Kulazimishana usafi ni halali kikatiba?

Kulazimishana usafi ni halali kikatiba?

Duh, kwani JWTZ wanahusishwa na haya mambo pia?
Tumewah onya nchi kuendeshwa kwa kampeni, haya ni mambo ya ujamaa na ni laana mbaya sana kama mtuvanaelipa kodi bado aje afanye mannual work ya kusafisha mazingira?
Kuna haja gani kuipa hii serikal kodi kama hata usafi wa mitaa lazima tufanye kampeni, had madawat kampeni, njaa kampeni, sukari nk....
Tunarud kwenye ujima tukiangalia na macho yetu hivi hivi......
This is unncessessary disturbance, atypical in any civilized society....face palm...
Kweli ni ujamaa huu sasa..
 
Kituko kingine hapa wanajeshi walikuwa wanawalazimisha wachina na wahindi washuke kwenye nagari yao kufanya usafi. Raia mmoja akawa anatumia simu kupiga picha Tukio hilo ambalo lilikuwa public. Wanajeshi wa JWTZ wakamnyang'anya simu yake wakaipasua waka mpiga kidogo yule raia alikuwa na mtoto mdogo anayekadiriwa kuwa na miaka miwili hadi mitatu wakampeleka polisi wakashinda huko hadi sisi tunaondoka kwenda kumsikiliza mkuu wa Mkoa. Hatujui yule mtoto alipata japo chakula au chai.
Watu wanaoitikia kwa hiyari maagizo ya viongozi wap waheshimiwe. Mimi siku nyingine sitashiriki kampeni zinazohushisha JWTZ
Hapo sasa tunafikisha ujumbe gani kimataifa? ni bora wangemfanyia hivyo mbongo hilo lingeishia humu humu sisi hayo tumeyazoea lakini hilo swala akilifikisha kwenye ubalozi wa nchi yake linaweza kusababisha mzozo mkubwa·
 
Huu ni udikteta unaojijenga siku na siku. Kimsingi, unavyomsimamisha mtu afanye usafi(kwa lazima) unajua yupoje kiafya? Serikali tunailipa kodi, wanapeleka wapi hela zetu?
 
Imeingizwa na kuwa sheria ya mazingira sasa unashitakiwa ukikataa kufanya usafi na kuna fine sh 2000 hadi mil 2....na kifungo hadi miaka 7!
Haya ndio madhara ya kuchagua viongozi wasio na uwezo. Nchi hii inafahamika kuwa kwa sehemu nyingi za kazi wanatumia 45 hours work week ikimaanisha hata Jumamosi watu wana shifti ya kazi. Na wale wenye biashara binafsi wengi wanafungua Jumamosi full day na ni walipakodi wazuri. Je serikali itapiga marufuku kazi zote hiyo Jumamosi ya mwisho wa mwezi watu wakafanye usafi? Kwa nini wanasheria wetu wakubaliane na amri hizi ambazo zinakiuka katiba? Ni lini tutapata kiongozi mstaarabu atakayetambua kuwa hakuna kitu cha bure hata kufanya usafi ni gharama pia
 
Utashtakiwa kwa kula pilau na kunywa Heineken at the same time. You feel me?
 
Unachanganya mambo, sijui umefikiaje conclusion kuwa kupinga hili suala maana yake ni kuunga mkono uchafu. Hoja hapa ni kuwa kuna mgawanyo wa uwajibikaji. Usiposafisha eneo lako la biashara unachukuliwa hatua kwa kuwa unakuwa na wajibu wa moja kwa moja kwa usafi wa hapo. Lakini usafi wa mazingira ya umma ni jukumu la serikali/manispaa/jiji na wafanyakazi wa kusimamia hilo wapo. Hii ni kazi professional. Dunia iliyostaarabika haiwezi kumsimamisha mtu kaulamba zake, chini ya ulinzi wa JESHI na kumlazimisha ghafla ashike fagio na kufagia barabara! Kama wewe unasema hiyo ndio katiba basi sawa, inatosha kukuelezea wewe ni msomi kiasi gani wa hiyo katiba!
Haya mambo ya kutoka pamoja kufanya usafi ni katika kuzoeshana kumiliki mazingira yetu. Hii akili ya kusema hayo ni maeneo ya umma na serikali ndiyo yenye wajibu ni kukwepa majukumu kama mwananchi.
Yaani bora uwe unakaa kimya kuliko kuchefua watu. Yaani kitendo cha mara moja kwa mwezi kujumuika na wenzio kwa saa zisizo zidi tatu kuangalia swala la usafi katika eneo lako kwa faida yako na jamii yako unaweka pingamizi? Hivi umesomea ujinga au kupata maarifa.
Wakati mwingine hii ndiyo sehemu ya kufahamiana kwa wanajamii wa mtaa husika na kujuliana hali.
 
Nyumbu kama hawawezi kufanya usafi kwa hiari , wafanye usafi kwa lazima
 
Nimeangalia taarifa ya habari ya ITV muda huu, nimeona wanajeshi wa JWTZ wakisimamisha magari na kulazimisha abiria kushuka na "kufanya usafi" kwa agizo la serikali. Kwamba jumamosi ni siku rasmi ya usafi. Je hii kitu ina uhalali gani kikatiba? Mbona kama ni udikteta?
Nijuavyo jukumu la usafi wa public areas ni la serikali kupitia manispaa/jiji na tunalipia kodi kwa hilo. Iweje serikali ilazimishe wananchi kufanya shughuli zake, tena kwa kutumia jeshi ambalo kikatiba ninavyojua kazi yake ni kulinda mipaka tu? Hii ni halali? Kama sitaki kukubali amri hiyo je nitashitakiwa kwa kosa lipi mahakamani?
Mkuu jambo la usafi si la serikali tu ni letu sote. Kinachotakiwa ni serikali kutoa taarifa mapema ili kuepusha usumbufu. Tuiunge mkono serikali kwenye suala la usafi!
 
Stupidity at its best !! Nenda kacharazwe bakora mwenyewe unakopenda, usituletee ushamba, heboo..

Kwa andiko hili, na kwa wale waliosomea psychology, ni rahisi kujua na kufahamu wewe ni mtu wa aina gani...
 
Wakati mwingine kuongoza vichaa ni budi nawe uwe kichaa.
Je kuchafua mazingira ni jambo la kikatiba?
 
Mlipokuwa mnadeki barabara kumbe yalikuwa maigizo tu hampendi usafi.

Sikuona kama walikuwa wanalazimiswa niliona wakideki kwa hiali yao. Kwab nini serkali inalazimisha watu kufanya usafi? Mbaya zaidi maeneo hayo unakuta si yao. Kwa mtindo huu siku moja tutakwenda kufanya usafi kituo cha polisi kwa nguvu.
 
Siku zone mabavu bila akili au busara Huwezi families....
 
Ni mambo ya hovyo kwa watendaji wa Magufuli kuanza kunyanyasa wananchi ili waonekane kama wanafanya kazi nzuri kumbe wanataka kumuharibia Rais, yaani nimesikitika sana kwa wanajeshi kulazimisha watu wafanye usafi, makundi ya kutafuta haki kwa nguvu huanza baada ya manyanyaso ya watawala
 
Hii kwa kweli haijakaa sawa, mkuu alisema mara moja kwa mwezi, mkuu wa mkoa kasema kila jumamosi! Sasa hii ya kila jumamosi adha yake haifai hata kusimulia! Kwa hili ninao mfano so shocking kuna mama yeye ni mjasiriamali wa chapatti na alifanya usafi wake akamaliza na saa tatu akajifungia kunako kibanda ili afanye matayarisho ya chapatti zake! Lol uongozi wa mtaa ulimvamia kama mwewe na kumtishia kumpeleka polisi au alipe 50000tzs. Mama aliomba ila hakusikilizwa ila alibidi kulipa hiyo hela! Ni hii hali ipo mbaya kwa wajasiriamali wa kada ya chini! Hawana pa kulalamikia! Niseme wazi hili litaleta madhara mbeleni!

Mmmmmmmmmmmmmmmhhhhhhhh, sawa comrade, kama ni kweli huyo mama alifanya usafi na hakusikilizwa then hiyo ni mbaya...lakini isije ikawa alijitetea tu, kwani sisi watanzania ni wazuri wa kujitetea na kulalalamika.....
 
Ni mambo ya hovyo kwa watendaji wa Magufuli kuanza kunyanyasa wananchi ili waonekane kama wanafanya kazi nzuri kumbe wanataka kumuharibia Rais, yaani nimesikitika sana kwa wanajeshi kulazimisha watu wafanye usafi, makundi ya kutafuta haki kwa nguvu huanza baada ya manyanyaso ya watawala

You may have a point...lakini sidhani kama hao askari wamewanyanyasa raia...nadhani walichofanya askari ni kuwasimamisha watu na kuwaelekeza kuwa 'jamani, leo ni siku ya usafi kwa hiyo twendeni tukafanye usafi..'. Kama mtu ana jambo la muhimu kama kwenda hospitali sidhani kuwa amekataliwa...sasa sisi watanzania tumezidi kulalamika kwa masuala ya msingi, usafi ni lazima na ni jambo jema...ingekuwa siku hiyo ni siku ya kugawa sukari ungewaona watu wote wamejaa kwenye maeneo yaliyotengwa....imefika wakati lazima tulazimishane, hakuna namna...
 
Back
Top Bottom