Taazia: Yusuf Salum Maleta nahodha wa Sunderland

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
20,921
30,266
TAAZIA: NINAVYOMKUMBUKA YUSUF SALUM MALETA 1960s

Yusuf Salum Maleta ni kaka yangu.

Mwaka ni 1963 nimekuja kutoka Moshi nilipokuwa nasoma na nimefikia nyumbani kwa mmoja wa baba zangu Mzee Abdallah Mtaa wa Gogo No. 6.

Mtaa wa Gogo ni katika mitaa mifupi sana ya Dar-es-Salaam.
Mtaa wa Gogo ndipo ilipokuwa Zawia maarufu Kariakoo ya Sheikh Uwesu.

Sheikh Kassim Juma aliyekuja kuwa sheikh maarufu sana alitoroka nyumbani kwao Bagamoyo kuja Dar es Salaam akiwa mtoto mdogo kwa na nia ya kutafuta elimu zaidi.

Alipofika Kariakoo sokoni hakuwa anajua aende wapi akawa kazubaa na kimzigo chake kwapani anapepesa macho.

Alikuwa hajapata kufika Dar es Salaam.

Msamaria Mwema akamuona pale katoto kadogo na katika kumsaili ndipo akamwambia kaja Dar es Salaam kusoma.

Msamaria Mwema akamchukua hadi Mtaa wa wa Gogo kwa Sheikh Uwesu.

Kilwa Jazz Band ilianza hapa Mtaa wa Gogo nyumbani kwa mama yake Abdul Kigunya.

Nilimuona Abdallah Kassim Hanga kwa mara ya kwanza kwenye nyumba hii ambako akija kucheza bao hapo.

Katika nyumba hii kulikuwa na moja ya barza kubwa za bao Dar-es-Salaam.

Nyingine ilikuwa Mtaa wa Tandamti nyumbani kwa Mshume Kiyate na nyingine Mtaa wa Mafia kwa Maneno Kilongora.

Hawa wote walikuwa wanachama shupavu wa TANU.

Babu yangu Salum Abdallah alikuwa akija Dar-es-Salaam kutoka Tabora yeye akipenda kwenda kucheza pale Mtaa wa Mafia na Congo.

Nawakumbuka watoto wenzangu na nitaanza na mkubwa kwetu sote Amadi Msangamapesa na mdogo wake Hamza na dada yao Mariam, Abdul Kigunya, Ebbie Sykes na mdogo wake Ada.

Amadi ndiye alikuwa akitupeleka pwani na mara yangu ya kwanza kuiona bahari kwa karibu yeye ndiye aliyenionyesha.

Ebbie na Ada wao walikuwa wakitoka makwao wakija mtaani kwetu kucheza.

Amadi tukimwita Amadi Msafi kwa kuwa kulikuwa na Amadi Mchafu.

Amadi alikuwa anasoma Middle School Kitchele Boys mdogo wake Hamza alikuwa Mchikichini.

Hamza akicheza mpira vizuri sana.

Mzee Abdallah alikuwa mtu karimu sana alitoa vyumba viwili kwa wapangaji wake walale watoto wa kike chumba chao na wa kiume chumba chao.

Mtaa huu umebeba kumbukumbu nyingi sana za utoto wangu za mapenzi ya rafiki zangu hao niliowataja na wengine hapo mtaani kama Gopi, Mohamed Kitunguu na ndugu yake Ali "Nakioze" Hussein aliyenifunza kuvua kwa ndoana baharini sehemu za Ocean Road.

Likizo ikimalizika ninapopanda basi la DMT kurudi Moshi nilikuwa natokwa na machozi.

Ilikuwa wakati huu ndipo nilipomfahamu Yusuf Salum yeye kwetu sote pamoja na Amadi Msangamapesa alikuwa kaka yetu mkubwa akisoma Aga Khan Secondary School.

Nyumba yao Mtaa wa Sikukuu na Stanley haikuwa mbali na kwetu Mtaa wa Gogo.

Nyumba ya baba yake Mzee Maleta ikitazamana na nyumba ya Abdul Sykes.

Nyumba ya Mzee Maleta ilikuwa ubavuni mwa nyumba ya bibi yangu Bi. Deborah na akiishi baba yangu mkubwa Augustino Mgone na wanae.

Mkabala wa nyumba hii kwenye kona ndipo ilipokuwa ofisi ya Tanganyika Federation of Labour (TFL).

Ofisi hii ina historia kubwa katika kupigania uhuru wa Tanganyika kwani Katibu Mkuu wa TFL alikuwa Rashid Mfaume Kawawa.

Lakini mimi kumbukumbu yangu si ofisi ya TFL bali duka la Mbaraka kona ya Mchikichi na Sikukuu kulipokuwa kunapigwa Mkwaju.

Nyimbo zake bado nazikumbuka hadi leo.

"Sikujua,
Sikujua kama litatoka jua."

"Kamwambie polisi bangi lipo mfukoni.

Akichelewa atalikuta mdomoni."

Yusuf Salum alikuwa na dada yake mdogo Mashavu huyu alikuwa rika langu na tulikuja kusoma pamoja Kinondoni Primary School.

Mzee Maleta alikuwa na nyumba nyingine Kinondoni kati ya nyumba nzuri mtaani kwa nyakati zile.

Nyumba hii haikuwa mbali sana na nyumbani kwetu.

Mashavu alikuwa akiishii nyumba hii na alikuwa katika wasichana wanaopendeza sana pale shuleni.

Miaka mingi sijamtia machoni Mashavu.

Yusuf Salum sisi wadogo zake tukimuusudu kwanza yuko sekondari kisha sifa zake za uchezaji wake mpira zilikuwa zimeenea.

Wakati huu alikuwa bado hajaanza kucheza Sunderland alikuwa akicheza Kahe Republic timu iliyokuwa na wachezaji vijana hodari.

Yusuf Salum alikuwa akicheza Half Back wa kulia.

Kahe ilikuwa Mtaa wa Mchikichi na Msimbazi.

Toka udogo nikiwausudu sana wakubwa zangu waliokuwa mbele shule mimi bado nipo shule ya msingi.

Sisi bado tuko Shule ya Msingi Yusuf Salum akamaliza shule akaenda Urusi kusoma zaidi.

Tukapoteana na tulipokuja kukutana tena mimi si mtoto tena naishi Kinondoni niko Cargo na yeye kesharejea kutoka Urusi.

Yusuf Salum Maleta akawa mzungumzaji wangu sana.

Ndipo nilipojua kuwa alikuwa bingwa wa mambo ya "signals," yaani mawasiliano na akijua "morse."

Alinihadithia kuwa siku moja alijikuta yuko katika chumba cha polisi na wakirusha taarifa kwa morse.

Katika chumba kile kulikuwa na polisi ambae alikuwa kwa muda mrefu akimwangalia Yusuf Salum muda taarifa zilipokuwa zinarushwa kwa morse.

Yusuf Salum anasema baadae yule polisi alimfuata akamuuliza kama anajua morse.

Yusuf alimkubalia.

"Una maana muda wote uko hapa ulikuwa unatusikiliza?"

Yusuf akamjibu, "Ndiyo."
"Umejifunza wapi?"

Yusuf Maleta akamwambia alisoma shughuli za mawasiliano Urusi.

Kifo cha Yusuf Salum kimenikumbusha kifo cha rafiki yake ambae muda wote walikuwa pamoja miaka ile Mohamed Kokson.

Kokson alifariki mdogo sana miaka ile hata kabla Yusuf Salum hajakwenda Urussi.

Allah awarehemu wote wawili.

Amin.

1705589589218.jpeg
Waliosimama katikati ni Yusuf Salum Maleta kushoto ni Mussa "Libabu" Wambangulu na kulia ni Hassan "Tony British" Mlapakolo.
Chini kulia ni Njunde na kushoto Said Walala.​
 
Inna li Llahi wa Inna Ilayhi Rajiun.

kwenye picha hapo nimekumbuka jina la Mlapokolo tu, kwa sababiu nadhani atakuwa mdogo wake, aliwahi kuolewa na jamaa yangu anaitwa Captain Abdu Kassa (marehem) wa Arusha. Huyo alikuwa Captain wa Boeing 747 za mwanzo za Sudia Airlines.
 
Sheikh Mohamed Said ukiniruhusu ntakupa "surprise" ya Jeddah, Saudi Arabia na family yako nahisi.
 
Kama Mrs. wako aliwahi kusoma Marekani basi tulikutana nae kwa mdogo wangu hapo Jeddah alipokwenda Umrah akitokea Marekani, nadhani ilikuwa late 80's.

Ma shaa Allah kama ni yeye nnaefikiria mimi basi una kifaa cha uhakika hapo nyumbani.
Maalim Faiza,
Ndiye.
Ilikuwa 1987.

Nacheka peke yangu.
Leo Maalim umeniweza.
 
Maalim Faiza,
Ndiye.
Ilikuwa 1987.

Nacheka peke yangu.
Leo Maalim umeniweza.
Ma Shaa Allah, hapana, nadhani nilisoma jina pahala, ulikuwa ukielezea kisa cha Salim Ahmed Salim, nikaona jina ika click nikawa nawaza wapi nalijuwa hili jina. Nikakakumbuka, nikamuuliza mdogo wangu eti unakumbuka jina hili, akanambia anakumbuka sana tena sana, akanikumbusha kuwa hata mimi namfahamu nilikuwaepo kwake wakati alipokuja Umra, akanikumbusha mpaka story tulizokuwa tunapiga, nikamkumbuka vizuri sana. Ni mtu ambae ni ngumu sana kumsahau. Tabaraka Allah.

Hapo Maalim, Tabaraka Allah.

In shaa Allah tutatafuta siku kuja kuwaona.
 
Maalim,
Dunia ndogo hii.
Karibuni sana ndugu zetu.
 
Maalim,
Dunia ndogo hii.
Karibuni sana ndugu zetu.
Ni ndogo sana. Ukimkumbusha nyumba aliyofikia Jeddah atakumbuka, kwa mdogo wangu hapo, ndipo nilipooanana nae, na mimi nilikuwa mgeni kama yeye. Kwa hiyo tukawa hatuonani sana, maana mimi nilishikwa na marafiki zangu wengine Jeddah hapo wakaniondoa kabisa kwa mdogo wangu. Kama unamkumbuka Mohamed Ghaid, kijana wa zamani sana Dar, kwao Morogoro, ni mchezo mmoja na kina Kellow kama unawafahamu. Ndiyo mkewe alinizowa zowa, akanambia mwache mdogo wako mshamba huyo, tukakuoneshe jiji. Lakini nilikuja yeye akiweppo hapo mara mbili tatu, maana hao wenyeji, rafiki zangu wa zamani sana Dar., walikuwa hawanipi hata muda wa kukaa na mdogo wangu.

Huyo mkewe Ghaid, kwao pale kwa Bi Khoula, Livingstone, katikati ya mchikichi na mahiwa. kama unamkumbuka.
 
Ghaidi tunafahamiana miaka mingi.
Nina picha yake tulipiga pamoja Jeddah mwaka wa 1997 sijui iko wapi.

Kellow tunafahamiana miaka mingi.
Siku zimekwenda.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom