Kulazimishana usafi ni halali kikatiba?

Kulazimishana usafi ni halali kikatiba?

badala yaa kulazzimisha watu wafanye wangekuwa wanakaagua usafi kwani swala la usafi ni wajibu wa kila mtu kwa kila siku na sio kulazimishana
 
Nimeangalia taarifa ya habari ya ITV muda huu, nimeona wanajeshi wa JWTZ wakisimamisha magari na kulazimisha abiria kushuka na "kufanya usafi" kwa agizo la serikali. Kwamba jumamosi ni siku rasmi ya usafi. Je hii kitu ina uhalali gani kikatiba? Mbona kama ni udikteta?
Nijuavyo jukumu la usafi wa public areas ni la serikali kupitia manispaa/jiji na tunalipia kodi kwa hilo. Iweje serikali ilazimishe wananchi kufanya shughuli zake, tena kwa kutumia jeshi ambalo kikatiba ninavyojua kazi yake ni kulinda mipaka tu? Hii ni halali? Kama sitaki kukubali amri hiyo je nitashitakiwa kwa kosa lipi mahakamani?
Umoja wetu ndio ukombozi wetu
 
Ndio usafi unaozungumzwa ni wa public areas, ndio maana wanakukamata barabarani na sio nyumbani kwako au kwenye biashara yako. Kwa kawaida unatakiwa kuwajibika kwa usafi nyumbani kwako kwa kuwa wewe na familia yako ndio mnachafua hapo, vile vile kwenye mtaa inabidi wakazi wa hapo muwajibike vile vile kwa kuwa nyinyi ndio wakazi wa hapo. Hata mnaweza kuchanga na kuweka utaratibu wa watu wa usafi.
Lakini hili la kulazimisha kuwa watu wasafishe popote pale watakapokutwa na jeshi wewe unaona ni ustaarabu? Huwezi kumlazimisha mtu afanye usafi eneo la public kwa sababu yeye hayuko responsible na uchafu mahala hapo. Ndio maana tunafanya collective responsibility kwa kulipa kodi manispaa/jiji mahsusi kwa ajili hiyo.

Umezungumza vizuri, nimependa namna ulivyojenga hoja...hata hivyo inawezekana pengine kama watu wangekuwa wamejikita kwenye usafi wa maeneo yao, wasingeguswa na jeshi au chombo chochote cha dola...mimi nafahamu watu wengine ni wabishi tu, nyumbani kwao kuchafu na hata mtaani kwao ni kuchafu, sasa baadala ya kufanya usafi wanazurura tu...sasa basi hao 'wakikamatwa' na 'kulazimishwa' kufanya usafi kwenye 'public areas' mimi siwaonei huruma...mimi nakaa au kuishi katika eneo ambapo mwenyekiti na serikali ya mtaa hutoa tangazo kuwa watu wafanye usafi kwenye maeneo yao..na wenye shughuli au maeneo ya biashara nao hufanya usafi kwenye maeneo yao...biashara na shughuli nyingine katika eneo letu huanza saa 4.00 asubuhi, wote tumekubali utaratibu huo na tunaipongeza serikali kwa hilo...lakini wako ambao kwa mfano jeshi, taasisi za vyuo na kadhalika wakiwemo wananchi wa kawaida hitikia mwito wa kwenda kufanya usafi kwenye 'public areas', na hakuna anayelalamika'...na awali ya yote huko kwenye usafi mnakutana na watu mbalimbali na kujenga 'mshikamano' hukumkifurahi, kucheka na kadhalika...

Kuhusu maeneo ya 'public areas' na hoja kwamba mtu asilazimishwe kufanya usafi pale kwa kuwa 'hayuko responsible na uchafu mahala hapo' nadhani ni hoja ambayo haina mashiko. Ni kweli tunalipa kodi ili manispaa wafanye shughuli zao zikiwemo za usafi...lakini pia tunafahamu pia matatizo yetu kuhusu utendaji wa manispaa na pia namna watu wanavyokwepa kulipa kodi...hivyo basi inawezekana manispaa zinaelemewa na hata wakifanya usafi bado watu wanaendelea kuchafua kwa makusudi na moja ya sababu ni kwa kuwa wapo manispaa wa kufanya usafi. Nadhani mtazamo huu siyo sahihi. Tuhimize usafi kwa kuwaambia manispaa wafanye usafi lakini na sisi pia tuwasaidie kwa kufanya usafi kutokana na 'tabia zetu mbaya' za kuchafua mazingira.

Nadhani umeshawahi kusafiri kwenye mabasi yawe ya kwenda mikoani au usafiri wa daladala mijini. Utaona watu wanakula karanga, miwa, mikate, chips na kadhalika, na wakimaliza kula tu, utaona wanafungua dirisha na kutupa nje uchafu. wanafanya hivyo licha ya ukweli kuwa katika mabasi kuna chombo cha kuhifadhi uchafu na kondakta anatangaza kuhusu uwepo wa chombo hicho.

Sisi watanzani lazima tubadili 'mindset' zetu na kama hatubadiliki tulazimishwe kubadilika. Kwa hiyo, kwa maoni yangu, Jeshi 'kuwakamata' wale wanaozurura siku ya usafi ni sahihi kabisa. Maendeleo hayaji kwa kubembelezana na kuzungumzia ustaraabu, haki za binadamu na kadhalika. Nchi zote zilizoendelea zilifanya hivyo kwa kuwepo sheria kali katika jamii, na vyombo husika vikiwemo vya dola kama jeshi kuwa mstari wa mbele kuwashughulikia wanaokiuka.
 
Kwanza acha kudhani, yaliyotokea hayapingiki. Pili hoja hapa ni kwamba usafi wa maeneo ya umma (yasio majumba ya watu) ni la serikali. Hii ndio maana kuna watu maalum walioandaliwa kwa ajili ya kufanya usafi. Raia wanalipa kodi ili kugharamia watu hao. Kama watu hao hawawajibiki na kufanya uchafu kulundikana hovyo mitaani tunapaswa kuwawajibisha hao na sio kuhamisha majukumu yao kwetu. Vile vile tunapaswa kusimamia sheria za kudhibiti utupaji taka hovyo ili wachafuzi wa mazingira wadhibitiwe. Kulazimisha raia kufanya usafi wa maeneo ya public kwa maoni yangu ni serikali kukwepa kuwajibika. Hata wewe haiwezekani uajiri housegirl au houseboy wa kufanya usafi ndani kwako, halafu asipofanya usafi wewe bosi ndio uanze kuhangaika na mkeo/mmeo kufanya majukumu ambayo tayari mnayalipia!

Comrade, nashukuru nimependa hoja zako, ingawa baadhi nitatofautiana na wewe...ni kweli tunapaswa kudhibiti sheria za kudhibiti utupaji taka ovyo ili wanaochafua mazingira waadhibiwe..hapo, naungana mkono na wewe...ni kweli wako maalum waliowekwa kufanya usafi lakini ni kweli pia watu hao hata wakifanya usafi haipiti muda tayari uchafu unakuwa umerundikana tena...sababu yake ni kuwa watu au sisi wananchi wenyewe hatuwajibiki ipasavyo, tuna tabia mbovu ya kutupa taka ovyo kwa kuwa 'wapo watu maalum wa kufanya usafi'...ninatofautiana na wewe kwa hoja yko kwamba 'kulazinsiha raia kufanya usafi wa maeneo ya public ...ni serikali kukwepa kuwajibika'. Kwanza, ieleweke kuwa wanaochafua maeneo hayo ya public ni sisi wenyewe wananchi, kwa hiyo na sisi pia tunawajibika kwa eneo hilo la public. Tunawaona wenzetu wanachafua mazingira hatuwachukulii hatua kwa kuogopana na 'kuheshimina'.. Hapa Dar es Salaam wakati wa mvua wako watu ambao hutoka maofisini kwao kwa nguvu kwenda majumbani kwao kwa lengo moja tu nalo ni lile linaloitwa 'kufaulisha' vyoo vyao ili uchafu uchanginyike na maji ya mvua..Hii iko kila mahali Dar es salaam-Sinza, Kariakoo, Ubungo, Manzese, Magomeni na kadhalika na kadhalika..watu wa aina hii wenye tabia za ajabu wanafahamika lakini majirani hawawasemi wala 'kuwachongea' kwenye vyombo husika...sasa hapo utalaumu pia serikali????!!! na awali ya yote serikali ni sisi wenyewe wananchi.
 
Haya ndio matokeo ya kubana matumizi, hawataki kuwekeza ktk matumizi ya teknolojia ya kisasa ktk kuiweka miji na majiji yetu safi kwa kukwepa gharama,wanakimbilia kuwalazimisha raia watumie mafyekeo,mifagio,majembe,makoleo kusafisha maeneo kwasababu ndio njia ya gharama nafuu zaidi. Kwa mwendo huu wa kubana matumizi kwa serikali hii naona kama ni sawa na gari lililowashwa na kuendeshwa kinyume nyume kwa kasi kubwa, yaani kuelekea kule linakotoka.
 
Umezungumza vizuri, nimependa namna ulivyojenga hoja...hata hivyo inawezekana pengine kama watu wangekuwa wamejikita kwenye usafi wa maeneo yao, wasingeguswa na jeshi au chombo chochote cha dola...mimi nafahamu watu wengine ni wabishi tu, nyumbani kwao kuchafu na hata mtaani kwao ni kuchafu, sasa baadala ya kufanya usafi wanazurura tu...sasa basi hao 'wakikamatwa' na 'kulazimishwa' kufanya usafi kwenye 'public areas' mimi siwaonei huruma...mimi nakaa au kuishi katika eneo ambapo mwenyekiti na serikali ya mtaa hutoa tangazo kuwa watu wafanye usafi kwenye maeneo yao..na wenye shughuli au maeneo ya biashara nao hufanya usafi kwenye maeneo yao...biashara na shughuli nyingine katika eneo letu huanza saa 4.00 asubuhi, wote tumekubali utaratibu huo na tunaipongeza serikali kwa hilo...lakini wako ambao kwa mfano jeshi, taasisi za vyuo na kadhalika wakiwemo wananchi wa kawaida hitikia mwito wa kwenda kufanya usafi kwenye 'public areas', na hakuna anayelalamika'...na awali ya yote huko kwenye usafi mnakutana na watu mbalimbali na kujenga 'mshikamano' hukumkifurahi, kucheka na kadhalika...

Kuhusu maeneo ya 'public areas' na hoja kwamba mtu asilazimishwe kufanya usafi pale kwa kuwa 'hayuko responsible na uchafu mahala hapo' nadhani ni hoja ambayo haina mashiko. Ni kweli tunalipa kodi ili manispaa wafanye shughuli zao zikiwemo za usafi...lakini pia tunafahamu pia matatizo yetu kuhusu utendaji wa manispaa na pia namna watu wanavyokwepa kulipa kodi...hivyo basi inawezekana manispaa zinaelemewa na hata wakifanya usafi bado watu wanaendelea kuchafua kwa makusudi na moja ya sababu ni kwa kuwa wapo manispaa wa kufanya usafi. Nadhani mtazamo huu siyo sahihi. Tuhimize usafi kwa kuwaambia manispaa wafanye usafi lakini na sisi pia tuwasaidie kwa kufanya usafi kutokana na 'tabia zetu mbaya' za kuchafua mazingira.

Nadhani umeshawahi kusafiri kwenye mabasi yawe ya kwenda mikoani au usafiri wa daladala mijini. Utaona watu wanakula karanga, miwa, mikate, chips na kadhalika, na wakimaliza kula tu, utaona wanafungua dirisha na kutupa nje uchafu. wanafanya hivyo licha ya ukweli kuwa katika mabasi kuna chombo cha kuhifadhi uchafu na kondakta anatangaza kuhusu uwepo wa chombo hicho.

Sisi watanzani lazima tubadili 'mindset' zetu na kama hatubadiliki tulazimishwe kubadilika. Kwa hiyo, kwa maoni yangu, Jeshi 'kuwakamata' wale wanaozurura siku ya usafi ni sahihi kabisa. Maendeleo hayaji kwa kubembelezana na kuzungumzia ustaraabu, haki za binadamu na kadhalika. Nchi zote zilizoendelea zilifanya hivyo kwa kuwepo sheria kali katika jamii, na vyombo husika vikiwemo vya dola kama jeshi kuwa mstari wa mbele kuwashughulikia wanaokiuka.

