Hezbollah wana nguvu kiasi gani kama Jeshi?

100 others

JF-Expert Member
Aug 5, 2017
3,626
12,057
Hezbollah ilianzishwa rasmi mnamo mwaka 1985 huku lengo kuu ikiwa ni kulinda ardhi ya Lebanon dhidi ya utawala wa Israel kuivamia Lebanon.

Hezbollah ina askari ambao ni muslims, shia, sunni na wakristo.

Hezbollah wapo vizuri hasa katika kuilinda Lebanon dhidi ya uvamizi kama ilivyotokea First Lebanon War na Hezbollah wakafanikiwa kuzuia jeshi la Israel kuivamia Lebanon.

Hezbollah wanafanya kazi kama Professional Military ambao ni organized structured na sio kikundi cha kienyeji kama wanamgambo au kama wale wachunga mbuzi wa Afghanistan kama wengi wanavyofikiri.

Kama nilivyosema Hezbollah wanafanya kazi kama professional military kama majeshi mengine, wana vitengo(army branches) katika.

Infantry
Armor
Artillery
Air Defense
Intelligence
Ordnance
Supply & Transport
Signal
nakadhalika.........

Tofauti kabisa na makundi mengine kama watu wanavyofikiri hasa humu jf, hawa jamaa wanafundishwa mafunzo maalumu na nidhamu, pia wana special forces command ambao ni sawa na kama iivyo Israeli Shin Beth, US Navy SEALS au British SAS.

Kama unafuatilia ukisoma battle moja iliitwa Binte Jbiel, askari 5000 wa Israel wakiwa na support ya anga walishindwa kuteka kijiji kilichokuwa kinalindwa na askari wa Hezbollah 150 tu, ilifikia kipindi wale IDF wakaanza kuwaita wale askari wa Hezbollah kwamba ni mizuka(ghosts), kwa maana walikuwa wanashambuliwa pasipo kufahamu kwa usahihi ni uelekeo upi hayo mashambulizi yanatokea.

Katika battle hilo sio kwamba tu walifanikiwa kulinda hiko kijiji dhidi ya uvamizi lakini pia walisababisha hasara kubwa katika jeshi la Israel, na sababu pekee ambayo ilipelekea Hezbollah wasipate madhara makubwa ni kwa sababu Israel walikuwa wakirusha makombora hovyo.

Hezbollah wana mafunzo kama vile :

Close Quarter Battle
Ninaposema close quarter combat ni ile kunakuwa na mashambulizi/mapigano baina ya makundi mawili inaweza kuwa jeshi dhidi ya jeshi lingine, askari dhidi ya makundi ya kihalifu n.k, aina hii ya mapigano mara nyingi inakuwa ndani ya mita 100, na kinachotumika ni bunduki na vifaa vingine, mfano kama SWAT mara nyingi unaona wanavamia nyumba na kuingia ile tunasema ni Close Quarter Battle.
AC-110520-CQ-9.jpg

Guerrilla Warfare.
Hii ni aina ya vita/mapigano baina ya kikundi flani ambacho yaweza kuwa wananchi wenye silaha, waasi n.k wakipambana na jeshi, police n.k, mara nyingi aina hii ya mapigano inahusisha aina mbali mbali za mashambulizi kama ambush, kushambulia na kukimbia, utekaji, uvamizi na mbinu zingine mbali mbali.

Lengo kubwa la aina hii ya mapigano ni kukwepa makabiliano ya ana kwa ana dhidi ya maadui, hii ni kutokana na kuwa na silaha duni, jeshi dogo au sababu zingine. Au kwa ufupi ni uncoventional warfare unaweza kusoma zaidi mtandaoni, aina hii ya mashambulizi inatumika hata na Navy Seals.
what-is-guerilla-warefare.jpg

Sabotage.
Hii ni ile vita unashambulia miundo mbinu au silaha za adui ili kumdhoofisha, mfano jeshi dogo la askari wenye mafunzo ya hali ya juu (special forces) wanakwenda kushambulia na kulipua daraja ili adui asipitishe silaha na askari, hio ni sabotage, au kushambulia pipeline ya mafuta adui asipate mafuta ili adhoofike, kuna mifano mingi.
Russian-saboteurs.jpg

Espionage
Huuni ujasusi, kwenda kuchukua taarifa kutoka kwa adui na kuzitumia kwa ajili ya manufaa yako ili kunufaika zaidi, au kumdhoofisha adui, aina hii ya ujasusi inafanyika hata katika makampuni yenye ushindani kibiashara, hii inahusisha kuiba taarifa muhimu.
Inahusisha kwenda jeshi la adui kuchunguza aina ya silaha alizo nazo, nguvu aliyo nayo n.k.
how-india-is-behind-russian-espionages-growth-into-its-transnational-form.jpg

Covert Operations
Hii ni undercover operation, ni ile kwenda kufanya tukio pasipo adui kufahamu nani amefanya shambulizi, inaweza kuwa mauaji, utekaji n.k hizi ni aina ya mission ambazo zinapangwa kwa ustadi na usiri mkubwa sana, akili nyingi inatakiwa, mfano mauaji ya Mohsen Fakhrizadeh yule mwanasayansi wa atomiki nchini Iran, ile ni mfano wa covert opertaion.
23388773201_0988b6400c_k-1200x640.jpg

Intelligence Gather
ni ukusanyaji wa taarifa za maadui, hapa kuna mbinu mbali mbali hutumika za upelelezi kama vile kupiga picha, kuhoji n.k mfano US au Russia wanapotumia satellite ku monitor movement za maadui ile tunasema ni intelligence gathering. Au unarusha drones ndogo na kuanza kupiga picha kambi za adui.
mfrack_realistic_photo_of_military_internet_access_b3773517-959b-464b-8fa7-e27090533cbd.jpeg

Counter Terrorism.
kitengo maalumu dhidi ya kupambana na ugaidi, kwa kifupi ni anti-terrorism, hii sina haja sana ya kuelezea.
Kuwa katika kitengo hiki unapewa mafunzo yote yanayohusu kupambana na ugaidi, unawafahamu magaidi kuanzia wanavyofikiri n.k. Mfano Herzbollah walisaidia pakubwa kupambana na ISIS nchini Syria.
PI2G_2F.jpg

Hayo ni baadhi ya mafunzo siwezi list yote nilikua naelezea kwa ufupi tu.

Hezbollah inasemekana wana vitengo kama vitatu vya kiintelejensia, taarifa zaidi kuhusu intelligence yao haifahamiki zaidi kutokana na kuwa na usiri mkubwa.

Wana SIGNT(Signal Intelligence), wana CVTDIV (Covert Division) na CI (Counter Intelligence), wale majasusi wa Jf nadhani wamenielewa, signal intelligence kwa ufupi ni ile kuingilia mawasiliano ya watu au vifaa vya ki electronic, unakuwa unaskikiliza na kupata taarifa za adui.

Counter Intelligence ni ile unajizuia dhidi ya adui yako kupata taarifa zako, kama tulivyosoma hapo juu kuna espionage kwa maana kuwa unakuwa unaishi na jasusi akichukua taarifa zako pasipo wewe kufahamu, sasa counter intelligence division ni kitengo maalumu kwa ajili ya kukabiliana na masuala ya kijasusi

Kutokana na reports mbali mbali Hezbollah walishafanikiwa kuingiza watu wao katika jeshi la IDF, na pia walishafanikiwa kuingilia mawasiliano ya jeshi la Israel kutoka vitengo vya juu kabisa.

Kwa sababu nimchoka kuandika naomba nihitimishe kama ifuatavyo.
Hezbollah ni jeshi lenye nguvu, Hezbollah sio tena kama walivyodanganywa watu kwamba ni Guerrila Unit, wana intelejensia ya hali ya juu na air support wanayo, hivyo Hezbollah ni jeshi kama yalivyo majeshi mengine, watu wengi humu wanafikiri ni kikundi cha wachunga mbuzi milimani kule Afghan. ukisikia Israel inasema Hezbollah akiingia kuisadia Hamas na yeye anaita washirika jua kuna kitu.

Ukitizama kuanzia wanavyovaa, wapo full gear kama IDF walivyo.

Watu waache ushabiki wa hear say, wawe wanasoma, media hazina double standards.

nipo hapa kutoa elimu kuna wajinga wataleta uislamu na ukristo, Hezbollah kuna askari wa kikristo wengi, sio kundi la kidini, bali wazalendo kwa ajili ya kuipigania Lebanon.

lelo3.jpg

Askari wa Hezbollah.

5eb75d7b2d3896976146f5213f1a2dc4.jpg

Askari wa Hezbollah.

Soma pia.
Ni jinsi gani Hezbollah iliweza kushinda vita dhidi ya Israel? (2006)
 
Uislamu umetoka wapi, nazungumzia Hezbollah, nyie ndiye mnaharibu poss za watu, ukafiri na hii mada vimetokea wapi? jeshi la Hezbollah kuna christians wengi tu, Lebanon 32% ni Christians, 31.9% Sunni, 31.2% Shia, hakuna udini hapa master kama huna hoja kaa kimya.
Hana akili kabisa anawaza ujinga mtu unatoa analysis lenyewe analeta udini akili mbovu kabisa hawa ndio akili za taifa teule
 
Hana akili kabisa anawaza ujinga mtu unatoa analysis lenyewe analeta udini akili mbovu kabisa hawa ndio akili za taifa teule
Kabisa mkuu, haihitaji udini kuongea ukweli, wa Tanzania wengi sijui tuna akili gani..
 
Nyie jamaa mnadanganyana sana

Nchi 5 zenye wakimbizi wengi Duniani

1. Uturuki Wakimbizi 3.6M
2. IRAN wakimbizi 3.4M
3. Colombia 2.5M
4. Ujerumani 2.1M
5. Pakistan 1.7M

Nchi 5 zenye wakimbizi Wengi 3 za kiisilamu ila propaganda kibao eti wanakimbilia Ulaya hawaendi Nchi za kiisilamu wakati UNHCR inaonesha otherwise

Sasa Jiulize Afghanistan apige Marekani Zigo la wakimbizi Wabebe Pakistan na Iran.

Syria Wapige Marekani na Washirika Wake Zigo la Wakimbizi Abebe Uturuki.

Ingekua Mimi ndio Erdogan ama Iran ningebeba wote niwapeleke huko huko Israel, Marekani, Uingereza etc haiwezekani wao Wapige Nchi za watu halafu Zigo lote la wakimbizi waachie wengine.
Watu hawapendi kufuatilia mambo yenye ukweli na uhalisia nyuma ya pazia.
 
Ila elimu ni kitu cha muhimu sana,
hayo yote uliyo yaandika hapo yana uhusiano gani na mada hapo juu?

Hivi watz mbona wamekuwa watu wapumbavu kupita kiasi hichi aisee?

Kwa hiyo ukrisito wao ndo umewafanya waweze kutengeneza hizo simu sio? Kama ni hivyo ww hapo umesha tengeneza simu ngapi kutokana Ukrisito wako?

Kila jamii ina mchango wake katika ulimwengu huu punguza ufala.

Hicho kiswahili unacho tumia kila siku kimebuniwa na hao waisilam unao waponda.

Hizo tarakimu yaani 0 to 9 ulizo tumia kusoma kuanzia chekechea mpaka mwisho wa elimu yako na mpaka sasa unazitumia kwenye maisha yako ya kila siku zimebuniwa na waarabu ambao ni waisilam.

Alafu kingine unacho takiwa kujua ni hayo makampuni yapo kibiashara na haya tengenezi bidhaa kwa ajili ya watu wa dini furani na wameajili wataalamu wa dini na jamii zote, hivyo bidhaa unazoona ni ubunifu kutoka watu wa jamii na dini zote.

Mfano makampuni mengi ya kiteknolojia ya kimarekani wabunifu wake wengi ni Wayahudi,Waajemi na watu kutoka Asia ya mbali ambao kimsingi hawana uhusiano na huo ukrisito wako.

Kuhusu wakimbizi kukimbilia Uclaya hilo linakuzwa na vyombo vya habari ebu nenda kwenye vyanzo vya shirika la wakimbizi duniani uone ni nchi gani zinazo hifadhi wakimbizi wengi duniani.
Sahihi sana kiongozi, hata Steve Jobs baba yake ni mtu kutoka Syria.
 
  • Thanks
Reactions: ITR
Nyie jamaa mnadanganyana sana

Nchi 5 zenye wakimbizi wengi Duniani

1. Uturuki Wakimbizi 3.6M
2. IRAN wakimbizi 3.4M
3. Colombia 2.5M
4. Ujerumani 2.1M
5. Pakistan 1.7M

Nchi 5 zenye wakimbizi Wengi 3 za kiisilamu ila propaganda kibao eti wanakimbilia Ulaya hawaendi Nchi za kiisilamu wakati UNHCR inaonesha otherwise

Sasa Jiulize Afghanistan apige Marekani Zigo la wakimbizi Wabebe Pakistan na Iran.

Syria Wapige Marekani na Washirika Wake Zigo la Wakimbizi Abebe Uturuki.

Ingekua Mimi ndio Erdogan ama Iran ningebeba wote niwapeleke huko huko Israel, Marekani, Uingereza etc haiwezekani wao Wapige Nchi za watu halafu Zigo lote la wakimbizi waachie wengine.
Waarabu wanapigana wenyewe kwa wenyewe kwa kuunda vikundi vya kigaidi vya kiislamu kama Islamic state, Hezbollah, Al Qaeda etc.
Magaidi wa kipalestina wamevamia wananchi wa Israel wakaua na wakachukua mateka na kwenda nao ugaidini (Palestina) halafu unategemea waachwe tu?
Gaidi anatakiwa apigwe tu hiyo haina namna.
Ukilea magaidi dunia haitakuwa salama pa kuishi kutakuwa kuna vita kama Sudan na Somalia
- Ona Nigeria, ilikuwa imetulia lakini likaundwa kundi la kigaidi la kiislamu Boko Haram, linachinja watu, kuba na kuua raia ovyo
  • Somalia kuna kundi la kigaidi la kiislamu Al Shabab
  • Gaza kuna kundi la kigaidi la kiislamu la HAMAS, hii vita ya Israel na Gaza wala ingekuwepo
  • Msumbiji kuna kundi la kigaidi la Kiislamu
  • Syria kuna kundi la kigaidi la Kiislamu
  • Pakistan kuna kundi la kigaidi la kiislamu
Iran naye anawasupport magaidi (anafuga magaidi) kwanini hao magaidi wa kiislamu usiwapelekee kwenye nchi za magaidi wenzao?
 
Waarabu wanapigana wenyewe kwa wenyewe kwa kuunda vikundi vya kigaidi kama Islamic state.
Magaidi wa kipalestina wamevamia wananchi wa Israel wakaua na wakachukua mateka na kwenda nao nchi magaidi (Palestina) halafu waachwe tu?
Kagaidi anatakiwa apigwe tu hiyo haina namna.
Ukilea magaidi dunia haitakuwa salama pa kuishi, ona Nigeria, ilikuwa imetulia lakini likaundwa kundi la kigaidi la kiislamu Boko Haram, linachinja watu na kuua raia ovyo
  • Somalia kuna kundi la kigaidi la kiislamu Al Shabab
  • Gaza kuna kundi la kigaidi la kiislamu la HAMAS, hii vita ya Israel na Gaza wala ingekuwepo
  • Msumbiji kuna kundi la kigaidi la Kiislamu
  • Syria kuna kundi la kigaidi la Kiislamu
  • Pakistan kuna kundi la kigaidi la kiislamu
Iran naye anawasupport magaidi (anafuga magaidi) kwanini hao magaidi wa kiislamu usiwapelekee kwenye nchi za magaidi wenzao?
Sasa kama hayo makundi ni Ya kigaidi na ya waisilamu kwanini
1. Yanapewa Silaha na Marekani
2. Wanaenda kutibiwa Israel?
 
