Kumbukizi: Waarabu walipokojoa Uwanja wa Taifa

SAYVILLE

JF-Expert Member
Mar 25, 2010
5,113
7,863
Wengine inawezekana mmeanza kujua mpira baada ya uwanja wa Mkapa kujengwa. Ngoja leo niwape story moja.

Wakati tunatumia uwanja ambao leo unaitwa wa Uhuru, uwanja ulikuwa katika hali mbaya sana, ingawa kwa macho na mtazamo wetu uwanja ulikuwa fresh tu. Huko ndiyo jina la 'Shamba la Bibi' lilipotokea. Tukumbuke pia kulikuwa na majukwaa mawili tu yaliyokuwa upande mmoja. Upande mwingine na nyuma ya magoli, watazamaji wanasimama!

Siku moja walikuja Waarabu fulani kucheza mechi ya CAF, sikumbuki ilikuwa ni club ya Misri au Algeria. Wakashangaa uwanja wetu ulivyo, na katika kutuonyesha dharau, kuna wachezaji wao wakaamua kukojoa, yaani kujisaidia haja ndogo pale uwanjani.

Ndiyo maana wengine tunapopiga kelele mambo fulani nchini yaboreshwe, ni kuepuka kudharauliwa kunakoweza kuepukika.
 
Back
Top Bottom