Kujiuzulu kwa Profesa Mohamed Janabi, akiunganishwa na Taarifa za Corona (Usahihi wa Taarifa)

Status
Not open for further replies.

Johnny Sack

JF-Expert Member
Jan 21, 2017
8,834
18,833
Usiku wa leo imesambaa taarifa kwamba Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete, Profesa Mohamed Janabi amejiuzulu kwa shinikizo baada ya kutoa maoni yake kuhusu mwenendo wa ugonjwa wa Corona nchini.

Taarifa hizo zimekanushwa; Kwa mujibu wa barua hiyo inayoonesha Profesa Janabi amefanya kumkaimisha ofisi Dr. George Longopa kuwa Acting Head Of Adult Cardiology Unit na Dr. Tatizo Waane kuwa Acting Director of Cardiology.

EUIGCBPWsAAO-1D.jpg
 
Zitto amekurupuka tena kama ilivyokuwa kwa ziara ya Rais Kusini mwa Tanzania, pale alipoibuka na mapambio ya VP.

Safari hii kakurupuka na Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete pale Muhimbili (MNH). Baada ya ile barua ya kukabidhi majukumu, Zitto kama kawaida yake kakurupuka kuaminisha umma mkuu wa Taasisi ya Moyo JK pale MNH ameachishwa au kaacha kazi.

Ieleweke kuwa Janabi mkurugenzi Mtendaji (Executive Director) wa taasisi ya Moyo JK. Sasa kaweka wasaidizi baada ya kuanzisha idara mbili ambazo zitaongozwa na wakurugenzi wawili kama wakuu wa idara hizo (Deprtmental Directors).

Kilichoandikwa kwenye ile barua (Notice) ni kuwa Janabi atakabidhi majukumu kwa wakurugenzi hao. Ieleweke kuwa awali na kabla ya Notice hii yeye Janabi alikuwa akisimamia majukumu yote, lakini baada ya hii Notice atabaki kuwa mkurugenzi Mtendaji akiacha shughuli za kila siku kusimamiwa na wasaidizi wake.

Hii pia inadhihirisha kuongezeka kwa majukumu katika taasisi hii hivyo kubadili mfumo wa usimamizi kuongeza ufanisi hakuepukiki.

Zitto acha utoto, watanzania wanauelewa zaidi yako.

BTW wewe ni wa kupuuzwa tu maana ndio siasa zenu za matukio na kukosoa mitandaoni badala ya sera na kuelemisha watu kujiletea maendeleo.
 
Niliona jana twitter.
Zitto na Msemaji wa CDM Bw.John Mrema.
Tena Mrema ndio aliishupalia kweli kweli, kuwa Dr. JANABI kaacha kazi huku wote kwa pamoja wakieleza kuwa sababu ni ile "voice note" yenye maelezo ya Dr. Janabi kuhusu virusi vya Corona iliyosambaa kwenye mitandao ya kijamii ikiwemo "whatsup".
Angalau Zitto baadae aliomba radhi, ila Mrema limemshuka mazima hajarudi tena kwenye post yake twitter.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Zitto amekurupuka tena kama ilivyokuwa kwa ziara ya Rais Kusini mwa Tanzania, pale alipoibuka na mapambio ya VP.

Safari hii kakurupuka na Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete pale Muhimbili (MNH). Baada ya ile barua ya kukabidhi majukumu, Zitto kama kawaida yake kakurupuka kuaminisha umma mkuu wa Taasisi ya Moyo JK pale MNH ameachishwa au kaacha kazi.

Ieleweke kuwa Janabi mkurugenzi Mtendaji (Executive Director) wa taasisi ya Moyo JK. Sasa kaweka wasaidizi baada ya kuanzisha idara mbili ambazo zitaongozwa na wakurugenzi wawili kama wakuu wa idara hizo (Deprtmental Directors).

