Serikali haiwezi kuweka utaratibu ambao unavunja utaratibu, especially wa kikatiba. Mtu yuko huru kufanya anavyotaka. Huwezi kumpangia mtu kuwa saa fulani siku fulani utafanya hiki na hiki...halafu ukaficha huo udikteta ndani ya koti la "by laws". Unauliza mchango wangu katika nchi ni nini? well, ni kodi! Sasa swali, magari ya taka na wale wafagiaji wao wanaolipwa na kodi zangu wao kazi yao ni nini? Au ndio kama tunavyozoeshwa sasa kuwa "watapangiwa kazi nyingine" 😀.
Hapa hakuna malalamiko ya kitoto hata kidogo. Mimi nina wafanyakazi wa kufanya usafi ndani kwangu iweje nikasafishe mitaro barabarani? Kwani suala ni usafi au suala ni mimi kuonekana nimebinuka mtaroni na chepe?
Mwisho kisingizio cha kwamba haiwezekani kufanya kila jambo...ni just that, kisingizio! Mbona Moshi mji msafi? Je kule sio Tanzania? Ukiuliza wazee watakuambia Dar ilikuwa safi mno enzi hizo. Ni uongozi mbaya uliotufikisha kwenye uchafu sio umaskini wetu. Badala ya magari ya taka tunanunua mawashawasha...