Kulazimishana usafi ni halali kikatiba?

Kulazimishana usafi ni halali kikatiba?

We unatakiwa ukamatwe ufanyishwe usafi siku nzima. Hata usafi tu lazima tulazimishwe na tudai kama ni haki au sio haki. Watanzania siasa zinatuharibu sana. Mambo mengine lazima yaende hata kwa viboko
Aliyekwambia kwangu kuchafu ni nani?
 
Mmmmmmmmmmmmmmmhhhhhhhhhhhh...kwani usafi unaozungumzwa ni wa public areas tu??????????!!!!!!!!!Siipendi tabia ya watanzania ya kulalamika, kulalamika,kulalamika, kulalamika.......Watanzania lazima walazimishwe kufanya usafi, kama hawataki walazimishwe kwa nguvu, ikibidi hata kwa viboko...tena jeshi liendelee kuwalazimisha watu, katika suala hili...sisi watanzania tumezidi ubishi...hakuna itikadi wala siasa katika suala hili...usafi lazima, kama hutaki au hamtaki mtaufanya kwa nguvu, hakuna kubembelezana hapa...watu tunakufa kwa kipindupindu kwa sababu ya watu wachache, haiwezekani ...Wajerumani waliwacharaza viboko mababu zetu ili wafanye kazi, sasa ni zamu sisi wenyewe tucharazane bakora...
Ndio usafi unaozungumzwa ni wa public areas, ndio maana wanakukamata barabarani na sio nyumbani kwako au kwenye biashara yako. Kwa kawaida unatakiwa kuwajibika kwa usafi nyumbani kwako kwa kuwa wewe na familia yako ndio mnachafua hapo, vile vile kwenye mtaa inabidi wakazi wa hapo muwajibike vile vile kwa kuwa nyinyi ndio wakazi wa hapo. Hata mnaweza kuchanga na kuweka utaratibu wa watu wa usafi.
Lakini hili la kulazimisha kuwa watu wasafishe popote pale watakapokutwa na jeshi wewe unaona ni ustaarabu? Huwezi kumlazimisha mtu afanye usafi eneo la public kwa sababu yeye hayuko responsible na uchafu mahala hapo. Ndio maana tunafanya collective responsibility kwa kulipa kodi manispaa/jiji mahsusi kwa ajili hiyo.
 
Sidhani kama hawa vijana walipokea amri kutoka juu wafanye hivyo. Ni akili zile zile walizonazo askari wa majeshi mengine. Bado tunayo safari ndefu kufuta ujinga na poor reasoning ya wanaovitumikia vyombo hivi. Tatizo ni mifumo inayowaandaa.
 
Kwani ukifagia dk mbili ukaomba uendelee na safari kuna tatizo gani, wajeda wafagie road halafu raia wachafue na mitairi yao izo ni dharau, ni muhim wajeshi kila wanapokuwepo waweke heshima.
Kule mtwara watu hawakujitokeza kabisa kwenye usafi, na siku ii imetangazwa kitaifa kwamba ni siku ya usafi kila jumamosi ya mwisho wa mwezi nenda kigali wanalazamishana kupaka rangi nyumba sembuse kufagia barabara.

Kuna sehemu pia nimesikia wafanyabiashara walitaku kumpiga mtendaji kwa kuwambia wafanye usafi kwanza huo si uzalendo, coz tunapita masoko mengi ni machafu mpaka watu wanaahirisha kununua bidhaaa
 
Haya mambo ya kutoka pamoja kufanya usafi ni katika kuzoeshana kumiliki mazingira yetu. Hii akili ya kusema hayo ni maeneo ya umma na serikali ndiyo yenye wajibu ni kukwepa majukumu kama mwananchi.
Yaani bora uwe unakaa kimya kuliko kuchefua watu. Yaani kitendo cha mara moja kwa mwezi kujumuika na wenzio kwa saa zisizo zidi tatu kuangalia swala la usafi katika eneo lako kwa faida yako na jamii yako unaweka pingamizi? Hivi umesomea ujinga au kupata maarifa.
Wakati mwingine hii ndiyo sehemu ya kufahamiana kwa wanajamii wa mtaa husika na kujuliana hali.
Kama ni kweli nimesomea ujinga basi wewe utakuwa mjinga kwa kabila hivyo ujinga upo kwenye DNA yako! Ujinga wangu ni huu hapa:
Maeneo ya umma/public ni jukumu la serikali na yako chini ya jamhuri. Ndio maana ukivua nguo barabarani utashitakiwa kwa kosa la jinai. Ni serikali ndio itakushitaki sio raia wenzio. Lakini ukivua nguo kwako hakuna serikali itakayokuingilia huko. Usafi, usimamizi, uendeshaji na mambo yote yanayohusu maeneo hayo ni wajibu wa serikali sio mwananchi. Mwananchi yeye wajibu wake ni kulipa kodi zitakazosimamia mambo hayo.
Huoni kuwa kama kufagilishwa Ubungo bus terminal ni wajibu wa mwananchi basi pia ni wajibu wa mwananchi huyo huyo pia kupokea tozo inayotolewa pale getini, kodi za vile vibanda pale, etc?
 
