Kuku wana uhusiano mkubwa sana na dinosaur

Kuku wana uhusiano mkubwa sana na dinosaur

chai ya rangi

JF-Expert Member
Joined
Mar 7, 2026
Posts
1,041
Reaction score
3,089
images (9).jpeg


Angalia wanavyofanana sana,

Katika kutoa insight ya makala ninayoandaa kuhusiana na kuku nitagusia hili swala ambalo limeshafanyiwa uchunguzi na wanasayasi wengine.

Ukimuona kuku ujue umemuona T.Rex mdogo Kwa kuthibitisha hili licha ya mfanano wao wa muonekano, chunguza tabia zakuku,

Kuku ni watata ni wakorofi wanaweza kudonoana hadi kuuana kama wana ugomvi au majogoo wakikutana

Mbali na hilo, kuku analinda mayai na watoto wake kwa wivu mkubwa sana kiasi kwamba anaweza kupigana hadi na mtu.

Pia kuku ni muwindaji mzuri sana, ni kwasababu tunamfuga ndo maana tunamlemaza ule uwindaji wake unajificha. lakini panzi au wanyama wadogo wakikutana na kuku wanajua kabisa wameisha au wamedandia mtumbwi wa vibwengo kwasababu kuku ana instinct za uwindaji za hali ya juu sana.

Kwaiyo siku nyingine ukimuona kuku jua kwamba umeona dinosaur mdogo au umemuona T. Rex mdogo
 
Back
Top Bottom