Kulazimishana usafi ni halali kikatiba?

Kulazimishana usafi ni halali kikatiba?

watu wawe na hali ya kutunza na kuyapenda mazingira sio mpaka kushikiana fimbo ndio usafi ufanyike.
 
Hili jambo limenipotezea muda na pesa leo aghrrrrrrrrrrr kwakweli nimetukna matusi ya kutosha mpaka hasira zikashuka[emoji35] [emoji35] [emoji35] [emoji35]
Hiyo pesa uliyopoteza ukianza kuharisha itakutokea puani dogo.
 
Nimeangalia taarifa ya habari ya ITV muda huu, nimeona wanajeshi wa JWTZ wakisimamisha magari na kulazimisha abiria kushuka na "kufanya usafi" kwa agizo la serikali. Kwamba jumamosi ni siku rasmi ya usafi. Je hii kitu ina uhalali gani kikatiba? Mbona kama ni udikteta?
Nijuavyo jukumu la usafi wa public areas ni la serikali kupitia manispaa/jiji na tunalipia kodi kwa hilo. Iweje serikali ilazimishe wananchi kufanya shughuli zake, tena kwa kutumia jeshi ambalo kikatiba ninavyojua kazi yake ni kulinda mipaka tu? Hii ni halali? Kama sitaki kukubali amri hiyo je nitashitakiwa kwa kosa lipi mahakamani?
We unatakiwa ukamatwe ufanyishwe usafi siku nzima. Hata usafi tu lazima tulazimishwe na tudai kama ni haki au sio haki. Watanzania siasa zinatuharibu sana. Mambo mengine lazima yaende hata kwa viboko
 
Kinga ni bora kuliko tiba
Leo na kesho kikazuka kipindupindu lawama hurudi tena serikalini hivyo ni bora tujihadhari mapema hata kwa nguvu tu
Hivyo hamjui kipindupindu kinambukizwaje au mnapotezea tu?
 
Sasa kama umeshafanya eneo lako umemaliza unashushwa kufanya usafi gani. Ubabe wao wanaouleta hautazaa matunda
 
Nimeangalia taarifa ya habari ya ITV muda huu, nimeona wanajeshi wa JWTZ wakisimamisha magari na kulazimisha abiria kushuka na "kufanya usafi" kwa agizo la serikali. Kwamba jumamosi ni siku rasmi ya usafi. Je hii kitu ina uhalali gani kikatiba? Mbona kama ni udikteta?
Nijuavyo jukumu la usafi wa public areas ni la serikali kupitia manispaa/jiji na tunalipia kodi kwa hilo. Iweje serikali ilazimishe wananchi kufanya shughuli zake, tena kwa kutumia jeshi ambalo kikatiba ninavyojua kazi yake ni kulinda mipaka tu? Hii ni halali? Kama sitaki kukubali amri hiyo je nitashitakiwa kwa kosa lipi mahakamani?

Mmmmmmmmmmmmmmmhhhhhhhhhhhh...kwani usafi unaozungumzwa ni wa public areas tu??????????!!!!!!!!!Siipendi tabia ya watanzania ya kulalamika, kulalamika,kulalamika, kulalamika.......Watanzania lazima walazimishwe kufanya usafi, kama hawataki walazimishwe kwa nguvu, ikibidi hata kwa viboko...tena jeshi liendelee kuwalazimisha watu, katika suala hili...sisi watanzania tumezidi ubishi...hakuna itikadi wala siasa katika suala hili...usafi lazima, kama hutaki au hamtaki mtaufanya kwa nguvu, hakuna kubembelezana hapa...watu tunakufa kwa kipindupindu kwa sababu ya watu wachache, haiwezekani ...Wajerumani waliwacharaza viboko mababu zetu ili wafanye kazi, sasa ni zamu sisi wenyewe tucharazane bakora...
 
Je ikatokea kipindupindu kwa mfano nani anakua responsible

Kipindu pindu kina sababishwa na ukosefu wa maji safi...hilo jukumu la serikali
kupindupindi kina sababishwa na miundo mbinu mibovu ya kutokuwa na sewage system..hilo jambo la serikali.

usafi wa Roads zetu nao ni jukumu la halmashauri.

watu hawawezi wote waache kazi zao za kujenga Taifa ili wafagie bara bara. Ndio maana kuna mgawanyo wa kazi.
Tualipa kila nyumba na ofisi kodi ya usafi ambayo inakusanywa na Manispaa
Mji wa Moshi umeweza kwa kusimamia manispaa na kwa sheria za kuhimiza usafi , na kutotupa vitu.

