Kula tunda kimasihara kunavyoigarimu ndoa yangu

Yaani anajifanya mjanja wakati wakwake analelewa na mkewe, anamtafutia manyanyaso huyo mwanaye

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu ungejiuliza kidogo kwanza maswali haya,huyo shemeji yake aliyempa mimba huko wapi? Je upande wa mume wa shemeji kwanini wasimchukue? Au kwanini asimpeleke kwa mama yake au mama mkwe? Kusema nayeye alileta mtoto ambaye ni damu yake kabisa kufananisha na hii case ya shemeji hapana.
 
Best wangu aliacha mtoto wa mwezi mmoja kwenda uni, lakini yeye alimuoa has kwa baba na mama yake. Alipata mimba akiwa jeshini matokeo Yamato’s alikua na div 2 PCB
Bado inauma kumuacha mtt mdogo hivyo. Tena kama chuo kuna option ya kuhairisha mwaka au siku hizi hakuna hizo kitu?
 
Bado inauma kumuacha mtt mdogo hivyo. Tena kama chuo kuna option ya kuhairisha mwaka au siku hizi hakuna hizo kitu?
zipo sana... By the way chuo mbona wengi wana familia zao, wapo wenye vichanga wanapiga shule km kawaida...
 
Kama kiongozinwa familia shikilia msimamo huo ambao unafaida kwa mtoto mwenyewe,,yan mwanachuo alipokiwa anafanya hayo na kupata ujauzito alikua anategemea nin,,mtoto wa mmwezi kweli,, familia ya ukweni kwako bro wakoje kwa malezi ya watoto,wew utampa nin mtoto ambaye mama yake yupo eti anasoma,,mwambie shemeji asikutanie aende nae shule au aahirishe masomo,,kosa lako si lazima iwe fimbo kwako...pia hukufanya vyema tena kama tayari ulikuwa na mke

Sent using Jamii Forums mobile app
 
kwani hakuna ndugu mwingine mfano bibi wa huyo mtoto yuko wapi? i mean mama wa mkeo, kwanini asipekelewe kichanga akalea, nazani utuambie zaidi ili tujue jinsi ya kutoa msaada wa mawazo zaidi
 
kwani hakuna ndugu mwingine mfano bibi wa huyo mtoto yuko wapi? i mean mama wa mkeo, kwanini asipekelewe kichanga akalea, nazani utuambie zaidi ili tujue jinsi ya kutoa msaada wa mawazo zaidi
Ma mkwe mgonjwa, uzee umemtinga,,, kumpelekea kichanga ni km haiwezekani
 
kwani hakuna ndugu mwingine mfano bibi wa huyo mtoto yuko wapi? i mean mama wa mkeo, kwanini asipekelewe kichanga akalea, nazani utuambie zaidi ili tujue jinsi ya kutoa msaada wa mawazo zaidi
Hili suala la kumpelekea bibi alee mtoto na wazazi mpo mnajiweza na nguvu zenu huwa silielewi. Kwanini muwatese mama zenu muda wa yeye kupumzika uzeeni hakuna.
Kalea watoto wake kamaliza hlf muwapelekee wa kwenu. Tuache hizo jamani labda iwe sababu ya msingi sana.
.
.
Mama yangu atanitoa mbio kumuachia mtoto sijui naanzia wapi loh

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwani uyo mtoto wa shemeji yako hana baba??

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Habar za muda huu wanajamvi. Nitaeleza kwa kifupi.,

Kama tujuavyo mabaharia tunapita na wengi kimasihara, sasa Ktk ptpt zangu nikapata zawadi ya mtoto nje ya ndoa, mama wa uyu mtoto hana maisha ya kueleweka yupo yupo yani kimasihara, ni mtu ambaye yan ht ukiamua umwezeshe kimaisha hawezi., mambo mengi muda mchache.. kwa hiyo mimi kama baba wa uyu mtoto nikamsoma mapema hawezi kumlea mwanangu.

Nikamwambia wife everything going on, hali ilikua tete bt baadae ilibidi tu anielewe, nikamchkua mtoto akiwa na mwaka tu. na mama wa mtoto ye hana hbr yan ndo kwanza nilivomwambia akaona nampunguzia mzigo.

Mtafaruku umeanza pale shemeji wa mimi mdogo wa mke wangu anataka atuachie kichanga cha mwezi mmoja kwa kigezo anaenda kuendelea na masomo ya chuo yaani kwa kifupi kitoto kinamtinga akiwa masomoni. Kapata backup toka kwa dadaye ( mke wangu) kwamba ni sahihi aache huyo mtoto yy akapige shule.

Nilipokataa kwa busara tu za kawaida kwamba mamaye yupo haumwi na kitoto bado kidogo mno, ndipo nilipogeuka adui wa kila mtu si mke wangu, si mashemeji wote wananiona mimi sitaki kutoa msaada wa malezi ya ndugu wa mke..

Mke wangu nae ananikumbusha khsu uyu mwanangu nliempata nje ya ndoa kila ninapinga hili swala. Juzi kanijibu mbovu nikashindwa kujizuia nikampa kibano cha haja kidogo, hadi saivi yupo kwao...

Mabaharia wenzangu, dada zangu na mama zangu wazoefu wa maisha ya ndoa nipeni mwongozo, uhusiano na ndugu wa mke kwa sasa ni mbaya sana.,.

Je ni ubinafsi wangu ndo unaosababisha huu mgogoro? Niumalize huu mgogoro vipi.? Nikipokee kichanga kwa kigezo tu cha mamaye kusoma?
Mkuu tatizo lako ni dogo tu, umefunga ndoa kwa mtindo wa HISA. Mkeo ana asilimia 50 na wewe 50. Badala ya kuleta msaidizi umeleta mwanahisa, endelea kulipa gharama.

Sent from my SM-T355Y using Tapatalk
 
Ma mkwe mgonjwa, uzee umemtinga,,, kumpelekea kichanga ni km haiwezekani

somehow nakuelewa sana kwanini unamkataa huyo mtoto lakini pia it seems mkeo nae hana choice kama unavyosema kulingana na nature ya familia ndo mana amekubali huyo mtoto, inaonyesha hakuna mwingine mwenye maisha ya kueleweka anaeweza kubeba huo mzigo na anaona kabisa asipobeba hilo jukumu hicho kichanga kimekwisha. Inabidi hekima itumike hapo tena sana, na pia kumbuka mkeo bado ana maumivu ya uzinzi wako wa mpaka kumletea mtoto alee, sasa na yeye its time anahitaji uwe mwelewa kama yeye alivyokubali kuelewa ulichomletea, tumia hekima zaidi bro
 
Hili suala la kumpelekea bibi alee mtoto na wazazi mpo mnajiweza na nguvu zenu huwa silielewi. Kwanini muwatese mama zenu muda wa yeye kupumzika uzeeni hakuna.
Kalea watoto wake kamaliza hlf muwapelekee wa kwenu. Tuache hizo jamani labda iwe sababu ya msingi sana.
.
.
Mama yangu atanitoa mbio kumuachia mtoto sijui naanzia wapi loh

Sent using Jamii Forums mobile app
Mtoto mpumbavu ni mzigo wa ***** my dear
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom