Kulazimishana usafi ni halali kikatiba?

Kulazimishana usafi ni halali kikatiba?

leo hii ndio mnauliza eti ni halali KIKATIBA nyinyi mlivyomuingiza mwanachama ambaye hakukaa hata mwezi mmoja mkampa na nafasi ya kugombea urais kupitia chama chenu ilikuwa ni halali kikatiba?
Sio kila mtu chadema humu, jifunze kujadili hoja sio watu. Hata sisi tusiokuwa chadema tunaanza kuwa na wasiwasi iweje kila siku mnaweweseka kumtajataja mtu mmoja tu.
 
Hiyo ya kulazimishana kufanya usafi hizo ni akili za shuleni.
Kwahiyo mtu mzima huwezi ukawa unamlazimisha kufanya usafi kama mtoto wa darasa la pili.
 
Hata wewe ikigundulika huogi na hufui nguo zako ukawa msafi utalazimishwa kufanya hivyo.
 
Imetokea hadi huku kwetu mtwara, tena wanalazimisha tu bila hata ya kukusikiliza, wengine wametoka mkwao wana haraka zao kufanya shughuli za msingi lakini wao wanawachelewesha, nahisi iandaliwe sera ambayo itawavutia zaidi wananchi kufanya usafi kwa hiyari kuliko huu ubabe wa kutumia jeshi kunyanyasa wananchi!!!

Mkuu kabla hujafikiria kukaidi agizo hilo bora kesho usikilize au ununue magazeti kwani kadri nilivyosikia taarifa ya habari Itv saa mbili usiku faini ni shs elfu hamsini na kifungo kuanzia miezi sita hadi miaka saba.Kwa mashirika na ofisi za serikali faini zake ni mamilioni.Nadhani hizo ni sheria ndogo ndogo zitakazoagizwa kutekelezwa na majiji na halimashauri.
 
Tuanzie hapa::;Kazi ya jeshi sio kulinda mipaka tu brother
 
Inawezekana nimesimplify, naomba unisaidie hili la kushusha watu kwenye magari na kuwalazimisha wafanye usafi ni jukumu lao kivipi?
Kiukweli sio nzuri hao walivyofanya pia labda kabla ya kupost ungefanya uchunguzi kwny maeneo tofauti ili ujue kama ni JESHI LA NCHI NZIMA ndo linawafanyia watu hivyo au ni hilo eneo uliposhuhudia tukio...kwa sababu jeshini ni kufuata amri tu..inawezekana afande mmoja akawa ameamrisha hivyo lkn ww ukahisi ORDER Inatoka kwa magufuli...fanya uchunguzi kwanza kwny maeneo tofauti kk..
 
Ni taarifa ya habari ya leo ITV na sio kwamba ni jambo la siri, nimesoma vile vile humu JF thread nyingine kuwa apparently hili jambo sasa ni rasmi. Je unakubali kuwa sio kikatiba?
 
Kimsingi kumtoa mtu kwny gari na kumlazimisha afanye usafi sio kitu kizuri cuz u never know anatoka wapi au anakwenda wapi..lkn kk..hivi vitendo vinatokea sehemu tofautitofauti au hizo taarifa za itv ndo zimepostiwa huku jf..!?
 
Nimeangalia taarifa ya habari ya ITV muda huu, nimeona wanajeshi wa JWTZ wakisimamisha magari na kulazimisha abiria kushuka na "kufanya usafi" kwa agizo la serikali. Kwamba jumamosi ni siku rasmi ya usafi. Je hii kitu ina uhalali gani kikatiba? Mbona kama ni udikteta?
Nijuavyo jukumu la usafi wa public areas ni la serikali kupitia manispaa/jiji na tunalipia kodi kwa hilo. Iweje serikali ilazimishe wananchi kufanya shughuli zake, tena kwa kutumia jeshi ambalo kikatiba ninavyojua kazi yake ni kulinda mipaka tu? Hii ni halali? Kama sitaki kukubali amri hiyo je nitashitakiwa kwa kosa lipi mahakamani?
Katiba gani iliyoruhusu kuchafua tu? Kila mwananchi ni askari wa kupambana kuondoa adui maradhi ujinga na umasikini. Njia mbalimbali hutumika kufanikisha hilo. Hizi njia haziwekwi kwenye katiba kwa sababu hubadirika kulingana na mahali na wakati.
Aliyekufundisha neno katiba hakumaliza somo wewe ukanyanyuka na kujinadi umeelewa katiba na sasa umekuwa kasuku kila kitu katiba, fuata uzazi wa mpango katiba, elewana na jirani zako katiba, chemsha maji katiba. Rudi kajifunze hujajua matumizi ya katiba.
 