Nyie jamaa mnadanganyana sana

Nchi 5 zenye wakimbizi wengi Duniani

1. Uturuki Wakimbizi 3.6M
2. IRAN wakimbizi 3.4M
3. Colombia 2.5M
4. Ujerumani 2.1M
5. Pakistan 1.7M

Nchi 5 zenye wakimbizi Wengi 3 za kiisilamu ila propaganda kibao eti wanakimbilia Ulaya hawaendi Nchi za kiisilamu wakati UNHCR inaonesha otherwise

Sasa Jiulize Afghanistan apige Marekani Zigo la wakimbizi Wabebe Pakistan na Iran.

Syria Wapige Marekani na Washirika Wake Zigo la Wakimbizi Abebe Uturuki.

Ingekua Mimi ndio Erdogan ama Iran ningebeba wote niwapeleke huko huko Israel, Marekani, Uingereza etc haiwezekani wao Wapige Nchi za watu halafu Zigo lote la wakimbizi waachie wengine.
Waarabu wanapigana wenyewe kwa wenyewe kwa kuunda vikundi vya kigaidi vya kiislamu kama Islamic state, Al Qaeda, Hezbollah n.k
Magaidi wa kipalestina wamevamia wananchi wa Israel wakaua na wakachukua mateka na kwenda nao ugaidini (Palestina) halafu waachwe tu?
Gaidi anatakiwa apigwe tu hiyo haina namna.
Ukilea magaidi dunia haitakuwa salama pa kuishi km Sudan na Somalia
  • Nigeria, ilikuwa imetulia lakini likaundwa kundi la kigaidi la kiislamu Boko Haram, linachinja watu, kubaka na kuua raia ovyo
  • Somalia kuna kundi la kigaidi la kiislamu Al Shabab
  • Gaza kuna kundi la kigaidi la kiislamu la HAMAS, hii vita ya Israel na Gaza wala isingekuwepo
  • Msumbiji kuna kundi la kigaidi la Kiislamu la Islamic State (IS)
  • Syria kuna kundi la kigaidi la Kiislamu la ISIS
  • Pakistan kuna kundi la kigaidi la kiislamu
  • Bongo kuna kundi la kigaidi la kiislamu lilikuwa limeanzishwa Kibiti
  • Uganda kuna kundi la kiislamu la IDF wanashilikiana na Al Qaeda linaua watu ovyo, kubaka na kupora mali ovyo.
Iran naye anawasupport magaidi (anafuga magaidi kwanini hao magaidi wa kiislamu usiwapelekee kwenye nchi za magaidi wenzao?
 
  • Una uhakika wanapewa silaha na Marekani?
  • Tangu lini Muislamu akashirikiana na Kafiri?
Ushahidi huu

1. Al qaeda wanatibiwa na Israel kama alivyokiri mkuu Wa Zamani wa MOSSAD alipo kua anahojiwa na akasema Al Qaeda hawajawahi piga Israel, Fikiria tumia hata Iq moja ya Ubongo wako kuna Isis, Al Nusra, Is, Iss, Al Qaeda na makundi kibao ila yanapigana tu Nchi za kiarabu hayagusi Israel Na ipo km kadhaa tu toka kwao. Video hii

View: https://m.youtube.com/watch?v=vweHtxqnh-Y

So Bishana na Mkuu Wa MOSSAD kwamba Hawatibiwi Israel

2. Marekani ndio anasupply Silaha kwa hayo Makundi ushahidi huu

Hapo kumewekwa Manunuzi, viwanda zilipotengenezwa, zikasafirishwa hadi wapi na wamepewa kina nani ushahidi wote upo hapo.

Nasubiria na wewe upinge hizo evidence kwa data.
 
Nyie jamaa mnadanganyana sana

Nchi 5 zenye wakimbizi wengi Duniani

1. Uturuki Wakimbizi 3.6M
2. IRAN wakimbizi 3.4M
3. Colombia 2.5M
4. Ujerumani 2.1M
5. Pakistan 1.7M

Nchi 5 zenye wakimbizi Wengi 3 za kiisilamu ila propaganda kibao eti wanakimbilia Ulaya hawaendi Nchi za kiisilamu wakati UNHCR inaonesha otherwise

Sasa Jiulize Afghanistan apige Marekani Zigo la wakimbizi Wabebe Pakistan na Iran.

Syria Wapige Marekani na Washirika Wake Zigo la Wakimbizi Abebe Uturuki.

Ingekua Mimi ndio Erdogan ama Iran ningebeba wote niwapeleke huko huko Israel, Marekani, Uingereza etc haiwezekani wao Wapige Nchi za watu halafu Zigo lote la wakimbizi waachie wengine.
Wakimbizi hawapelekwi,hujipeleka wenyewe maeneo salama
 
Uislamu umetoka wapi, nazungumzia Hezbollah, nyie ndiye mnaharibu poss za watu, ukafiri na hii mada vimetokea wapi? jeshi la Hezbollah kuna christians wengi tu, Lebanon 32% ni Christians, 31.9% Sunni, 31.2% Shia, hakuna udini hapa master kama huna hoja kaa kimya.
ww ni mpotoshaj , kati ya Israel na Lebanon nan anajilinda dhidi ya mwenzie? je ni nchi ilianza ivamia mwenzie ? WAISLAM MNAPEND UNAFIKI
 
Hana akili kabisa anawaza ujinga mtu unatoa analysis lenyewe analeta udini akili mbovu kabisa hawa ndio akili za taifa teule
analysisi ya kusema Hizbollah inajilinda dhidi ya uvamiz wa israel ? kwamba Israel na Lebenon hujui nan alianza mvamia mwenzie ? waislam ni wanafiki sana
 
Nyie jamaa mnadanganyana sana

Nchi 5 zenye wakimbizi wengi Duniani

1. Uturuki Wakimbizi 3.6M
2. IRAN wakimbizi 3.4M
3. Colombia 2.5M
4. Ujerumani 2.1M
5. Pakistan 1.7M

Nchi 5 zenye wakimbizi Wengi 3 za kiisilamu ila propaganda kibao eti wanakimbilia Ulaya hawaendi Nchi za kiisilamu wakati UNHCR inaonesha otherwise

Sasa Jiulize Afghanistan apige Marekani Zigo la wakimbizi Wabebe Pakistan na Iran.

Syria Wapige Marekani na Washirika Wake Zigo la Wakimbizi Abebe Uturuki.

Ingekua Mimi ndio Erdogan ama Iran ningebeba wote niwapeleke huko huko Israel, Marekani, Uingereza etc haiwezekani wao Wapige Nchi za watu halafu Zigo lote la wakimbizi waachie wengine.
kwahiyo Ulaya hakuna wakimbiz w kiislam? je wanafuata nn huko ?
 
ww ni mpotoshaj , kati ya Israel na Lebanon nan anajilinda dhidi ya mwenzie? je ni nchi ilianza ivamia mwenzie ? WAISLAM MNAPEND UNAFIKI
Hapa hakuna udini, huo ndio ukweli, wakati mwingine ruhusu kichwa chako kupokea ukweli hata kama unaumiza tofauti na hapo ni tabia ya unafiki na uchawi waliyonayo wa Tanzania wengi.

Haihitaji kuwa muslim kusema kwamba Hezbollah wapo vizuri kijeshi, Lebanon Christians wapo wa kutosha, Hezbollah ni jeshi la wazalendo wanaoilinda nchi yao, ni uzalendo sio udini.

Kama una facts lete, kama masuala ya udini tafuta masheikh na wachungaji ukawaulize sijasoma dini yeyote.

Thanks.
 
Back
Top Bottom