Kukosa pesa kunaweza kitu watu wengi wenye tabia mbovu wanajificha humo (camouflage) na kuonekana ni wastarabu ilhali sio

May 13, 2014
90
100
Salaam wadau.!

Natumaini kabisa mko njema. Kwenye maisha yetu kila siku tumekua tukipitia vipindi tofauti tofauti ambavyo vimejaa furaha, machungu na Majonzi wakati fulani.

Binadamu anaweza kuwa ni kiumbe pekee mwenye hisia hasa hasa kwenye masuala ya kiuchumi na kijamii, ambaye kwenye vipindi ambavyo uchumi wake unapokua hauko sawa hupitia magumu sana.

Utakubaliana nami kwenye hili, Pesa ni Sabuni ya Roho na kitu ambacho kinaweza kumfanya mtu awe mwenye furaha au huzuni muda mwingi (Akiwemo mimi mwenyewe 😂). Japo wengine wenye imani zao huamini kuwa mitume wao ndio kila kitu ila mwisho wa Siku Pesa inashika nafasi ya kwanza au ya pili kwa waumini wa dini mbali mbali.

Katika uzoefu wangu wa kuishi hapa dunia toka nimeanza kuwa na akili za kutambua na kuelewa mambo, nimekuja kuona kuwa watu wengi wanaishi maisha ambayo sio yao. Sio yao kwa maana gani? Okay iko hivi, Mtu anaishi maisha ya kitumishi au mcha Mungu sana na kuanza kuzodoa au kukosoa maisha ya watu fulani oooh mara hivi mara vile.

Kuna kipindi nikiwa Chuo, nilikua naishi room mate mmoja alikuwa anajiita msabato wa matengenezo ambaye hali Nyama, hanywi Soda wala Vyakula vya Viwandani kisa tu kuwa eti vinamakemikali nilimkosoa sana kumwambia hoja zake zilikuwa dhaifu sana. Mara nyingine atashindia mkate ambao ni Brown akisema hawezi kula wali ambao umekobolewa hauna virutubisho na hakua anakula nyama ikitokea anakula wali basi anakula wali mboga mboga 😁😁.

Lakini baadae hayo maisha amekuja kuyaacha na kuishi uhalisia wake baada ya kuajiriwa. Kipindi hicho wadada walimpenda wakidai kuwa huyu hatakua tatizo kwenye ndoa. Ila leo hii anaishia maisha yake, anakula nyama, anakula wali mweupe na vingine ambavyo alidai hawezi kuvila ikiwemo pizza kisa eti inapitishwa kwenye oven mara oven inaweza kuwa miale yenye madhara.

Tuachane na huyo mwamba, Mfano mwingine unaweza ni wewe hapo unayesoma huu uzi. Kuna muda watu wamekna kama kaka au dada fulani mstarabu hanywi pombe na wala huna makuu kwenye kuvaa. Weee ukienda mwenge au makubusho stand pale unaondoka na nguo nyingi mpaka mtu fulani amevutiwa na wewe uko simple hutumii vitu ghari kumbe wapiii.!

Ni hitimishe, mimi mwenyewe asee nikiwaga sina hela huwa nashinda na wife na familia weekend nzima na huwa nasaidiaga sana kazi za nyumbani kumsaidia wife kuweka mambo sawa. Na hii yote nahisi inachangiwa na 50% upendo na 50% kukosa hela.

Sasa sijui nikija kuzifuma itakuwaje (sijui) ila umasikini ni tatizo kubwa Na wengi tunaisji kwa kuigiza sana ili tupate usikivu kutoka kwa watu kama huyu Tiktoker aliyekula Buibui akadhurika akapelekwa hospitali. Yote hayo ni kukosa pesa na kuhangaika kufuraisha watu upate follower wengi ili uweke matangazo upate hela. Ni Changamoto sana. Niwasihi ambao mnahisi watu wenu wanavumilia shida muwe wavumilivu kama wao ili mje mzione tabia zao wakizipata uo uvumilivu utaendelea kuwepo ?

 
Mwanaume kosa pesa uzijue tabia za mkeo na ukitaka kuzijua tabia za mwanaume Basi subiri apate pesa.
 
Back
Top Bottom