Simulizi mbaya, baba yangu wa Ubatizo Kazikwa leo kijijini kwetu Kisana ila namtakia kila la kheri

sifi leo

JF-Expert Member
Mar 30, 2012
5,013
8,369
Hakika namwombea Pumziko liliro la kheri Mwenyezi Mungu ampokee panapostaili.

Niseme ukweli Baba yangu wa Ubatizo alikuwa Mtu mwema sana,wema wake niliona pale alipo kubali ombi la Bibi yangu kunizaa kwenye Ubatizo ili hali hamjui Mama yangu wala Baba yangu.

Baada hapo mimi niliondoka nikaenda jijini Dsm kwenda kuisaka Elimu, zaidi ya miaka 20 paspo kuonana mwaka juzi nilirudi kijijini na kumkuta Baba yangu wa Ubatizo akiwa mzima wa Afya.

Tulipiga stori nyingi sanaa za hapa na pale katika stori zetu hakusita kunisii kuishi na mke wangu kwa akili na nikiona tumechokana basi nimwachie mji niende nikaanze upya life lisonge ila nisiuze mji nilio ujenga nae,wara nisimfukuze.

Usia wa baba wa ubatizo ulilenga kutaka kunieleza kisa chake yeye na mkewe ambae baada ya miaka 35 ya maisha ya raha waliingia kwenye mtifuano baada ya Baba wa Ubatizo kumfumania mkewe.

Kwa kuwa walisha zaa mtoto mmoja wa kike na watano wa kiume Baba wa ndoa aliondoka zake akatokomea mkoani mwanza wilaya ya sengerema akaanza upya.

Akiwa sengerema aliona bora arudi kwake kwa mashariti ya kuto kula chakula kilichopikwa na mkewe,wala kutofuliwa nguo na mkewe,baya zaidi waligawana milango Baba wa ubatizo wangu,alikuwa akiingilia mlango wa nyuma, na mama akiingilia mlango wa mbele.

Wameishi maisha hayo mtu yyte aliyefika kwenye mji ule hasingejua kama hawa wanandoa wana ugomvi.

Yaani Baba yangu wa ubatizo alikuwa mzungu mweusi yeye alimchekea mkewe kana kwamba hakuna kilichotokea.

Ubaya ni kuwa si watoto wa kike wala wa kiume walio jua nini kilijili dhidi ya wazazi wao.

Uwezi amini baada ya Mama kuona Mume Wake hana muda wa kuelezea kosa la mkewe kwa wanawe,Mama ilibidi apike majungu mabaya yakuwa Baba yangu wa ubatizo aliopoa katoto kakamkimbiza kijijini akaenda kula maisha sengerema sasa zimeisha amerudi nyumbani.

Kwa kuwa mitoto ya siku hizi akili hazimo nayo ikakubaliana na Mama yao wakamtenga Baba yao.

Cha kusikitisha juzi Baba yangu wa Ubatizo wao ni Baba yao wa kuwazaa, kwa kuwa uwa anajipikia hapo nyumbani alitoka kwenye kazi zake za ufundi seremala, akaijinka chakula kabla akijaiva akatoka nje kwa ajili kujisaidia kwenye migomba.

Alipo rudi akakuta ndizi zimeiva akapakua na kula

Walaiiiii! Laaaaura!

Kumbe yasemekana kuna mtu aliingia ndani na kumwekea sumu kwenye chakula kikiwa kwenye mafiga Mzee hamkumuona na Mkewe alikuwa amejifungia Ndani(inasemekana) ila tetesi ni kuwa baada ya kukaa muda mrefu wakilala vyumba tofauti mchepuko wa mke wa Baba yangu wa Ubatizo ulichoka sasa unataka wajivinjari ndani ya mji wa Baba yangu wa Ubatizo ndipo.ulipo.amua kumwekea Sumu Baba wa Ubatizo.).

Na yeye paspo kujua alikula chakula na baada ya kula tumbo lilimuuma sanaaaa kikumbizwa hopstali ya kwanza yaani kituo cha Afya akakosa dawa kupelekwa Rwantege akaaga Dunia.

Baba yangu wa Ubatizo ameaga Dunia na kuzikwa leo kijiji kwake kisana.

Funzo Dunia ya leo Mwana ndoa wako aweza kuwa chanzo cha Kifo chako.

Uzao wako waweza kuwa chanzo cha kifo chako.

Jifunzeni wana jf.
Mimi sifileo Mtoto niliyefiwa na Baba wa ubatizo usikoment kama uwezi kunipa pole.
 
Huzuni kweli, pole kwa kuondokewa na baba wa kiroho, watu Wana roho mbaya kweli kumwekea sumu mwenziwe Kama ye umauti hautomkuta vile.
 
Kwanza pole sana.

Watu wa KATAA NDOA wanachukua point tatu muhimu, nope wanachukua KOMBE kabisa.

Ndoa ni SCAM
 
Alitakiwa aachane na huyo mwanamke tangu mwanzo. Maisha gani hayo sasa...
 
Kwanza pole sana.

Watu wa KATAA NDOA wanachukua point tatu muhimu, nope wanachukua KOMBE kabisa.

Ndoa ni SCAM
NDOA NI UTAPELI KAMA UTAPELI MWINGINE.
chagua kuishi maisha ya furaha kwa kuepuka kitu inatwa NDOA a big scam
 
Pole sana...

Wanawake tuna tabia mbaya sana, tunapika maneno ya kutenganisha wababa na watoto wao...

Pia ni wauaji wanaoua waume zao kwa kuwapa stress mpasuko...

Mungu nisaidie niwe mke mwema...
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom