Kumbukumbu nzuri kwenye maisha yangu(Baba yangu)

Aaliyyah

JF-Expert Member
Mar 20, 2022
15,822
37,811
Nawasalimu natumaini tuko poa na wagonjwa Mungu atujaalie afya zetu ziimarike.

Leo imekuwa siku nzuri ya kumbukumbu nzuri maishani mwangu
Kama kitu nilibahatika ni kuwa mtoto wake.

Mama aliwahi kunambia kabla ya kuzaliwa kwangu baba yangu alikuwa asiyejali kabisa kuhusu future yake ila baada ya mama kushika ujauzito wangu alibadilika sana.

Nilivyozaliwa na kuanza kupata akili sijawahi kumuona baba yangu akigombana na mama wala kumrushia kibao, mara zote huwa anarudi kazini mapema hata akichelewa huwa lazima ale chakula cha usiku na sisi

Nikiwa na miaka 6 nakumbuka nilipata ajali ya kukatwa na chupa mguuni nikicheza kwenye mvua, niliumia vibaya alinibeba mgongoni kutoka kwa Mfipa hadi Tumbi hakuona aibu wala hakujali watu watamuonaje na alihakikisha napata matibabu tukarudi wote akiwa kanibeba hivyo hivyo 🥰

Kipind hiki cha ugonjwa sikuweza kutembea alikuwa anamsaidia mama kuniogesha akirudi kazini jioni na kunifundisha maana sikuwa naenda shule kabisa

Ilikuwa lazima Kila mwisho wa mwezi arudi na vinywaji na nyama nyingi nyumbani

Alikuwa Mpenzi wa supu na nyama choma hivyo siku hiyo tunabaki mimi na yeye jikoni ananifundisha kuchoma nyama tunapika na ugali mama tunamuita aje kula tu 😍

Licha ya kuwa mkali(jeshi) na kuwa na hasira lakini alikuwa hatoi adhabu Zaidi ya fimbo kwa watoto, alikuwa anahakikisha mnaenda shule smart kufua kila siku na kupiga pasi Ilikuwa ni lazima na akiona unazubaa anakupigia pasi mwenyewe

Nakumbuka alishindwa kula sababu sikuonekana nyumbani kwa muda nilopangiwa, nilicheza kupitiliza alinitafuta sana ile siku na alivyonipata hakuongea chochote zaidi ya kunambia nikalale

Kiukweli maisha yangu na baba yangu yamenifanya niwe positive kila siku kwa wanaume naona nina bahati kulelewa na baba yule pia nilikuwa naona namna anavyopambana kuhakikisha tunaishi vizuri

Alipata ulemavu wa vidole viwili akiwa kazini ila nilielewa ni katika kuhakikisha tunakuwa katika mazingira safi
Sijawahi msikia mama yangu akimsema vibaya hata baada ya kifo chake

Matukio ni mengi sitaki niwachoshe. Kiukweli Nina bahati sana
Natamani watoto wangu wapate baba mzuri kama alivyokuwa babu yao 🥰🥰🥰
Na Mungu awalinde wanaume mnaolea vizuri watoto wenu. Nimegundua namna tunavyolea watoto ndio matokeo ya mienendo na tabia za watoto zinavyopatikana

I didn’t have to go searching for a role model when I grew up, I’ve always had one since the day I was born–my hero dad is my first and only role model.”❤️❤️❤️
 
No love from my daddy, 'cause the coward wasn't there
He went away and I didn't cry, 'cause my anger
Wouldn't let me feel for a stranger
-Dear Mama, 2Pac
 
Baba yangu ni adui yangu namba moja.
Kama umetazama series ya Brigerton, chuki aliyonayo huyo mtu aliyopo kwenye avatar yangu kwa baba yake. Namimi ni hivo hivo.

No love from my daddy, 'cause the coward wasn't there
He went away and I didn't cry, 'cause my anger
Wouldn't let me feel for a stranger
-Dear Mama, 2Pac
Pole sana alikufanyia nn Hadi umchukie hivo
 
Back
Top Bottom