Mkuu jambo la usafi si la serikali tu ni letu sote. Kinachotakiwa ni serikali kutoa taarifa mapema ili kuepusha usumbufu. Tuiunge mkono serikali kwenye suala la usafi!
Mambo yote ni majukumu ya wote lakini tumeweka utaratibu wa nani anawajibika. Ni jukumu letu sote kulinda amani, lakini wenye jukumu hilo specifically ni jeshi la polisi. Huwezi kukurupuka na kudai jumatatu ni zamu ya wananchi kuongoza magari barabarani na atakayekaidi atapigwa faini! Kama hakuna majukumu ambayo specifically ni ya serikali, serikali kazi yake ni nini? Hivi wewe inakuingia akilini mtu umeajiri housegirl na houseboy wa kufanya usafi ndani kwako, halafu unasimamishwa na serikali barabarani ili usafishe mitaro?
 
You may have a point...lakini sidhani kama hao askari wamewanyanyasa raia...nadhani walichofanya askari ni kuwasimamisha watu na kuwaelekeza kuwa 'jamani, leo ni siku ya usafi kwa hiyo twendeni tukafanye usafi..'. Kama mtu ana jambo la muhimu kama kwenda hospitali sidhani kuwa amekataliwa...sasa sisi watanzania tumezidi kulalamika kwa masuala ya msingi, usafi ni lazima na ni jambo jema...ingekuwa siku hiyo ni siku ya kugawa sukari ungewaona watu wote wamejaa kwenye maeneo yaliyotengwa....imefika wakati lazima tulazimishane, hakuna namna...
Kwanza acha kudhani, yaliyotokea hayapingiki. Pili hoja hapa ni kwamba usafi wa maeneo ya umma (yasio majumba ya watu) ni la serikali. Hii ndio maana kuna watu maalum walioandaliwa kwa ajili ya kufanya usafi. Raia wanalipa kodi ili kugharamia watu hao. Kama watu hao hawawajibiki na kufanya uchafu kulundikana hovyo mitaani tunapaswa kuwawajibisha hao na sio kuhamisha majukumu yao kwetu. Vile vile tunapaswa kusimamia sheria za kudhibiti utupaji taka hovyo ili wachafuzi wa mazingira wadhibitiwe. Kulazimisha raia kufanya usafi wa maeneo ya public kwa maoni yangu ni serikali kukwepa kuwajibika. Hata wewe haiwezekani uajiri housegirl au houseboy wa kufanya usafi ndani kwako, halafu asipofanya usafi wewe bosi ndio uanze kuhangaika na mkeo/mmeo kufanya majukumu ambayo tayari mnayalipia!
 
Ifike mahali kodi tunayolipa itumike kufanya usafi.

Mimi hata siku moja siwezi kufanya usafi kwa amri inayotolewa na mkuu wa nchi au mkuu wa wilaya au mkoa.
 
kama hakuna "by laws" katika sehemu husika hawawezi kukulazimisha wala kukushtaki.

Lakini tambua "kauli au maagizo ya watawala(viongozi) sometime zinasimama kama sheria"
Hakuna kitu kama hicho yani kauli ya viongozi igeuke kuwa sheria?

Ni vilaza tu ndiyo watatii hizo kauli za hao viongozi.
 
Ni udikteita , lakini mtajuta nilisema kuwa jamani CCM haifai!
siku hizi ccm imekuwa dikteta na siyo mafisadi anymore. wamesoma alama za nyakati kisawasawa. wakati wao wameondoka kwenye ufisadism vyama vyetu vingine ndio vimeingia sasa. hapo ndio utajua ccm wapo mbali sana kisiasa. there is a big gap in between.
 
