Kumbukumbu ya Sikukuu ya Eid Miaka ya 1960

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
20,922
30,271
SALUM ABDALLAH NA CUBAN MARIMBA CHACHA BAND "MKONO WA IDDI"
Katika utoto wetu tukiisikia nyimbo hii ya Salum Abdallah inapigwa TBC tunajua Iddi imeingia.

Watoto wa kike wako uani wanapakwa hina.

Jikoni unakandwa unga wa maandazi na matayarisho ya kutengeneza kaimati na mapochopocho mengine.

Nyumba nzima ni hekaheka hadi usiku wa manane.

Miaka hiyo jiko halikuwa ndani ya nyumba jiko lilikuwa uani.

Uani ndiko lilipokuwa karo la kuoshea vyombo na kamba za kuanikia nguo; na ua lazima upambwe na mkomamanga na mjengaua.

Wazee wetu walikuwa hawapandi michongoma.
Miti hii haipo siku hizi katika haya mazingira yetu ya mjini.

Alipofariki Salum Abdallah mwaka wa 1965 baada ya pale Iddi ikifika na ukapigwa mwimbo huu radioni mama yake Salum Abdallah akisikia sauti ya mwanae alikuwa akibwabwajika na machozi.

Katika.ujana wao Salum Abdallah alikuwa rafiki ya baba yangu.

Mimi nilibahatika.kumuona Salum Abdallah Mtaa wa Aggrey na Swahili ilipokuwa club ya Cuban Marimba Branch.

(Nyumba hii baadae ikaja kuwa club ya Hiari ya Moyo kundi la ngoma ya Kinyamwezi iliyokuwa ikiongozwa na Saleh Mwinamila).

Salum Abdallah alikuwa kakaa ndani ya club na mwenzake mmoja wakipiga magitaa.

Nakumbuka jina lake akiitwa Almasi.
Sikubanduka hapo.

Huu ulikuwa mwaka wa 1964 nina umri wa miaka 12.
Mwaka mmoja baadae Salum Abdallah akafariki dunia kwa ajali ya gari.

Nyimbo hii ya Mkono wa Iddi inaanza kwa tarumbeta iliyotiwa "mute," ili itoe sauti nyembamba.

Tarumbeta ikisindikizwa na "timing" na maracas inayopigwa kwa ufundi mkubwa.

Kisha inaingia "chorus," wanaingia waitikiaji halafu Salum Abdallah anaingia kuimba.

Salum Abdallah amekwenda kinyume cha kawaida.

Kawaida muimbaji anatangulia kuimba kisha ndiyo inaingia "chorus," yaani waitikiaji nyimbo ikiwa katikati na muziki umekolea.

Hii nyimbo inakaribia miaka 70 lakini kila ninapoisikia hainichoshi na kwangu mimi hunirudisha udogoni siku ya Iddi asubuhi yake na mchana kwenda kushehereka Iddi Viwanja Vya Mnazi Mmoja kwa karagosi na pembea.

Tukiwa ndani ya banda la karagosi kulikuwa na nyimbo tukiimba, ''Karagosi kalewa tembo.''

Tukiwa tuko katika pembea tunaimba, ''Mchimba kisima kaingia mwenyewe, kaingia.''

 
Saleh Mwinamila huyu ndo alikuja kuwa maarufu Kwa kupiga Ngoma nyingi Kwa pamoja??..
 
Karagosi ilikuwa maarufu Sana kidongo chekundu kabla TV hazija take over
 
Saleh Mwinamila huyu ndo alikuja kuwa maarufu Kwa kupiga Ngoma nyingi Kwa pamoja??..
The Boss,
Mwinamila akipiga nyimbo za Kinyamwezi (Khiyari ya Moyo).
Morris Nyunyusa ndiye aliyekuwa akipiga ngoma 10 kwa wakati mmoja.

45128307_711410655886233_8441603975127498752_n.jpg

Mzee Morris

 

Similar Discussions

Back
Top Bottom