Acha kuwa mbinafsi!!
Mkeo umemkosea, umefanya uzinzi, umezaa nje, bado kama haitoshi ukaamua kumlazimisha alee mwanao wa nje, makosa yote haya wewe unadhani unastahili adhabu gani?
Mkeo amefanya uamuzi wa kijasiri sana, kukubali uzinzi wako na kukulelea mwanao wa haramu, mwanamke mwingine asingekubali ujinga kama huo
Umefanya nini wewe kujutia kosa lako?
Umefanya nini kwa mkeo a) Kwa kosa la Kuzaa nje na b) kwa kukubali kumlea mwanao wa nje?
Mkeo bado ana kinyongo kwa makosa uliyomfanyia, ulipaswa kuwa considerate kukubali ombi la mkeo kumlea mtoto wa mdogo wake, angalau ingekuwa kama namna ya kuonesha appreciation kwake kwa ushenzi uliomtendea, bado kama haitoshi unampiga!!!!????
Ndugu zake na wengine wowote wenye akili timamu lazima wamuunge mkono mkeo
Haiingii akilini yaani ushindwe kujidhibiti nyeg zako, uzae nje, na kisha ulete mtoto nyumbani, umlalimishe mkeo amlee, halafu aombe kumlea mtoto wa ndugu yake aambulie kipigo kisa wewe ni mwanaume!!!???
Kwa makosa uliyomfanyia mkeo wewe upigwe mara ngapi!??
Hebu imagine, mkeo angekuwa dada yako na mumewe anamfanyia mambo kama haya unayomfanyia mkeo, wewe kama kaka yake ungejisikiaje!!!!???
Mkeo ni shujaa - amekuvumilia sana, alipaswa kuondoka hapo kwako siku nyingi, lakini uvumilivu wake wewe unauchukulia poa tu, wewe unashindwa naye kumvumilia!!??
Acha ubinafsi
Sent using
Jamii Forums mobile app