This is just too much, yani mtu unakatizwa matembezi yako ili ukafagie barabara? What's next? tutaanza kuchomolewa majumbani kwa mitutu?
Mfano umetoka out na demu wako mara unakutana na mijeda unaambiwa uokote takataka sijui
 
Mfano umetoka out na demu wako mara unakutana na mijeda unaambiwa uokote takataka sijui
Hapo sasa! Halafu niliuliza hili swali sikujibiwa:
Huu utaratibu wa kusimamisha magari yanayopita barabarani pia utatumika airport kusimamisha wale wanaokwenda sauzi nao pia wasipande ndege hadi wafanye usafi? sikujibiwa.😀
 
Je ikatokea kipindupindu kwa mfano nani anakua responsible
Serikali inayokusanya kodi iko responsible,
Umeshawahi kulipia leseni ya biashara?
Kila anayelipia leseni ya biashara lazima alipie na pesa kwa ajili ya taka.
Tunakatwa kodi kwenye kila bidhaa tunayonunua hadi kiberiti.
Sasa mazwazwa ya CCM pekee ndiyo yataona ni sawa raiya kuburuzwa na serikali kurupukaji.
 
leo hii ndio mnauliza eti ni halali KIKATIBA nyinyi mlivyomuingiza mwanachama ambaye hakukaa hata mwezi mmoja mkampa na nafasi ya kugombea urais kupitia chama chenu ilikuwa ni halali kikatiba?
Uko nje ya mada, punguza jazba rudi kwenye mada.
Mnakusanya kodi ya nini kama mnashindwa kusimamia usafi?
 
Nimeangalia taarifa ya habari ya ITV muda huu, nimeona wanajeshi wa JWTZ wakisimamisha magari na kulazimisha abiria kushuka na "kufanya usafi" kwa agizo la serikali. Kwamba jumamosi ni siku rasmi ya usafi. Je hii kitu ina uhalali gani kikatiba? Mbona kama ni udikteta?
Nijuavyo jukumu la usafi wa public areas ni la serikali kupitia manispaa/jiji na tunalipia kodi kwa hilo. Iweje serikali ilazimishe wananchi kufanya shughuli zake, tena kwa kutumia jeshi ambalo kikatiba ninavyojua kazi yake ni kulinda mipaka tu? Hii ni halali? Kama sitaki kukubali amri hiyo je nitashitakiwa kwa kosa lipi mahakamani?
serikali imeweka utaratibu. ni by laws kwamba kila mwisho wa mwezi ni usafi. na hii ni kwa faida ya wananchi wote si kwa faida ya serikali . dharura zinaeleweka si maelezo yapo? msingi wa swali lako sielewi. unajua watu wana hulka ya kukwepa mambo mengi ya msingi ya nchi kwa kudhania usafi ni jukumu la serikali tu..hivi wewe una mchango gani katika nchi. kumbuka mwl Nyerere alisema usiiulize nchi itakufanyia nini, jiulize wewe unaitaifanyia nini nchi kama mzalendo. malalamiko mengine ya kitoto tuyaache. nenda kafanye usafi. kwani ukifanya usafi utakufa? nchi zetu hizi bado zinapambana na kujikwamua kiuchumi. hazina uwezo wa kufanya kila jambo, sio kama nchi za wenzetu zilizoendelea kiuchumi. please note that.
 
Kinga ni bora kuliko tiba
Leo na kesho kikazuka kipindupindu lawama hurudi tena serikalini hivyo ni bora tujihadhari mapema hata kwa nguvu tu
Wewe ni msukule nini? Hivi kwa mfano mtu ana mgonjwa, anawahi kazini au anawahi safari halafu unamsimamisha? Bora waseme eneo unaloishi likiwa chafu ndio sheria ichukue mkondo wake lakini si vinginevyo
 
Mkuu kabla hujafikiria kukaidi agizo hilo bora kesho usikilize au ununue magazeti kwani kadri nilivyosikia taarifa ya habari Itv saa mbili usiku faini ni shs elfu hamsini na kifungo kuanzia miezi sita hadi miaka saba.Kwa mashirika na ofisi za serikali faini zake ni mamilioni.Nadhani hizo ni sheria ndogo ndogo zitakazoagizwa kutekelezwa na majiji na halimashauri.
Halimashauri yangu haijapitisha hizo bylaws.
Watu wasiojielewa ndiyo watatii huo upumbavu.
 
Hakuna haja ya kulazimisha watu, hiyo ni sawa na kulazimisha watu kufanya kazi. Hatuwezi kufanikiwa, tunatakiwa tuwashawishi watu kufanya usafi (au kazi) si kuwalazimisha.
Wewe utakuwa kibaka tu , kama hufanyi kazi unaishi kwa kuiba , hulipi kodi unaishi ka nguruwe na kuambukiza watu uchafu hili waugue ? shwaini !!!
 
Back
Top Bottom