Kumbe gari ya kampuni?

Domo ana tatizo ndani ya akili, hivi kwanini anapata sana tabu na walala hoi? anashindana na nani kulazimisha ku prove kuwa yeye ana pesa? kulikua na haja gani mpaka Bill of Lading ya hiyo gari yaka ikafika mitandaoni? Jama ni mshamba mno wa kiwango cha SGR
Wala sio ushamba, hizo exhibition zote unazoona anazifanya mond ni katika kuhakikisha ana maintain his fame, ambayo ni nzuri kwa afya ya kazi yake
 
Ile si V12 mbona hapo mnasema V8.. pia kwakua ni mlipa kodi mzuri kuingiza kwa kutumia company inamsaidia kwenye kupunguza gharama za ushuru.. hata makanisa hufanya hivyo
Mkuu ebu tusaidie kampuni inasaidia vp kupunguza ushuru?! Kwa makanisa, misikiti na non profit organization zilizojikita kwenye humanitarian aids hzo usamehewa kodi ya forodha.
 
Upo sahihi, exemption. Nilichanganya kidogo kwa kulinganisha. Ila mfanyabiashara ambae ni mlipa kodi mzuri inakuwa nafuu sana. Maana yangu kwa kanisa, watu siku hizi wanapitishia gari za thamani kupitia huko kukwepa tozo
Unafuu wa mlipa kodi mzuri unapatikan vipi ktk kulipa kodi ya forodha?! Na wanaokwepa kodi kwa kupitisha magari kwa kupitia makanisa ama misikiti shida inayokuja ww unayefanya hvyo unakuwa sio mmiliki halali coz kadi ya gari itasoma jina la kanisa
 
Mkuu ebu tusaidie kampuni inasaidia vp kupunguza ushuru?! Kwa makanisa, misikiti na non profit organization zilizojikita kwenye humanitarian aids hzo usamehewa kodi ya forodha.
kuna sehemu nimeelezea hii kitu huko juu, ni kwamba ikiwa km mali ya kampuni kodi inayokatwa inakuwa ya jumla kwa assets zote zilizo chini ya kampuni husika, tofauti na ukinunua wewe km ww, kodi ya ushuru itakuwinda kwa hilo gari moja tu!
 
Nyie si ndio mlikuwa mkimdiss asichukue tuzo ya BET mkiongozwa na Lema na wale madada fyatu wa Twitter..!?

Imekuaje tena unaanza kulamba matapishi hata mwezi haujaisha!???

Eti MADADA FYATU wa Twitter, lmao!
 
Domo ana tatizo ndani ya akili, hivi kwanini anapata sana tabu na walala hoi? anashindana na nani kulazimisha ku prove kuwa yeye ana pesa? kulikua na haja gani mpaka Bill of Lading ya hiyo gari yaka ikafika mitandaoni? Jama ni mshamba mno wa kiwango cha SGR
We umeishia la ngapi? Tasnia ya mziki unaijua kweli , ? Unajua nini kipo nyuma ya pazia Mzee ..
 
Hakuna cha ajabu hapo. Matajiri wakubwa hawanunui magari au mali zozote kwa majina yao, wanatumia majina ya kampuni zao ili kupunguza kodi na gharama zinginezo
Yaani wabongo ni wataalam wa kila kitu, jiridhisheni basi kabla ya kuandika kitu kisichokuwa kweli. Kununua kitu kwa ajili ya hanasa/luxury haikupi nafuu yoyote ya kodi iwe kwa kampuni au mtu binafsi, tena ndio unalipishwa zaidi
 
Acha kusema uongo, makanisa yana msamaa wa kodi lkn sio kwa kampuni za kibiashara
Nimeleewesha nilichokuwa na maanisha, kuna watu kwakua ya msaha wa kodi wanapitishia magari kanisani, na kwa kampuni ambazo walipa wazuri wa kodi wana unafuu flani.. ukiwa mtu wa Tax au kama ni mfanya biashara utakuwa umenielewa
 
kuna sehemu nimeelezea hii kitu huko juu, ni kwamba ikiwa km mali ya kampuni kodi inayokatwa inakuwa ya jumla kwa assets zote zilizo chini ya kampuni husika, tofauti na ukinunua wewe km ww, kodi ya ushuru itakuwinda kwa hilo gari moja tu!
Mkuu bado hujanijibu unafuu wa kulipa kodi ya forodha unapatikana vp kwa mali iliyonunuliwa kupitia kampuni. Ukizungumza Assets za kampuni ni vitu kama Majengo, thamani, magari, pikipik na kadhalika sasa hizo zina effect gani ktk ulipaji wa kodi ya forodha?! Kodi ya forodha ni kodi inayokatwa kwa kuingiza bidhaa yoyote kutoka nje ya nchi kulingana na thaman yake regardless kwamba imeingizwa na kampuni ama mtu binafsi. Sasa kama mali imengizwa nchini na kampuni huo unafuu wa kulipa kodi ya forodha unapatikana vp kulinganisha na mali iliyoingizwa na mtu binafsi ?
 
Watanzania wengi hua hatuna utamaduni wa kuappreciate vitu vizuri vya watu wengine au watu waliofanikiwa, huwezi kufanikiwa kama unachuki na watu waliofanikiwa, wapende waliofanikiwa then jifunze na ukubali juhudi zao then na wewe uongeze juhudi zaidi ikiwezekana kawaombe hata ushauri
 
Back
Top Bottom