Kuku wangu

Ongea na jirani msameheane..siku nyingine anaweza kukufanyia kitu kibaya wewe kwa bahati mbaya!!..Mfundishe kusameheana..kosa ni kosa pale linaporudiwa!!
 
Mpige kuku faini ya ku-trespass na umkate kwenye mshahara wake ambao ni pumba na maji
 
Sitaki kumchinja bana. Kuchinja ni ukatili. Ujue kuku naye ana haki ya kuishi kama wewe ulivyo na haki hiyo.

Mchukue huyo kuku mpitie na jamaa mwende naye mahakamani. Kama una mwanasheria wako basi kamkabidhi huyo kuku ili aendelee na kesi.
 
Jamani eeh naombeni msaada. Kuku wangu kala mtama wa jirani sasa jirani kaja juu. Anataka anipeleke mahakamani. Msaada jamani.
Wewe Nyani, unamaanisha kuku ndege wa kweli au una maana kuku mwingine????? Kama ni kuku mwingine kala mtama wa jirani, mwambie naye amwachie kuku wake ale mtama wako. Hapo mtakuwa ngoma droo na kutakuwa hakuna kupelekana mahakamani tena!! Kama ungekuwa muwazi ukafafanua kwamba ni "jogoo" lako ndilo limekula mtama wa jirani ningekuelewa vizuri zaidi.
 

Similar Discussions

2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom