Mkuu
Copenhagen DN hapo kwa Mamajusi upo sure kweli?
Nijuavyo mimi, wale Mamajusi walikuwa ni watu wa maeneo mbalimbali ya dunia.....walikuwa kama ifuatavyo;
1.Gaspar aliyekuwa Mfalme wa Sheba alipeleka Ubani.Ubani uliashiria uhusiano wa lile tukio na Mungu
2.Melkiory aliyetoka Arabia alipeleka Dhahabu.Dhahabu iliashiria kuwa Yesu ni Mfalme.
3.Baltazar alitoka Tarse & Egypt alipeleka Manemane.Manemane iliashiria kuwa Yesu atakufa.
Hawa watu walitoka maeneo mbalimbali lakini wakakutana kwa Herode(inasemekana)
Pia hakuna ushahidi kama wote watatu walikuwa wafalme, lakini wote walikuwa Astrologers ndio maana waliweza kusoma nyota ya Yesu na kugundua kwamba haikuwa nyota ya mtu wa kawaida.
[Haya ni maandiko yasiyo rasmi]