Kulazimishana usafi ni halali kikatiba?

Kulazimishana usafi ni halali kikatiba?

Usafi lazma cyo kulazmishwa ukijua maana ya neno usafi usingepost hata!!
 
Thanks,

1. Nakubaliana na wewe kwa asilimia 100 kuwa serikali/jiji/manispaa wana wajibu wa kufanya usafi katika maeneo ya umma. Zaidi ya hapo serikali/manispaa/jiji na kadhalika wana wajibu pia kuhakikisha kuwa hata maeneo ambayo siyo ya public nayo yanakuwa safi. kwa maana kuwa wana wajibu kuwa raia wanayaweka mazingira yao kuwa safi.

2. kuhusu hoja yako ya serikali kuingilia uhuru wa raia kwa kuwapangia raia nini cha kufanya kwa siku iliyopangwa maelezo yangu ni kuwa mamlaka zinawajibika kuhakikisha kuwa wananchi wako katika mazingira safi ikiwa ni pamoja na kuwaelekeza wananchi kufanya usafi katika maeneo yao yanayowazunguka. Serikali ya mtaa na kadhalika ina mamlaka ya kuhakikisha kuwa nyumba ya raia anayoishi iko katika mazingira safi.

That's exactly what is required!!

Lakini hii ya Mtwara jana, no way ni out of order na ni wazi wahusika walipotoka!

Na kwa kuongezea tu ni kuwa, inakubalika kabisa kwa vikundi au utaratibu flani wa kuhamasishana kwenda kushiriki kwa kusaidia kufanya usafi sehemu flani mfano hospitali, stendi au ktk taasisi flani yoyote!

Na hii ni sharti iwe kwa hiari lakini si kwa kulazimishana kama ilivyotokea Mtwara kwa JWTZ na RC kukamata raia wenye mishe mishe zao eti kushiriki usafi kwa lazima ktk maeneo yasiyo wahusu!!
 
Sawa kabisa, kwani hata mtoto asiyependa kuoga huogeshwa kwa nguvu. Watanzania wengine ni kama watoto wasiojua maslahi yao. Ukifuata "Katiba" tu (ambayo hawaijui ila vipengee vinavyowabana) hutafika.
 
Usafi sio hiari ni lazima...na tulijua mtalalamika.
 
Imetokea hadi huku kwetu mtwara, tena wanalazimisha tu bila hata ya kukusikiliza, wengine wametoka mkwao wana haraka zao kufanya shughuli za msingi lakini wao wanawachelewesha, nahisi iandaliwe sera ambayo itawavutia zaidi wananchi kufanya usafi kwa hiyari kuliko huu ubabe wa kutumia jeshi kunyanyasa wananchi!!!
Sasa kama kwa hiari hawataki inakuwa tena hamna namna bali kulazimishwa tu.
 
kwa hiyo watu wa Moshi mko tofauti na watanzania wengine....niko sahihi kabisa, kwamba, mtu aliyepitia psychology atafahamu na kujua wewe ni mtu wa namna gani, sijakosea kwa hilo, you think Moshi is not part and parcel ya Tanzania ...pole, mko wachache sana wenye mawazo hayo, na time will tell kama kweli mko sahihi...

Hapo kwenye nyekundu umetoa jibu mwenyewe.. kwa hiyo niambie kama kwa Moshi imewezekana, kuna haja gani yakutumia mbinu zingine kwingine Tanzania? Isn't it easier to follow suit?

Halafu tusi refushe zaidi, ngoja niwatafute hao ma psychologists aniambie ninacho stahili kuambiwa, naweza nikagundua kitu...
 
Tunafanyiwa mambo mengi ya hovyo na viongozi wa Serikali kwa sababu wananchi nasi tumekuwa wapole kupitiliza ,maeneo ya soko la Kariakoo wafanya biashara wamewekewa na muda kabisa.Hakuna kufungua Duka mpaka ifike 10:00am na haijalishi eneo lako umeshalisafisha kabla ya huo muda.Wanao kaidi wanakamatwa mapema kabisa...
 
You are foolishly intimidated na kutoa mimicho mithili ya chura aliyebanwa na mlango!!

Pole.....

