Nadhani mimi na wewe tuko pamoja, ila kuna jambo moja ambalo tunatofautiana na hili lile na wananchi 'kujitokeza' kufanya usafi kwenye 'public areas'...Kwa wakati huu naona ni sahihi wananchi 'wajitokeze' kufanya usafi lakini ni wazi hili siyo suluhisho la kudumu...Suluhisho la kudumu ni 'wananchi' wenyewe kubadilika kifikra au 'mindset' kuhusu usafi na pia vyombo vile vinavyowajibika kufanya usafi kwenye 'public areas' vifanye hivyo....Mimi naamini hivi sasa unatengenezwa utaratibu wa namna ya kuwaajibisha wanaohusika kufanya usafi...Na hii ni pamoja na kuwaajibisha wananchi kuhusu masuala ya usafi...kulikuwepo utaratibu ambapo maafisa wa afya walikuwa wanapita kila nyumba kufanya ukaguzi wa usafi, mimi nakumbuka miaka kwenye minne au mitano hivi hapa Dar es Salaam, walikuwa wanapita watu wa serikali za mitaa na kuangalia usafi na kuleta 'demand note' ya mchango wa usafi ambao nadhani ulikuwa sh. 1,000/- hivi kama sijakosea...utaratibu huo ulikufa kwa sababu mbalimbali zikiwemo za kisiasa na pia ubadhirifu wa wanaokusanya fedha hizo na pia wananchi wenyewe kutoonyesha ushirikiano...Lakini usafi ni tabia, sisi wananchi wenyewe tabia zetu ni 'chafu' kuhusu masuala ya usafi..tumejiachia, hatuwajibiki ipasavyo....kufanya usafi kwa pamoja kwa siku za miwsho wa mwezi ni namna mojawapo ya 'kuimarisha' fikra zetu kuhusu usafi, lakini ni wazi huu siyo utaratibu wa kudumu...utaratibu wa kudumu ni sisi wenyewe kwenye familia na jamii kwa ujumla kubadilika pamoja na halmashauri za mitaa, miji, manispaa na serikali kuwajibika ipasavyo kwa mambo mengi kuweka sheria kali, kusimamia sheria hizo, kuchukua hatua na kadhalika.
Kuhusu suala la houseboy na housegirl kama hawawajibiki ipasavyo...jibu lake ni simple...wewe mwenyewe, mkeo, mumeo na watoto wenu mtafanya usafi, na kumwajibisha hlousegirl huyo ikiwemo hatua ya kumwachisha kazi na kumwajiri mwingine....Lakini, comrade, siamini kuwa housegirl/houseboy anaweza akaacha kuosha vyombo na kukujibu kuwa 'vyombo anachafua nani'...Ikifikia housegirl/houseboy anafanya na kusema hivyo ujue wewe na familia yako mna matatizo...ziko nyumba nyingine zinawafanya housegirl/houseboy kuwa ni kama watumwa...wanafanyishwa kazi kuanzia saa 11.00 alfajirimpaka saa 6.00 usiku...mshahara wanalipwa kiduchu labda chini ya 50,000/- kwa mwezi na hawalipwi kwa kisingizio kuwa wanawekewa...ma-housegirl/houseboy hao hata mahali pa kulala ni shida..na chakula wanakula peke yao tena basi wanakula jikoni huku familia ikila mezani...yaani ma-housegirl/houseboy wanafanyishwa kazi kama watumwa...kuaripiwa, kupigwa, kutukanwa, kunyanyaswa na kadhalika. Ni dhahiri ma-housegirl/houseboy wa aina wanajenga chuki na ni lazima waje wakujibu hovyo na pengine hata kukufanyia jambo baya kabisa...Ndivyo ilivyo hata kwa wafanyausafi...ukipita mitaani utakuta akina mama wanafanya usafi hawana hata vifaa wala gloves, unawaona wamekata tama ya maisha...watu wanapita hata kuwapa salaamu tu hawatoi, watu wanawaona wale wanaofanya usafi kana kwamba wamelaaniwa, ni wachafu hawapaswi kuheshimiwa na kadhalika...watu wa namna hii hawawezi kuwa na moyo wa kufanya kazi kwa bidii, watafanya usafi kidogo na kuondoka zao kwanza awali ya yote mshahara wao ni mdogo sana...Mimi huwa napita mitaani wakati mwingine huwa nawaona hao akina mama na vijana wanaofanya usafi na waliokata tamaaa ya maisha...inasikitisha sana...Kwa hiyo tunahitaji serikali makini na inayowajibika, serikali hii ya awamu ya tano ina mwelekeo huo ingawa imeanza kupigwa vita kwa hatua inazochukua...wameanza kuiita hii ni serikali ya maigizo, mara ya udikteta na kadhalika...kwa hiyo tuna safari ndefu sana katika kuijenga nchi hii.