Kwa wadau wanaoishi Marekani..haswa wa Houston. Kuna tetesi kwamba Dr Tenende wa Houston na wenzake wachache wako mbioni kuandaa mkutano wa diaspora ya watanzania wanaoishi marekani. Cha kushangaza ni kwamba waandaaji hawajafanya jitihada zozote za kuwashirikisha watanzania wengine katika maandalizi ya huu mkutano. Mkutano huu unaandaliwa kinyemela.
Kwa watu wenye data za maandalizi ya huu mkutano, naomba majibu ya maswali yafuayo.
1. Mikutano kama hii huwa na lengo la kuwanufaisha watanzania wote. Kama nia ni hiyo kwa nini watanzania wengine hawajataarifiwa kupitia mitandao ya jumuiya za watanzania katika miji mbalimbali?
2. Balozi Sefue mwaka jana alikuja kwenye mkutano wa diaspora uliofanyika Houston. Baada ya mkutano wa diaspora Sefue alikutana na watanzania wengine. Akaulizwa kwanini mkutano wa diaspora 2008 ulihusisha watu wachache. Alijibu kwamba huo ulikua mkutano wa kwanza na kwamba mikutano ya mbele itahusisha wengi. Sasa tupo 2009 na mkutano huu pia unafanywa kinyemela. Kwanini? Mh. Sefue, tunaomba jibu.
3. Mkutano wa 2009 utafanyika lini?
4. Kwanini waandaaji wanakua "hand picked"? Inasemekana waandaaji wote ni marafiki.
5. Je mafanikio ya diaspora ya UK ni nini. Au tunapoteza muda tu?