Kilichoandikwa kwenye ile barua (Notice) ni kuwa Janabi atakabidhi majukumu kwa wakurugenzi hao. Ieleweke kuwa awali na kabla ya Notice hii yeye Janabi alikuwa akisimamia majukumu yote, lakini baada ya hii Notice atabaki kuwa mkurugenzi Mtendaji akiacha shughuli za kila siku kusimamiwa na wasaidizi wake.

Hii pia inadhihirisha kuongezeka kwa majukumu katika taasisi hii hivyo kubadili mfumo wa usimamizi kuongeza ufanisi hakuepukiki.

Zitto acha utoto, watanzania wanauelewa zaidi yako.

BTW wewe ni wa kupuuzwa tu maana ndio siasa zenu za matukio na kukosoa mitandaoni badala ya sera na kuelemisha watu kujiletea maendeleo.
Kwa serikali ambayo ilimfukuza Mwele Malecela kisa katangaza matokeo ya kazi yake ya utafiti, Zito ana kila haki ya kusema aliyoyasema. Na si ajabu wamebadilisha baada ya ukelele wa Zitto!
 
Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya moyo ya Jakaya Kikwete ( JKCI) Prof Janabi ambaye jana alixushiwa kuwa amefukuzwa kazi leo ameonekana hospitalini hapo akiendelea na majukumu yake kama kawaida.

Source : Ayo tv
 
!
 
Attachments

  • Instagram media - B-P-yz1ALgK ( 857 X 1080 ).jpg
    Instagram media - B-P-yz1ALgK ( 857 X 1080 ).jpg
    66.8 KB · Views: 17
Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya moyo ya Jakaya Kikwete ( JKCI) Prof Janabi ambaye jana alixushiwa kuwa amefukuzwa kazi leo ameonekana hospitalini hapo akiendelea na majukumu yake kama kawaida.

Source : Ayo tv
Nilisema jana kuwa huo ni uongo huyo Jon Mrema aliyezusha uongo huo nafikiri uelewa wake ni mdogo sana katika mambo ya kiutawala anaona Memo yeye anafikiri ni barua ya kujihudhuru!
 
Binafsi nimesoma hiyo internal memo ambayo kwa kuisoma inaeleweka/inaonyesha alikuwa anatoa taarifa tu na sio kwamba amejiuzulu au kuondolewa, ila tatizo pengine lilikuwa katika matumizi ya maneno haya:'hand over note" kwenye ile internal memo.

By definition,

A hand over note is a report that gives a summary of the activities carried out in an office or a position. It is a document that an employee who is about to leave his or her position, temporarily or permanently, writes to serve as a guide to a successor so that the workflow is not affected.

Mwenye akili atajua kosa lilikuwa wapi.
 
Tatizo ni hili:

A hand over note is a report that gives a summary of the activities carried out in an office or a position. It is a document that an employee who is about to leave his or her position, temporarily or permanently, writes to serve as a guide to a successor so that the workflow is not affected.
Did you read the contents of that Handing Over Note? It seems your extremely idiot when comes to administrative issues!!
 
Tatizo ni hili:

A hand over note is a report that gives a summary of the activities carried out in an office or a position. It is a document that an employee who is about to leave his or her position, temporarily or permanently, writes to serve as a guide to a successor so that the workflow is not affected.
Kwa wenye kuelewa , naomba nikupongeze.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unafiki wa wanajf wengi ndo utaona hapa. They are not objective but wanafuata mlengo wao blindly.

Waliosambaza uongo Ni watu wakubwa kwa maana ya Siasa za JF. Narudia JF. Not Tanzanians. Sasa Kuna watu huwa kila uzi wa kijinga lazima wa wawepo. Sasa hutawaona hapa. That says a lot about them and their ill intentions.

But all in all, tuungane kupambana na Coronavirus kadiri ya uwezo wetu. Pamoja na mazingira mazuri ya huku ulaya bado wengi tumefungiwa na Hakuna kutoka. Tunatii. Tunamshukuru Mungu kwa yote. Basi Nanyi watz wenzangu mjaribu linalowezekana kwa nidhamu na utii.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom