Ubinadamu unapo ingia kwenye maslahi ya wakubwa, na kupelekea tafrani

Intelligent businessman

JF-Expert Member
Sep 6, 2022
25,386
51,546
85 Years Ago to date, Sunday, 10 October 1938 Soviet Union, Moscow Siku hii anazaliwa mtoto mwenye akili nyingi sana Jijini Moscow Urusi, Hawa ndio wale watoto ambao huzaliwa mara moja Baada ya miongo kadhaa.

Kwa kuwa alikuwa ni mtoto mwenye akili nyingi, alifanikiwa kusoma kwenye shuke za vipaji hadi chuo kikuu cha Moscow akisoma mahusiano ya kimataifa. Pia alikuwa anaimudu vizuri lugha ya kijerumani. Alipomaliza chuo akapangiwa kazi katika ubalozi wa ujerumani Mashariki mwaka 1961 Mwaka 1961 alirudi Moscow na kujiunga na idara ya ujasusi KGB ambako alipata mafunzo ya utimamu wa mwili, kujihami, ujasusi na matumizi ya silaha.

Mwaka 1966 akapangiwa kazi katika ubalozi wa Denmark jijini Copenhagen. Mwaka 1968 Akiwa Denmark kukatokea maandamano makubwa yakitaka mabadiliko katika nchi ya kijamaa ya Czechoslovakia. Maandamano haya yaliitwa “Plague springs” Umoja wa nchi za kijamaa USSR wenye makao yake makuu jijini Moscow ukaingilia kati kuwatawanya waandamani wale. Nguvu kubwa iliyotumiwa na nchi yake dhidi ya waandamani haikumfuraisha Kachero huyu hivyo akawa ameingia roho ya uasi dhidi ya taifa lake.

Akaanza kutuma ishara kwa mashirika ya kijasusi ya Denmark na Uingeleza kuwa amejitolea kuwafanyia Counter Intelligence dhidi ya Urusi Alijaribu kutuma ishara ya kwanza kwa kumpigia simu mke wake aliyeitwa Yelena ambaye naye alikuwa ni KGB Akiwa na uhakika kuwa serikali ya Denmark ilikuwa ikizifatilia simu za ubalozi wao, akaanza kuongea maneno mengi ya kuishitumu serikali yake ya Urusi na sera zao za kijamaa. Mkewe akawa anampinga huku yeye akishikilia msimamo wake.

Aliamini kama maafisa wa Denmark watakuwa wamesikiliza mazungumzo yale basi watamtafuta.Ishara hii haikuweza kueleweka na majasusi wa Denmark. Majasusi wa Denmark nao walijikuta wanamhitaji kachero huyu baada ya kubaini lazima atakuwa sio afisa tu wakawaida wa ubalozi wa Urusi.

Bahati mbaya nao walimtumia ishara ambazo kachero hakuweza kuzibaini. Maafisa hao walikosea kwa kuhisi huenda Mtu huyu anajihusisha na mapenzi ya jinsia moja hivyo wakamtumia “Shoga” mmoja ambaye alimuomba kachero huyu wapange miadi ya kunywa pombe pamoja kwenye pub fulani. Nia yao ikiwa akikubali kukutana nae ndiye wamshawishi awe mole wao.

Kachero akamtolea nje! Wakati haya yanaendelea, mashushushu wa Uingeleza wakawa wamepewa sifa nzuri kumhusu mtu huyu kupitia mmoja wa wanafunzi aliyesoma naye Moscow. Mwanafunzi huyu aliewaeleza maafisa wa MI6 kuwa kachero huyu anachukizwa sana na sera ya ujamaa Taarifa zake kikawavutia Ukawekwa mtego kumnasa kwa kumtumia mwadadada mrembo mwanafunzi wa udaktari wa meno ambeye alikuwa mchezaji mashuhuri wa vinyoya(badmiton) mcheo ulipendwa sana na kachero huyu.

Kachero huyu alikuwa akinywa, akichati na hata kutoa out na mwanadada huyu lakini hakuwa anamuonyesha hisia zozote za kimapenzi. Hivyo mpango huu haukuzaa matunda. Ikabidi mkuu wa MI6 pale Denmark asonge front mwenyewe.

Mwaka 1974 shirika la kijasusi la Uingeleza MI6 (Military Intelligence Section 6) kupitia mkuu wake nchini Denmark, akamfata binafsi na kumuomba waongee faragha. Akakubali Huu ndio ukawa mwanzo wa mtu huyu ambaye anadaiwa alikuwa na uwezo wa ajabu wa kukumbuka kuanza kazi kama Mole wa MI6 ndani ya KGB ambaye alipewa jina la uficho la SUNBEAM,

Kwa wakati huo ilikuwa ni kazi ngumu sana kumpata afisa wa KGB ambaye angekubali kuuza siri za taifa lake. Ilikuwa ni sawa na kumpeleka mpelezi akafanye upelelezi ndani ya sayari ya Mars. Hii ilikuwa ni kalata iliyochezwa vizuri na mataifa ya magharibi. Taarifa alizokuwa akituma SUNBEAM, ziliishia mikononi wa rais wa Marekani Ronald Reagan zikitoka kwa waziri mkuu wa Uingeleza Margaret Thatcher ambao saa nyingine aliwasiliana nao directly bila kupitia MI6 JINSI ALIVYOKUWA ANAVUJISHA TAARIFA Wakati ule maelekezo kutoka KGB Moscow yalikuwa yakitumwa kwenda Copenhagen kwa njia ya “microfilm” iliyokuwa inawekwa kwenye “diplomatic pouch” Microfilm ni kifaa kama ule mkanda wa picha uliokuwa unatumika kwenye kamera za zamani.
Pia diplomatic bag ni mfuko au begi linalotumika kusafilishia nyaraka za kidiplomasia kuingia au kutoka ndani ya nchi. Kwa sheria za kimataifa begi hili haliruhusiwi kusachiwa.

Kwa njia hii ndio KGB walikuwa wakituma maelekezo ya kijasusi kwenye ubalozi wa Denmark.
Wakati wa mapuziko kwa ajili ya chakula cha mchana, ndani ya nusu saa, kachero huyu angechukua microfilm iliyoletwa na kwenda kumpatia agent wa MI6 ambaye alikuwa akisimama nje ya ubalozi kwa utulivu usiotia mashaka. Agent huyu alikuwa akichukua microfilm na kwenda kuikopi kwenye kifaa maalumu kilichoandaliwa maalumu kwa kazi hii kwenye safe house yao ya karibu. Baada ya kazi hii Agent aliirudisha original microfilm kwa kachero kisha naye angeirudisha mahali pake bila kushtukiwa ikiwa imeshanakiliwa. Kwa njia hii MI6 na CIA waliweza kupata maelfu ya taarifa nyeti za Urusi kuhusu Denmark kama vile majina ya uficho ya operations zao, maelekezo na uchunguzi wao wa siri.

Pia kachero huyu alikuwa anapeleka taarifa binafsi kwenye safe house ya MI6 alipokuwa akienda mwenyewe. Hapa ndipo Sunbeam aliwashangaza mashushushu kwa uwezo wake wa kutunza kumbukumbu kwani alikuwa akifika bila file lolote lakini alikuwa anashuka data toka kichwani kwa uwezo wa hali ya juu.

Alikuwa anakumbuka maongezi aliyofanya na majasusi wenzake na maudhui yake huku akifafanua kwa taaluma ya hali ya juu. Akapewa jina la utani la “Operation download” Miula yake miwili ya kufanya kazi nchini Denmark iliisha mwaka 1978 hivyo akarudi nchini kwake Urusi jijini Moscow.

I will be back, ni ndefu sana.- I mean no malice to nobody.
GHCJ7gpXEAAXfzl.jpeg

Kipande Kinachoendelea
 
View attachment 2918084
Interesting
 
Nakukubali mwanangu, shusha habari za jasusi huyu mbobezi wa nguvu.
 
Episode 2.

Akiwa Moscow akakata kabisa mawasiliano na makachero wa MI6 Alitumia muda mwingi akijifunza kiingereza na pia akikusanya taarifa nyeti za uingeleza na kuwapa mabosi wake ambazo alidai amezipata kutoka kwa watu aliowapandikiza uingeleza.

Kihalisia taarifa zile alikuwa akizipata kwenye open sources kama magazeti nk Taarifa zile kwa lugha ya kijasusi ziliiywa “Chicken feed” kwani hazikuwa na athari mbaya kwa serikali ya Uingeleza. Kutokana na jinsi alivyokuwa akitoa taarifa ambazo wakuu wake waliamini ni “intell” kutoka Uingeleza, aliwashawishi wakuu wake na mwezi june mwaka 1982 Sunbeam akapangiwa kazi ubalozi ya urusi nchini uingeleza.

Naam! Kachero wa Urusi akawa rasmi jijini London akifanya kazi za MI6 Urusi ikiamuamini sasa mtu wao kama “Resident Designate” Hii tunaiita kitaalamu “Home and Away” Alipofika Uingeleza akawashawishi maafisa wa MI6 kupitia wizara yao ya mambo ya nje wafanye juu chini kuwakataa mabosi wake waliopo Ubalozi ili yeye awe bosi aweze kufanya kazi vizuri.

Hili lilifanyika hatua kwa hatua na Sunbeam akajikuta anapandishwa cheo cha Kanali na kufanywa mkuu wa KGB nchini Uingeleza. Naam! Hata maafisa wa MI6 wakambadilishia jina lake la uficho la SUNBEAM Sasa aliitwa kwa jina la uficho la NOCTON na sio SUNBEAM tena Huku CIA sasa wakimuita kwa jina la uficho la TICKLE.
Kazi ya kwanza aliyofanya akiwa London ni kumsanua aliyekuwa anatarajiwa kuwa mgombea wa uwaziri mkuu kupitia chama cha Labor Party bwana Michael Foot kuwa ni mtu aliyekuwa akilipwa na Serikali ya Urusi kufanya ujasusi dhidi ya Uingeleza.

Huyo alikuwa ni Mbunge na Kiongozi wa chama cha Labor. Kachero huyu aliwapa taarifa zile Makachero wa MI6 ambao walisubiri kwanza waone mwenendo wa uchaguzi kama anaelekea kushinda ndio wamlipue kulinda Maslahi ya Uingeleza. Lakini tatizo hili lilijitatua lenyewe kwani waziri mkuu Margaret Thatcher alishinda uchaguzi na Michael foot akalazimishwa kujiuzuru. Kachero huyu alitoa taarifa nyingi na nyeti juu ya mipango ya KGB Lakini alikuja kufanya kazi moja nzuri sana kwa wapenda amani wakati wa Vita baridi. Kwanza taarifa zake zilikuwa zinawafanya rais Reagan na waziri Mkuu Margaret kupunguza makali ya sera zao dhidi ya urusi baada ya kuwahakikishia Urusi haikuwa hostile kama walivyoichukulia.

Kisha akafanikiwa kuwachezesha mziki katika tune moja aliyekuwa rais wa Urusi Mikhail Gorbachev na waziri mkuu Thatcher. Wakati ule mwaka 1984 Gorbachev alikuwa ni katibu mkuu wa chama cha Kimomunisti cha Communist Party na alipanga kuzuru Uingeleza. Kwakuwa sasa NOCTON alikuwa ndiye jicho la KGB nchini Uingeleza, akatumwa akusanye details zote za muhimu kabla na wakati wa Ziara hiyo.
Kwa ufupi ni mashushushu wa Uingeleza ndio walikuwa wakimpa Mole wao taarifa hizi naye akawa anaipa timu ya Gorbachev.
Aliweza hata kutabiri mazungumzo yatakayofata yatahusu nini alivyoamuliwa kufanya hivyo kwa kuwa MI6 walikuwa wanamueleza kila kitu kwa upande wa waziri wao Mkuu. Aliweza hata kumshauri Gorbachev aongee nini wakikutana na Thatcher na hivyo hivyo aliwashauli MI6 wamwambie Thatcher mambo yatakayomfurahisha Gorbachev.

Kazi hii nzuri ilifanikisha sana kubadili mtizamo wa Marekani na Uingeleza dhidi ya serikali ya Kijamaa ya Urusi na ukawa ndio mwanzo wa kuisha kwa vita baridi. Mwaka 1985 haukuwa mzuri kwa Jasusi huyu ambaye si vibaya sasa tukimfahamu kwa jina lake halisi.

Jasusi huyu si mwingine bali ni Oleg Gordievsky Kama una kumbukumbu nzuri kulikuwa na Jasusi wa CIA bwana Aldrich Aimes aliyekuwa anauza siri za CIA kwa Urusi. Ni jasusi huyu ndiye aliwatonya KGB kuwa mtu wanayemuamini sana jijini London ndiye anayewauza. Kwamba mtu huyu ana jina la uficho la TICKLE Kichomi huyu wa CIA akaeleza baadhi ya taarifa walizouziwa na TICLE Kwa maelezo yake, Maafisa wa KGB wakabaini kuwa huyu TICKE si mtu mwingine bali ni Oleg Goldievsky Haraka sana wakaitwa arudi nchini Urusi mwaka huohuo wa 1985 Kachero huyu akajua lazima inawezekana mambo yatakuwa yameharibika Maafisa wa MI6 wakamtaka akatae kurudi Urusi na wao watampa ulinzi. Lakini jamaa alikataa na kusema ngoja akajue walichomuitia.
GHCJ7gpXEAAXfzl.jpeg

I will be back, I mean no malice to nobody
 
Back
Top Bottom