Kula tunda kimasihara kunavyoigarimu ndoa yangu

Kula tunda kimasihara kunavyoigarimu ndoa yangu

Habar za muda huu wanajamvi. Nitaeleza kwa kifupi.,

Kama tujuavyo mabaharia tunapita na wengi kimasihara, sasa Ktk ptpt zangu nikapata zawadi ya mtoto nje ya ndoa, mama wa uyu mtoto hana maisha ya kueleweka yupo yupo yani kimasihara, ni mtu ambaye yan ht ukiamua umwezeshe kimaisha hawezi., mambo mengi muda mchache.. kwa hiyo mimi kama baba wa uyu mtoto nikamsoma mapema hawezi kumlea mwanangu.

Nikamwambia wife everything going on, hali ilikua tete bt baadae ilibidi tu anielewe, nikamchkua mtoto akiwa na mwaka tu. na mama wa mtoto ye hana hbr yan ndo kwanza nilivomwambia akaona nampunguzia mzigo.

Mtafaruku umeanza pale shemeji wa mimi mdogo wa mke wangu anataka atuachie kichanga cha mwezi mmoja kwa kigezo anaenda kuendelea na masomo ya chuo yaani kwa kifupi kitoto kinamtinga akiwa masomoni. Kapata backup toka kwa dadaye ( mke wangu) kwamba ni sahihi aache huyo mtoto yy akapige shule.

Nilipokataa kwa busara tu za kawaida kwamba mamaye yupo haumwi na kitoto bado kidogo mno, ndipo nilipogeuka adui wa kila mtu si mke wangu, si mashemeji wote wananiona mimi sitaki kutoa msaada wa malezi ya ndugu wa mke..

Mke wangu nae ananikumbusha khsu uyu mwanangu nliempata nje ya ndoa kila ninapinga hili swala. Juzi kanijibu mbovu nikashindwa kujizuia nikampa kibano cha haja kidogo, hadi saivi yupo kwao...

Mabaharia wenzangu, dada zangu na mama zangu wazoefu wa maisha ya ndoa nipeni mwongozo, uhusiano na ndugu wa mke kwa sasa ni mbaya sana.,.

Je ni ubinafsi wangu ndo unaosababisha huu mgogoro? Niumalize huu mgogoro vipi.? Nikipokee kichanga kwa kigezo tu cha mamaye kusoma?
Mke wako alikubali kumlea mwanao wa nje, hakika inabidi umshukuru kwa huu uamuzi wake. Huyu shemeji yako aliyena kichanga cha mwezi mmoja anaishi kwako au yopo kwao? Wewe ndio unaihudumia familia ya mke wako? Katika andiko lako ni kama mke wako ano ndugu wengi sio? Huyu shemeji yako kaolewa au kazalishwa? Nitakuja tena baada ya kupata majibu haya.
 
Kwani huyo mtoto utambeba mgongoni? Utamlisha,utamfulia au utalala naye wewe? Muache maana huyo mama kwanza ana hasira za wewe kufanya uzinzi,na unapozidi kumpandisha hasira ujue mwanao unamtengenezea mazingira magumu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Makosa ya kwako mwenyewe. Kumpiga mkeo hukutumia hekima. Kumleta mtoto wa nje nyumbani kwako hapo umelikoroga na huyo mtoto maisha yake yatakuwa hatarini sana. Kuna hatari ya hiyo ndoa yako kupaa.
 
Back
Top Bottom