1. Kwa taarifa niliyoiona watu hawakushurutishwa kufagia majumbani mwao wala nje ya nyumba zao bali maeneo public ambayo inawezekana kabisa hayawahusu, fikiria wewe uwe unakaa kimara unakwenda zako posta, usimamishwe kuzibua mitaro pale ubungo!
2. Kwenye suala la mabasi/daladala etc, yote hayo ni kweli, tuna ustaarabu wa kutotunza mazingira. Lakini zipo sheria ambazo zinambana mhusika moja kwa moja badala ya wote kiujumla. Mbona Moshi wameweza?
3. Napingana na wewe kabisa kusema kuwa watu wanazurura siku ya usafi. Sheria yenyewe ya uzururaji ni miongoni mwa sheria kandamizi. Kwa maoni yangu huwezi kumkamata mtu saa 3 asubuhi katika nchi ambayo inaendelea kama Tanzania, kwa kisingizio cha uzururaji iwe 'siku ya usafi' au la. Hivi kweli kuna mtu anayeendesha gari anaweza ku-fit description ya mzururaji? Ni bora hata ungesema wafungwa watumikie vifungo vyao kwa shughuli hiyo kidogo ningekuelewa.
4. Nchi gani hizo unazosema wewe, zilizoendelea unazozijua ambazo zilitumia jeshi lao kulazimisha walipa kodi kufagia barabara?
5. kuna suala lingine la fairness, kwa mujibu wa katiba raia wote ni sawa. Hivyo suala hili kama ni sheria linatakiwa liguse kila mtu. Sijaona hata chembe ya utaratibu ambao suala hili litakuwa na usawa. Hakuna standard definition ya "usafi", hivyo sijui ili mtu uhesabike kuwa umetimiza wajibu wako unatakiwa utimize masharti gani. Je nikishafanya huo "usafi" nitapewa cheti/tiketi ya kuonyesha nimefanya? Au bado nitakamatwa tena kwa vile muda hujaisha iwapo nitaendelea na safari?
Na pia sijaona sisitizo kuwa hili jambo ni kwa wote. Nimeona abiria wakishushwa kwenye mabasi kwa mabavu ya jeshi, lakini sijaona abiria wa ndege wakishushwa! Nimeona raia wa kawaida sijajua viongozi nao ni vipi.
 
Nimeangalia taarifa ya habari ya ITV muda huu, nimeona wanajeshi wa JWTZ wakisimamisha magari na kulazimisha abiria kushuka na "kufanya usafi" kwa agizo la serikali. Kwamba jumamosi ni siku rasmi ya usafi. Je hii kitu ina uhalali gani kikatiba? Mbona kama ni udikteta?
Nijuavyo jukumu la usafi wa public areas ni la serikali kupitia manispaa/jiji na tunalipia kodi kwa hilo. Iweje serikali ilazimishe wananchi kufanya shughuli zake, tena kwa kutumia jeshi ambalo kikatiba ninavyojua kazi yake ni kulinda mipaka tu? Hii ni halali? Kama sitaki kukubali amri hiyo je nitashitakiwa kwa kosa lipi mahakamani?
Kwani kuwa mchafu na kuhatarisha jamii kuangamia kwa magonjwa ikiwemo kipindupindu ni halali??
Tumekua wachafu hadi tumeuzoea uchafu na kuona kuwa tukilazimishwa kufanya usafi si halali na ingepaswa kuwepo katika katiba.
Swala la usalama wa raia limefafanuliwa vizuri katika katiba. Usalama ni pamoja na kutokuwepo kwa magonjwa yoyote ikiwemo yale yanayo sababishwa na kuzagaa kwa taka ngumu na taka maji. Swala la usafi wa mazingira lipo kikatiba na ndiyo maana limitungiwa sheria yake na Bunge letu.
Tumefikia kulazimishwa kufanya usafi kwa sababu ya ukaidi wetu wa kutofanya usafi wa mazingira yetu ili hali tunazalisha taka kwa kila shughuli tufanyayo ikiwemo kitendo chetu cha kula chakula.
 
Nimeangalia taarifa ya habari ya ITV muda huu, nimeona wanajeshi wa JWTZ wakisimamisha magari na kulazimisha abiria kushuka na "kufanya usafi" kwa agizo la serikali. Kwamba jumamosi ni siku rasmi ya usafi. Je hii kitu ina uhalali gani kikatiba? Mbona kama ni udikteta?
Nijuavyo jukumu la usafi wa public areas ni la serikali kupitia manispaa/jiji na tunalipia kodi kwa hilo. Iweje serikali ilazimishe wananchi kufanya shughuli zake, tena kwa kutumia jeshi ambalo kikatiba ninavyojua kazi yake ni kulinda mipaka tu? Hii ni halali? Kama sitaki kukubali amri hiyo je nitashitakiwa kwa kosa lipi mahakamani?
Hivi nyie bawacha mbona ni taka taka sana? Hivi watu wakifa na kipindu pindu nyie si ndio huwa wa kwanza kutoa lawama kwa serikali?

Hivi mna akili timamu kweli?
Usafi ni lazima ikiwezekana watu wachapwe viboko kabisa!
 
wewe ndio unaonekana kuwa totally biased upande wa maamuzi ya serikali. Kwani mkuu unavyojua wewe serikali inapata wapi fedha za matumizi mbali na kodi yangu na yako? Upotevu wa kodi ni responsibility ya serikali, wizi wa makontena, wafanyakazi hewa...yote hayo ni majukumu ya serikali. Nitumie mfano wako wa makontena, je itakuwa sawa kutenga siku maalum kwa kila mwananchi kwenda kulinda bandarini ili makontena yasiibiwe? Huku ukisisitiza kuwa ulinzi ni jukumu letu sote?
Usafi ni lazima kama hutaki hama nchi kabisa ....
 
Mkubwa sema kwa kufafanua vizuri ueleweke, kwa hiari na lazima ipi?

Na swali la nyongeza kwako ni hili; unajua unachoongea hapa na kujadili au ni mradi unaandika tu?

Utalazimishaje watu waliotoka majumbani kwao kuelekea ktk shughuli zao na matatizo yao mbalimbali kufanya usafi ktk maeneo ambayo siyo yao? Wale wamiliki wa maeneo hayo wanakuwa wako wapi?

Mathalani una appointment somewhere na unapaswa ufike saa 1:30 au 2:00. Uko ktk usafiri wako wa gari au baiskeli au pikpik au unatembea kwa miguu or whatever. Umetoka nyumbani kwako umefanya usafi au umeacha watu wanaendelea na usafi.

Ghafla unakutana na askari wa JWTZ wanakusimamisha na suti yako na wanakuambia tunafanya usafi ktk mitaro hii au hospitalini hapa...jiunge nasi na unapewa ufagio.

Unawaambia, nawahi kazini au interview au kukutana na clients wangu wa biashara....hawakuelewi wanakulazimisha kushika fagio kuwafanyia watu wengine usafi wa maeneo yao huku wewe shughuli zako zikikwama. Hebu jaribu kufikiri kwa akili pana, kwamba hivi hili lina make sense yoyote kweli?

Ningependa kuliona hilo Tangazo la kulazimisha watu kufanya usafi linasemaje hasa.....yaani limekuwa drafted ktk namna ipi ili kuepusha mambo kama haya!!

Maana ipo siku tutakuja kuambiwa tukadeki ofisi za mkuu wa mkoa au kufyeka nyasi zinazozunguka jengo la ofisi yake na ni lazima!!
Usafi ni lazima Bawacha mlimuita sana JK dhaifu sasa mmeletewa mliye muhitaji kelele za nini?

Kama huna uwezo wa kufanya usafi na hutaki ni bora uhame nchi lasivyo utafanya kwa lazima ikiwezekana utatandikwa!
 
Comrade, nashukuru nimependa hoja zako, ingawa baadhi nitatofautiana na wewe...ni kweli tunapaswa kudhibiti sheria za kudhibiti utupaji taka ovyo ili wanaochafua mazingira waadhibiwe..hapo, naungana mkono na wewe...ni kweli wako maalum waliowekwa kufanya usafi lakini ni kweli pia watu hao hata wakifanya usafi haipiti muda tayari uchafu unakuwa umerundikana tena...sababu yake ni kuwa watu au sisi wananchi wenyewe hatuwajibiki ipasavyo, tuna tabia mbovu ya kutupa taka ovyo kwa kuwa 'wapo watu maalum wa kufanya usafi'...ninatofautiana na wewe kwa hoja yko kwamba 'kulazinsiha raia kufanya usafi wa maeneo ya public ...ni serikali kukwepa kuwajibika'. Kwanza, ieleweke kuwa wanaochafua maeneo hayo ya public ni sisi wenyewe wananchi, kwa hiyo na sisi pia tunawajibika kwa eneo hilo la public. Tunawaona wenzetu wanachafua mazingira hatuwachukulii hatua kwa kuogopana na 'kuheshimina'.. Hapa Dar es Salaam wakati wa mvua wako watu ambao hutoka maofisini kwao kwa nguvu kwenda majumbani kwao kwa lengo moja tu nalo ni lile linaloitwa 'kufaulisha' vyoo vyao ili uchafu uchanginyike na maji ya mvua..Hii iko kila mahali Dar es salaam-Sinza, Kariakoo, Ubungo, Manzese, Magomeni na kadhalika na kadhalika..watu wa aina hii wenye tabia za ajabu wanafahamika lakini majirani hawawasemi wala 'kuwachongea' kwenye vyombo husika...sasa hapo utalaumu pia serikali????!!! na awali ya yote serikali ni sisi wenyewe wananchi.
Mkuu sababu zote za kuwapo uchafu haziwezi kuwa justification ya utaratibu huu wa kijima. Nashindwa kuelewa ni kivipi huoni ukwepaji wa majukumu unaofanya na serikali. Ni kweli uchafuzi wa mazingira unafanya na wananchi wenyewe. Lakini ni kipi ambacho serikali kina wajibu nacho na hakifanywi na wananchi? Turudi kwenye definition ya serikali. Serikali ni watu ambao sisi wananchi tunawateua kuendesha mambo yetu kwa niaba yetu. Serikali yenyewe ni wananchi! Hoja zako zinafanya kama vile serikali ni dubwasha tofauti sana na wananchi na haliko responsible kwa ajili yetu.
Nirudi kwenye mfano wangu kuwa unapoajiri housegirl/houseboy pale nyumbani ili aoshe vyombo, hivyo vyombo anachafua nani? Si wewe? Je ni haki kwa housegirl/houseboy huyu kutotimiza wajibu wake wa kuosha vyombo halafu wewe ulazimike kufanya kazi hiyo wakati unamlipa mshahara, halafu jibu liwe "kwani vyombo anachafua nani"?
 