Maagizo haya hayapo katika mataaifa yote yenye miji misafi.
Maagizo haya yana asili ya nchi ziliz feli za Kikomonisti kina Mao , Lenin, Stalin, Ceausescu na kama hao. Hawa walifeli kutengeneza nchi zao hivyo kuwafanya raia kila mara busy ili wasahau matatizo yao ya afya , elimu , chakula na kazi bora.

maamuzi haya yalipata wapingaji na mamlaka ndio walikua wakitafuta ili wakamatwe na waambiwe hawa ndio vitimba kwiri.

Hakuna katika Majiji Masafi zaidi Duniani yanayo tumia mbinu Hii au huko nyuma kutumia mbinu hii ya Ujima. Miji 10 misafi duniani ni kama ifuatavyo
  1. Calgary , Canada
  2. Adelaide , Australia
  3. Honolulu , Hawaii
  4. Minneapolis , USA
  5. Kobe , Japan
  6. Copenhagen, Denmark
  7. Wellington . New Zealand
  8. Helsinki Finland
  9. Oslo Norway
  10. Freiburg Germany
Africa miji ifuatayo ndio safi kabisa na Manispaa ndio wahusika sio raia na mifagio.
  1. Cape Town , South Africa
  2. Port Louis Mauritius
  3. Johannesburg South Africa
  4. Tunis , Tunisia
  5. Gaborone , Botswana
Manispaa za majiji hayo yamefanikiwa kwa kuweka sheria kali za kutupa Taka hovyo na kuweka yafuatayo kipau mbele
  • Sewage system zinazo fanya kazi vizuri kwa maeneo yote ya miji
  • Kuhakikisha maji safi ya kunywa yana patikana kila pembe ya majiji
  • Kuweka mikakati madhubuti ya Taka taka na njia bora ya ku Recycle Taka taka kama kuzitumia kama mbolea au kuzalisha umeme
  • kuondoa kabisa matatizo ya Foleni za magari
  • Kuondoa na kusimamia Kupunguza Polution na kusimamia njia Bora za kupunguza Industrial waste.
  • miundo mbinu ya kisasa ya barabara - sio hizi za kuweka mitaro ya wazi kila kwenye roads...hii sijui architecutre wetu wamesomea wapi . Dunia nzima hii ipo Bongo tu..hakuna miji yenye miundo mbinu kama hii yakwetu
Manispaa ziwajibike kuwatumikia wananchi ina wananchi wapewe muda wao wafanye kazi na kuzalisha ili waweze kulipa kodi ili manispaa ziwajibike kama wafanyavo wengine walofanikiwa.
..tuwajibike na tutafika
 
Kesho ukiumwa kipindu pindu unahisi nani atakuwa anaumia kama sio wewe na nduguzo?
 
You are very right mkuu. Na kwa kuongezea tu ni kuwa, ziko sheria nyingi zinazoongoza na kuwalazimisha watu kuwa wasafi.

Mfano sheria ya mipango miji ambayo inamwelekeza kila anayejenga nyumba kuhakikisha nyumba yake ina mfumo wa maji taka na choo. Lazima ramani ya jengo iwe approved na mamlaka husika kabla ya ujenzi kuanza!!

Zipo sheria nyingi ndogo ndogo (by laws) kutegemeana na sehemu zinazowalazimisha watu kuwa wasafi mfano kutotupa taka hovyo, kutopiga kelele kama za miziki mikubwa ya disco bar nk.

Tatizo ni kwamba usimamizi wa sheria hizi ndilo tatizo!

Na hii ya kukamata watu njiani kuwalazimisha kushiriki usafi wa maeneo ambayo tayari yana watu wanaopaswa kufanya usafi huo ktk maeneo yao wala hata halikubaliki!!

Huwezi ukazuia mtu ambaye ana safari zake njiani eti ashiriki usafi wa kusafisha eneo la hospitali au soko!!

Wenye soko na hospitali wanakuwa wako wapi kwani? Kwa nini wao ndiyo wasiwajibike kufanya usafi katika taasisi yao?

After all huyu mtu anayeshushwa katika gari akiwa ktk safari yake anakuwa ametoka nyumbani kwake ambako tayari alishafanya usafi vyema tu.

Nadhani hii ya kuwachukulia hatua za kisheria watu ambao hawafanyi usafi ni sawa iwapo itafanywa na serikali za mitaa kwa mtu kushindwa kuwa na choo ktk nyumba yake, kutosafisha eneo la nyumba yake, kutokuwa kuwa na shimo au chombo cha kuhifadhia taka ktk eneo la nyumba yake nk. Hii inaeleweka wala haina tatizo kabisa!!

Napata shida kidogo kuelewa hii iliyofanyika kule Mtwara kwa Jeshi kutumika kulazimisha kila mtu kushiriki usafi kwa lazima tena ktk maeneo ambayo hata hayawahusu huku wengine wakiwa ktk safari na shughuli zao za kila siku!!
 
Eti public areas,ukienda stand wanakutoza ushuru,hospital tunalipia mafungu pia wanapata,barabara wamiliki wanajulikana. By laws ni kuwabana wananchi katika mazingira yao ya makazi na kutokuchafua mazingira mengine.
Mie kwangu kusafi,uniambie nisafishe barabara,ama stand huo ni upumbafu wa viongozi ktk kufikiri. Ndio maana maeneo yanapimwa na mmiliki anajulikana.
 
Inasikitisha sana.. nchi yetu inakosa misimamo sahihi kwenye baadhi ya mambo
 
Kwasababu kwa hiari imeshindikana haina haina namna kwa lazma basi tutafanya manake usaf lazma mwisho wa siku
 
Usafi wa mazingira ni suala la lazima sio hiyari fuateni maagizo
Mkibanwa mnaanza kutafuta vipengele vya sheria,hayo mnayoyafanya kila siku yanafuata sheria?
 
Kituko kingine hapa wanajeshi walikuwa wanawalazimisha wachina na wahindi washuke kwenye nagari yao kufanya usafi. Raia mmoja akawa anatumia simu kupiga picha Tukio hilo ambalo lilikuwa public. Wanajeshi wa JWTZ wakamnyang'anya simu yake wakaipasua waka mpiga kidogo yule raia alikuwa na mtoto mdogo anayekadiriwa kuwa na miaka miwili hadi mitatu wakampeleka polisi wakashinda huko hadi sisi tunaondoka kwenda kumsikiliza mkuu wa Mkoa. Hatujui yule mtoto alipata japo chakula au chai.
Watu wanaoitikia kwa hiyari maagizo ya viongozi wap waheshimiwe. Mimi siku nyingine sitashiriki kampeni zinazohushisha JWTZ
 
Hii kwa kweli haijakaa sawa, mkuu alisema mara moja kwa mwezi, mkuu wa mkoa kasema kila jumamosi! Sasa hii ya kila jumamosi adha yake haifai hata kusimulia! Kwa hili ninao mfano so shocking kuna mama yeye ni mjasiriamali wa chapatti na alifanya usafi wake akamaliza na saa tatu akajifungia kunako kibanda ili afanye matayarisho ya chapatti zake! Lol uongozi wa mtaa ulimvamia kama mwewe na kumtishia kumpeleka polisi au alipe 50000tzs. Mama aliomba ila hakusikilizwa ila alibidi kulipa hiyo hela! Ni hii hali ipo mbaya kwa wajasiriamali wa kada ya chini! Hawana pa kulalamikia! Niseme wazi hili litaleta madhara mbeleni!
 
Mmmmmmmmmmmmmmmhhhhhhhhhhhh...kwani usafi unaozungumzwa ni wa public areas tu??????????!!!!!!!!!Siipendi tabia ya watanzania ya kulalamika, kulalamika,kulalamika, kulalamika.......Watanzania lazima walazimishwe kufanya usafi, kama hawataki walazimishwe kwa nguvu, ikibidi hata kwa viboko...tena jeshi liendelee kuwalazimisha watu, katika suala hili...sisi watanzania tumezidi ubishi...hakuna itikadi wala siasa katika suala hili...usafi lazima, kama hutaki au hamtaki mtaufanya kwa nguvu, hakuna kubembelezana hapa...watu tunakufa kwa kipindupindu kwa sababu ya watu wachache, haiwezekani ...Wajerumani waliwacharaza viboko mababu zetu ili wafanye kazi, sasa ni zamu sisi wenyewe tucharazane bakora...

Stupidity at its best !! Nenda kacharazwe bakora mwenyewe unakopenda, usituletee ushamba, heboo..
 
Imeingizwa na kuwa sheria ya mazingira sasa unashitakiwa ukikataa kufanya usafi na kuna fine sh 2000 hadi mil 2....na kifungo hadi miaka 7!
 
Back
Top Bottom