwa viongozi wa juu wa Hezbollah.

Siku iliyofuata KGB wakakamata ndugu mwingine wa karibu sana wa kiongozi wa Hezbollah, wakamfumua ubongo wake kwa risasi, wakaweka kwenye kiroba, kisha wakapeleka mwili wake kwa viongozi wa magaidi hao.

Kama hio haitoshi kuonesha ya kwamba wapo serious sana na kazi zao, wababe wa KGB wakawaambia viongozi wa Hezbollah ya kwamba tunajua walipo ndugu zenu wengine wa karibu kabisa na kwamba wategemee vifurushi zaidi vya maiti ndani ya mifuko ya viroba kama wanadiplomasia hao watatu hawataachiwa huru mara moja.

Baada ya kuonea sasa wamegusa pabaya pasipogusika, viongozi wa Hezbollah wakachukua gari mpya na za kisasa sana aina ya BMW zinazokimbia kwa kasi kubwa sana, wakawabeba wanadiplomasia wale waliobaki hai, kisha kiwapeleka katika ubalozi wa Urusi mjini Beirut.

Tangia siku hiyo, hakuna mwanadiplomasia wala raia wa Urusi aliyewahi kutekwa nchini Lebanon.

Hivi ndivyo KGB ilivyokuwa ilifanya kazi. Walikuwa hawaongei mara mbili mbili.
 
Duuuu !!!hiii kali. Kila mtu ana damu na mtu wake anayempenda. Waligusa mboni za macho yao. kumbe hata suicide senders wanaogopa ndugu zao kuwa mbuzi wa kafara
 
IRAN SIO WAARABU,NI WAAJEMI.HAWANA UHUSIANO KABISA NA WAARABU,HATA YA KUCHANGANYA DAMU,KWA KUOANA.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom