Kulazimishana usafi ni halali kikatiba?

Kulazimishana usafi ni halali kikatiba?

Imetokea hadi huku kwetu mtwara, tena wanalazimisha tu bila hata ya kukusikiliza, wengine wametoka mkwao wana haraka zao kufanya shughuli za msingi lakini wao wanawachelewesha, nahisi iandaliwe sera ambayo itawavutia zaidi wananchi kufanya usafi kwa hiyari kuliko huu ubabe wa kutumia jeshi kunyanyasa wananchi!!!
Mkuu wakati wa kampeni za uchaguzi wa mwaka jana wana mtwara walisema wana jambo lao!, mbona hadi sasa hatujaliona hilo jambo?
 
Upumbavu ulionao ni karama kutoka kwa Mungu hakuna wa kuuondoa. Jukumu la ulinzi wa nchi hii ni wa kila Mtanzania. Vyombo vilivyowekwa kwa ajili ya ulinzi vimepewa majukumu maalumu kwa kushirikiana na wananchi. Hivyo hivyo kwenye mazingira. Kila raia ni mlinzi wa mazingira. Hao walioajiriwa hufanya shughuli maalumu kulingana na ajira zao. Kama si upumbavu ni nini wewe kukumbushwa na kutakiwa kushiriki katika kusafisha mazingira ya mji wako ili kuukinga na maradhi ambayo huenda yakakuathiri wewe au mwanao? Basi tu kwakuwa huu upumbavu kakupa Mungu tuishie kusema kazi yake ihimidiwe huenda kwa miujiza yake atakuongoa au atajua namna ya kuikinga jamii unayoishinayo isiathirike na upumbavu wako. Amin
Kwa vile ni wewe hakuna shida.
 
Mimi nadhani suala hili la kukurupushwa mtu kwenda kufanya usafi kwenye 'public areas' linakuwa exaggerated...mimi nafahamu kuwa wanaokwenda huko kufanya usafi ni vikundi vya kujitolea na watu waliohamasika...lakini hili la usafi kwenye maeneo ya kila mtu hilo ndilo jambo lenyewe linalofanyika...Ila kama watu wanazururazurura tu na 'kufumaniwa' na 'kulazimishwa' kwenda kufanya usafi kwenye 'public areas' hiyo ni another issue, na mimi siwaonei huruma hata kidogo kama hiyo imetokea...Ofcourse suluhisho la kudumu kama ulivyoainisha wewe ni mamlaka husika kuwajibika ipasavyo kwa kusimamia sharia zilizopo na maafisa afya kupita kila nyumba kuangalia suala la usafi.
Unachofahamu hakina uzito kabisa kwa leo, thread inaongelea matukio halisi ambayo yametokea na kurushwa kwenye taarifa ya habari! Kilichofanyika ndicho hicho. Kushushwa kwenye magari na kulazimishwa kufanya usafi on the spot kabla ya kuendelea na safari. Ila nashukuru kwa kuunga mkono suluhisho la kudumu.
 
SHERIA YA MAZINGIRA YA MWAKA 2004 KIFUNGU CHA 191. USIPOFANYA USAFI FAINI YA PAPO HAPO KUANZIA LAKI MBILI NA MAKAMPUNI NI KUANZIA MILIONI MOJA.
Usipofanya usafi WAPI?
 
watu wapigishwe kazi tu kwa lazima maana kipindupindubkikitokea wa kwanza kulaumu ni nyie.HAPA KAZI TU
 
Back
Top Bottom