1. Jukumu la usafi wa maeneo ya public ni wa serikali. Ndio maana tuna magari ya taka. Mtu binafsi ninawajibika kuweka mazingira yangu binafsi kama nyumba, sehemu ya biashara etc,
2. Kumlazimisha mtu kufanya chochote kile bila ridhaa yake sio kuingilia uhuru binafsi wa mtu?
Nimemsikiliza, japo kwa kifupi, naibu waziri wa mazingira na muungano, mpina, alikuwa akiongoza shughuli za usafi leo pale UDOM Dodoma. Amesema tayari imepitishwa sheria inayowataka watu wote kufanya usafi kila Jumamosi ya mwisho wa mwezi. Amesema tayari serikali kupitia gazeti la serikali la Aprili 26, mwaka huu imetangaza kuanza kutekelezwakwa sheria hiyo ambayo imeainisha na adhabu kwa anayekiuka. Alitaja kiwango cha faini ila sikumsikia vizuri. Lakini nilichojifunza haraka haraka kupitia kauli na namna alivyokuwa akifafanua, ni kama vile viongozi wetu sasa wameamua kutumia mabavu hata kwa mambo ambayo hayahitaji mabavu. Ndio maana, bila shaka, leo tunaambiwa kule Mtwara wanajeshi wametumika kushusha watu kwenye magari ili wafanye usafi.
Ni jambo la kushangaza kwamba haya yanafanyika wakati kuna kodi zinazolipwa na wananchi ambazo zinatumika kwa ajili ya mambo hayo hayo ya usafi! Ngoja tuone......
 
Katiba gani iliyoruhusu kuchafua tu? Kila mwananchi ni askari wa kupambana kuondoa adui maradhi ujinga na umasikini. Njia mbalimbali hutumika kufanikisha hilo. Hizi njia haziwekwi kwenye katiba kwa sababu hubadirika kulingana na mahali na wakati.
Aliyekufundisha neno katiba hakumaliza somo wewe ukanyanyuka na kujinadi umeelewa katiba na sasa umekuwa kasuku kila kitu katiba, fuata uzazi wa mpango katiba, elewana na jirani zako katiba, chemsha maji katiba. Rudi kajifunze hujajua matumizi ya katiba.
Unachanganya mambo, sijui umefikiaje conclusion kuwa kupinga hili suala maana yake ni kuunga mkono uchafu. Hoja hapa ni kuwa kuna mgawanyo wa uwajibikaji. Usiposafisha eneo lako la biashara unachukuliwa hatua kwa kuwa unakuwa na wajibu wa moja kwa moja kwa usafi wa hapo. Lakini usafi wa mazingira ya umma ni jukumu la serikali/manispaa/jiji na wafanyakazi wa kusimamia hilo wapo. Hii ni kazi professional. Dunia iliyostaarabika haiwezi kumsimamisha mtu kaulamba zake, chini ya ulinzi wa JESHI na kumlazimisha ghafla ashike fagio na kufagia barabara! Kama wewe unasema hiyo ndio katiba basi sawa, inatosha kukuelezea wewe ni msomi kiasi gani wa hiyo katiba!
 
Nimemsikiliza, japo kwa kifupi, naibu waziri wa mazingira na muungano, mpina, alikuwa akiongoza shughuli za usafi leo pale UDOM Dodoma. Amesema tayari imepitishwa sheria inayowataka watu wote kufanya usafi kila Jumamosi ya mwisho wa mwezi. Amesema tayari serikali kupitia gazeti la serikali la Aprili 26, mwaka huu imetangaza kuanza kutekelezwakwa sheria hiyo ambayo imeainisha na adhabu kwa anayekiuka. Alitaja kiwango cha faini ila sikumsikia vizuri. Lakini nilichojifunza haraka haraka kupitia kauli na namna alivyokuwa akifafanua, ni kama vile viongozi wetu sasa wameamua kutumia mabavu hata kwa mambo ambayo hayahitaji mabavu. Ndio maana, bila shaka, leo tunaambiwa kule Mtwara wanajeshi wametumika kushusha watu kwenye magari ili wafanye usafi.
Ni jambo la kushangaza kwamba haya yanafanyika wakati kuna kodi zinazolipwa na wananchi ambazo zinatumika kwa ajili ya mambo hayo hayo ya usafi! Ngoja tuone......
Huku sasa tunaelekea siko kwenyewe. Hivi na ndege nazo jumamosi zitakuwa haziruhusiwi kuruka mpaka usafi uishe au hili zoezi ni kwa ajili ya wapanda mwendo kasi pekee?
 
Kinga ni bora kuliko tiba
Leo na kesho kikazuka kipindupindu lawama hurudi tena serikalini hivyo ni bora tujihadhari mapema hata kwa nguvu tu
Kipindupindu tatizo mabomba yavdawasa maji masafi na machafu yanilazwa pamoja njia moja
 
Wabongo tumezidi uchafu, unanyonya kiroba halafu unatupa, sasa ndio mtajifunza usafi lasivyo uliyo yatupa jana utayaokota kesho. Kwa mwendo huu utajifikiria mara mbili mbili kutupa uchafu hovyo.
 
Kama imepitisha inabidi iainishe namna ya kufanya uo usafi maana kunawasafiri, wagonjwa na wenye matatizo mengine bila ya kufanya ivyo italeta migogoro mingi
 
Back
Top Bottom