Call it what you want, hawa jamaa nimewahi kukabiliana nao na kuwaletea kiburi japo bado naamini ilikuwa ni haki yangu adhabu niliyopewa acha tu ni stori ya siku nyingine, huenda hujawahi kukutwa nao mkuu
 
pengine mnasema haya kwa chuki tu, lakini kwenye suala la kujitolea kufanya usafi, hiyo siku mtakapowakuta watu wakishughulika huwezi kupita labda uwe una mgonwa yu hoi... ni kisheria ile kama hamjui mkaisome sheria
 
kamanda umejitahidi kujibu kweli. yes kwa upande mmoja una point lakini tu naona upo biased totally. unadhani kodi unayolipa wewe inachangia kiasi gani katika matumizi ya serikali. je kuna wangapj ambao wanatafuta upenyo wa kukwepa kodi. sasa kama tuna watu namna hii its obvious serikali itakuwa na wakati mgumu wa kutimiza kila jambo kwa makusanyo ya kodi inayopata. angalia makontena hewa kiasi gani yanapita bandarini. wafanyakazi hewa wangapi. pesa zote hizi zimekuwa zikipotea na mwisho wa siku sasa serikali kama ina dhamira ya kuwatumikia wananchi kwa dhati kabisa kwa kuanzia ni lazima ihitaji msaada wa wananchi. ni mpaka pale mifumo yote ya ukwepaji kodi na mingine ikae sawa. hapo ndio labda tuanze ku enjoy service za serikali. we need to have positive thinking most of the time. au unasemaje

Ukitaka kuzungumza hivyo na sisi tutakuuliza ni mabiliioni mangapi yameshaibwa kutoka Serikalini na watumishi wanaosimamiwa na Serikali zilizopita na hii ya sasa !!?Tunaposema ni mgawanyo wa kimajukumu mtuelewe ndio maana Bungeni hatuendi wote vilevile Ikulu hatuendi wote tunawakilishwa,kila mmoja anao wajibu wake .Ubaya hapa mnachukua pesa zetu za kutekeleza jambo flani na hamfanyi hivyo ,papo hapo mnataka tutumie nguvu zetu na muda wetu kuwajibika ktk jambo ambalo tulishawajibishwa kwa kukatwa kodi.

Hawa waliopanga huu ulipaji wa kodi walizingatia mengi ,mfumo wa ujamaa sio wakati huu tena.
 
pengine mnasema haya kwa chuki tu, lakini kwenye suala la kujitolea kufanya usafi, hiyo siku mtakapowakuta watu wakishughulika huwezi kupita labda uwe una mgonwa yu hoi... ni kisheria ile kama hamjui mkaisome sheria

Unajichanganya ama haujui usimamie wapi ,kujitolea na ulazima wa Sheria ni vitu viwili tofauti
 
Nimeangalia taarifa ya habari ya ITV muda huu, nimeona wanajeshi wa JWTZ wakisimamisha magari na kulazimisha abiria kushuka na "kufanya usafi" kwa agizo la serikali. Kwamba jumamosi ni siku rasmi ya usafi. Je hii kitu ina uhalali gani kikatiba? Mbona kama ni udikteta?
Nijuavyo jukumu la usafi wa public areas ni la serikali kupitia manispaa/jiji na tunalipia kodi kwa hilo. Iweje serikali ilazimishe wananchi kufanya shughuli zake, tena kwa kutumia jeshi ambalo kikatiba ninavyojua kazi yake ni kulinda mipaka tu? Hii ni halali? Kama sitaki kukubali amri hiyo je nitashitakiwa kwa kosa lipi mahakamani?
SHERIA YA MAZINGIRA YA MWAKA 2004 KIFUNGU CHA 191. USIPOFANYA USAFI FAINI YA PAPO HAPO KUANZIA LAKI MBILI NA MAKAMPUNI NI KUANZIA MILIONI MOJA.
 
Hapo kwenye nyekundu umetoa jibu mwenyewe.. kwa hiyo niambie kama kwa Moshi imewezekana, kuna haja gani yakutumia mbinu zingine kwingine Tanzania? Isn't it easier to follow suit?

Halafu tusi refushe zaidi, ngoja niwatafute hao ma psychologists aniambie ninacho stahili kuambiwa, naweza nikagundua kitu...

That is very good, watafute hao psychologists na uwape hiyo post ya kwanza uliyokuwa umenijibu mimi, na uwape pia post yangu/zangu...
 
hapo sasa tunakwenda sawa mkuu, matatizo yangu sasa yako hapa:
Badala ya ku enforce sheria ili raia wachafuzi wachukuliwe hatua, serikali imeamua kuadhibu raia wote kwa ujumla. Mfano kama mimi kwangu safi, iweje nikurupushwe mahala pengine? Iweje niharibu ratiba zangu siku hiyo waliyopanga ili kuepuka kukamatwa barabarani nikafagie maeneo yasiyonihusu?
solution hapa ni kwa serikali hata za mtaa, kuhakikisha mazingira yako safi kwa kusimamia sheria ambazo tayari zipo.
Tukianzisha utaratibu wa kusolve matatizo kwa njia hizi, tutajikuta tunatenga kila siku, leo siku ya usafi, kesho siku ya ulinzi, etc..

Mimi nadhani suala hili la kukurupushwa mtu kwenda kufanya usafi kwenye 'public areas' linakuwa exaggerated...mimi nafahamu kuwa wanaokwenda huko kufanya usafi ni vikundi vya kujitolea na watu waliohamasika...lakini hili la usafi kwenye maeneo ya kila mtu hilo ndilo jambo lenyewe linalofanyika...Ila kama watu wanazururazurura tu na 'kufumaniwa' na 'kulazimishwa' kwenda kufanya usafi kwenye 'public areas' hiyo ni another issue, na mimi siwaonei huruma hata kidogo kama hiyo imetokea...Ofcourse suluhisho la kudumu kama ulivyoainisha wewe ni mamlaka husika kuwajibika ipasavyo kwa kusimamia sharia zilizopo na maafisa afya kupita kila nyumba kuangalia suala la usafi.
 
SHERIA YA MAZINGIRA YA MWAKA 2004 KIFUNGU CHA 191. USIPOFANYA USAFI FAINI YA PAPO HAPO KUANZIA LAKI MBILI NA MAKAMPUNI NI KUANZIA MILIONI MOJA.


Usipofanya usafi wapi?
Mana kama nimefanya usafi kwenye eneo langu asubuhi saa kumi na moja halafu sa moja nikawa naenda zangu shambani halafu unakuja kunikamata huko barabarani na kunilazimisha nifanye usafi kwenye eneo la mtu mwingine itakua ni jambo la uonevu mkubwa. Hizo ndizo kazi za wanajeshi za kujitolea mana kwa sasa hakuna vita wanabaki tu kupora wake za watu kwa mujibu wa mbunge wa Karagwe( CCM).
 
kwahiyo mnataka kusema kuna nguvu wameitumia au shida ni kuwa wanajesh wangelikuwa mgambo sidhani kama mngelisema
 
Kama ni kweli nimesomea ujinga basi wewe utakuwa mjinga kwa kabila hivyo ujinga upo kwenye DNA yako! Ujinga wangu ni huu hapa:
Maeneo ya umma/public ni jukumu la serikali na yako chini ya jamhuri. Ndio maana ukivua nguo barabarani utashitakiwa kwa kosa la jinai. Ni serikali ndio itakushitaki sio raia wenzio. Lakini ukivua nguo kwako hakuna serikali itakayokuingilia huko. Usafi, usimamizi, uendeshaji na mambo yote yanayohusu maeneo hayo ni wajibu wa serikali sio mwananchi. Mwananchi yeye wajibu wake ni kulipa kodi zitakazosimamia mambo hayo.
Huoni kuwa kama kufagilishwa Ubungo bus terminal ni wajibu wa mwananchi basi pia ni wajibu wa mwananchi huyo huyo pia kupokea tozo inayotolewa pale getini, kodi za vile vibanda pale, etc?
Upumbavu ulionao ni karama kutoka kwa Mungu hakuna wa kuuondoa. Jukumu la ulinzi wa nchi hii ni wa kila Mtanzania. Vyombo vilivyowekwa kwa ajili ya ulinzi vimepewa majukumu maalumu kwa kushirikiana na wananchi. Hivyo hivyo kwenye mazingira. Kila raia ni mlinzi wa mazingira. Hao walioajiriwa hufanya shughuli maalumu kulingana na ajira zao. Kama si upumbavu ni nini wewe kukumbushwa na kutakiwa kushiriki katika kusafisha mazingira ya mji wako ili kuukinga na maradhi ambayo huenda yakakuathiri wewe au mwanao? Basi tu kwakuwa huu upumbavu kakupa Mungu tuishie kusema kazi yake ihimidiwe huenda kwa miujiza yake atakuongoa au atajua namna ya kuikinga jamii unayoishinayo isiathirike na upumbavu wako. Amin
 
Hapa ndipo unapoona kuwa sisi waafrika bado sana hatuna viongozi wanaofikiri sawasawa zaidi ya kuwaza uchaguzi.
Tungekua na viongozi wenye kuwaza sawasawa karne hii ni karne ya kupata maendeleo kisayansi na sio kumwaga majasho na damu za watu maskini.

Tumeambiwa kuwa hii ni serikali ya viwanda. Tulitegemea tuone viwanda vya kuzalisha mbolea na gesi kwa kutumia taka zilizopo. Hali ambayo ingefanya takataka kuwa bidhaa ya kuuza na kununua. Watu wangeshindana kununua na wangeokota uchafua kama wendawazimu.
Leo hii uchafu mtu anaulipia badala ya kuuza.
Serikali za Wazungu wanarahisisha maisha ya watu wao lakini waafrika wanafanya maisha ya wanyonge kuwa magumu tena kwa kutumia mikanda ya jeshi na viboko.
Eti ndio njia ya kujiletea maendeleo.Wakati karne hii ina kila kitu cha kurahisisha maisha ya mwanadamu. Ni suala tu la mikakati ya kisayansi na sio vibako.
 
Back
Top Bottom