Hivi nyie bawacha mbona ni taka taka sana? Hivi watu wakifa na kipindu pindu nyie si ndio huwa wa kwanza kutoa lawama kwa serikali?

Hivi mna akili timamu kweli?
Usafi ni lazima ikiwezekana watu wachapwe viboko kabisa!

Ukianza kuchapwa viboko wewe it's well and good!!

Mimi itaisha miaka mitano ya huyu jamaa yenu na kamwe hawezi kunilazimisha ujinga huu!!
 
Usafi ni lazima Bawacha mlimuita sana JK dhaifu sasa mmeletewa mliye muhitaji kelele za nini?

Kama huna uwezo wa kufanya usafi na hutaki ni bora uhame nchi lasivyo utafanya kwa lazima ikiwezekana utatandikwa!

kha! wewe aliyekuambia kila criticism to Magufuli lazima inatokea Chadema ni nani? Wewe hilo jina la Ruttashobolwa umeiba wapi? tukikukuta laivu wenyewe lazima tukuchape, kabila letu hatunaga watu wenye akili kama zako🙂
 
Sidhani kama hawa vijana walipokea amri kutoka juu wafanye hivyo. Ni akili zile zile walizonazo askari wa majeshi mengine. Bado tunayo safari ndefu kufuta ujinga na poor reasoning ya wanaovitumikia vyombo hivi. Tatizo ni mifumo inayowaandaa.
We taka taka usafi si hiari ni lazima na ikiwezekana utapigwa! Siku ya usafi imesha rasimishwa ....
 
Attachments

  • Capture - Copy.PNG
    Capture - Copy.PNG
    49.5 KB · Views: 40
  • Capture2 - Copy (2).PNG
    Capture2 - Copy (2).PNG
    52.2 KB · Views: 43
  • Capture3 - Copy.PNG
    Capture3 - Copy.PNG
    47.7 KB · Views: 43
  • Capture4 - Copy.PNG
    Capture4 - Copy.PNG
    36.4 KB · Views: 41
Ifike mahali kodi tunayolipa itumike kufanya usafi.

Mimi hata siku moja siwezi kufanya usafi kwa amri inayotolewa na mkuu wa nchi au mkuu wa wilaya au mkoa.
Labda uendelee kujifungia ndani lakini ukikatiza mbele yao usafi utafanya na ikiwezekana utapigwa kabisa ili uwe na adabu!
 
Jukumu la usafi ni la kila mtu na serikali pia.
Jukumu la mtu binafsi ni kuangalia mazingira ya kwenye maeneo ya nyumbani kwake yapo safi, anatupa taka zinapotakika zitupwe na analipa kodi ipasavyo ili huduma zipatikane
Jukumu la serikali kupitia manispaa ni kuhakikisha uchafu unakusanywa na na kupelekwa kwenye jalala mbali na makazi ya watu na pia kutoa elimu kwa watu kuhusu umuhimu wa usafi wa mazingira.

Haya mambo ya kuteremshana kwenye mabasi kusafisha ni mambo ya kipuuzi sana na hayaendi na karne hii
 
binadamu hawajawahi kuridhika tangu kuumbwa kwa dunia. mtake mtafanya msitake mtafanya ngoja twende kwa mtindo huo kwanza kum## nyi
 
Back
Top Bottom