sirluta
JF-Expert Member
- Nov 28, 2012
- 6,325
- 2,487
Chama cha wananchi CUF kimesema kuwa, aliyekuwa mwenyekiti wa chama hicho Prof Ibrahimu Lipumba, anaweza akagombea tena uenyekiti wa chama hicho kwani ana uwezo mkubwa. Hayo yamesemwa na Kaimu Katibu Mkuu wa CUF-Bara alipokuwa akiongea na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.
Uchaguzi utafanyika 21 August 2016
========================
========================
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI JUNI 5, 2016
CUF KUFANYA MKUTANO MKUU WA TAIFA WA KUJAZA NAFASI ZA UONGOZI ZILIZO WAZI AUGUST 21, 2016:
Waheshimiwa Waandishi wa habari, kwa niaba ya Chama Cha Wananchi CUF napenda kuwakaribisha katika ukumbi wa mikutano wa Shaabani Khamis Mloo hapa Buguruni Dar es salaam. Natambua kwamba hivi sasa ndiyo tunakaribia kumaliza ngwe ya kwanza ya nusu mwaka kwa mwaka 2016 na ngwe ya pili tunatarajia kuianza ifikapo Julai mosi mwaka huu.
Napenda kuchukua nafasi hii kuwashukuru kwa dhati kabisa wanahabari wote na vyombo vya habari kwa ujumla kwa kazi kubwa mnayoifanya ya kuwahabarisha wanajamii juu ya yale yanayoendelea katika nchi na hata taarifa za nje ya mipaka ya nchi yetu. Kwa muktadha huo, natarajia pia katika tukio la leo, wananchi kupitia vyombo vyenu watapata fursa nyingine ya kufahamu nini kama Chama tunawajulisha ama wao moja kwa moja ama sehemu ya jamii kuelekea tarehe 21 August 2016.
Kwa kuanza, naomba kuwapa pole Watanzania kwa madhila yanayoendelea kuwakuta kutokana na utawala wa Dr. John Magufuli na CCM yake, pamoja na wasanii kwa nyakati tofauti kuwaambia wananchi kwamba CCM ni ile ile na Magufuli ni Yule Yule, bado watu waliamini tofauti na kwamba leo kila mmoja wetu ni shuhuda wa yanayoendelea nchini.
Sakata la uhaba wa Sukari nchini hakuna hasiyelijua likiambatana na kupanda kwa bei ya sukari ambapo katika baadhi ya maeneo hata viongozi wenyewe wa serikali wamekiri kwamba bei elekezi ya sukari haiwezi kutekelezeka kutokana na uhaba wa mali ghafi hiyo. Hivi sasa baadhi ya maeneo katika nchi hii watu wameanza kusahau matumizi ya Chai kwa kuwa uwezo wa kumudu upatikanaji wake umekuwa mgumu na hasa kwa wale waliokuwa wamezowea kupata chai mara mbili au tatu kwa kutwa.
Uendeshwaji wa kibabe wa shughuli za kibunge kunakopelekea baadhi ya wabunge wa upinzani kutimuliwa bungeni eti tu kwa kuwa walikuwa wameibana serikali kuhakikisha vikao vya bunge vinaoneshwa moja kwa moja kwenye Runinga (live coverage) imekuwa nongwa na kosa kwa mtazamo wa watawala unaochangiwa kwa kiasi kikubwa na kutokuwa na weledi wa kutosha wa Naibu Spika ni janga jingine la kitaifa linalohitaji kutafutiwa ufumbuzi wa utatuzi wake.
Matatizo yaliyowakumba wanafunzi wanaosoma Chuo Kikuu cha Dodoma zaidi ya 7000 waliotimuliwa vyuoni na maelezo tata ya vigogo wa serikali kuhusu sababu ya kuchukua uwamuzi huo mgumu ambao hauzingatii hali halisi ya kiini cha tatizo na ufumbuzi wake, ni dhahiri kwamba umelenga kuwaathiri wanafunzi katika maisha yao ya baadaye kwa kuandaliwa mazingira magumu ya kupata elemu na hivyo kufifisha ndoto zao za maisha.
Kimsingi tatizo hapa siyo wanafunzi waliopewa fursa ya kwenda kusoma, tatizo ni mfumo uliotumika wa Udahili, kitendo cha kuendelea kuwasakama na kuwahukumu wanafunzi ambao wamefuata utaratibu wote kama ulivyopangwa na serikali na kwamba wao waliofuata utaratibu wakaadhibiwa kinyama ni kutowatendea haki huku serikali ikijifanya uwamuzi waliochukua kuwa ni halali na unatibu tatizo ni kielelezo tosha kwamba nchi yetu haina haki.
Ni juzi tu hapa kila mmoja wetu amesikia hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakati akiweka jiwe la Msingi la Ujenzi wa Maktaba pale Chuo Kikuu cha Dar es slaam kwamba eti wanafunzi waliotimuliwa ndani ya saa 24 wawe wameondoka chuoni Dodoma kwa kuwa ni Vilaza na kuongeza kuwa anashangaa ni Tanzania tu ndiyo nchi ambayo waliofeli Kidato cha nne wanapata fursa ya kusoma Chuo Kikuu. Baadhi ya maneno yaliyotolewa na rais hayapaswi kusemwa na kiongozi mkuu wan chi.
Kuhamasisha Wakuu wa wilaya na Mkoa kwa hapa Dar es salaam pamoja na jeshi la polisi kuhusu wanaovunja utaratibu wa matumizi ya barabara ya magari yaendayo kasi kwamba wayakamate magari hayo na kwamba wayatowe matairi… ikiwa mwenye gari atakuja aelezwe kwamba wao (polisi) walilikuta gari likiwa halina matairi ikiwa ni njia ya kukomesha matumizi mabaya ya barabara, sina uhakika kama mheshimiwa rais anafahamu athari ya kauli yake na kwamba ikiwa huo ndiyo utawala wa sheria ambao Tanzania tunaufuata.
Wakati hayo yakijiri, wananchi wasisahau kwamba mmomonyoko wa maadili na vitendo vya kinyama vinadhidi kukithiri nchini; Mauwaji ya Waumini wa kiisalam yaliyotokea hivi karibuni pale Mwanza, tukio la juzi la wananchi wanane waliouawa pale Tanga mjini na mengineyo mengi, ni wajibu wa serikali sasa kusimama imara kuhakikisha kiini cha mauwaji kinawekwa wazi na hatua madhubuti ya kukomesha vitendo hivi vinachukuliwa kwa wahusika ili iweze kuwa funzo kwa wengine.
KUHUSU MKUTANO MKUU WA AUGUST 21, 2016:
Baada ya kuyatazama yote haya yanayoendelea hapa nchini, na kwa kuwa Watanzania wengi wameonesha kuanza kukata tamaa na mwenendo wa nchi yao, Chama cha Wananchi CUF kimeamua kuanza harakati za kujipanga upya ili kuweza kufufua matumaini ya watanzania kupata chama ambacho kitaweza kuwa mkombozi wa kweli wa maisha yao kwa kuanza na kuitisha Mkutano Mkuu wa taifa kwa lengo la kujaza nafasi zilizo wazi za uongozi wa chama ili kuweza kukiimarisha tayari kwa kuanza mapambano ya kuwapigania wananchi wa taifa hili.
Kuitishwa kwa mkutano huu Mkuu kumetokana na kuwa wazi kwa nafasi ya Mwenyekiti wa Chama taifa kufuatia kujiuzuru kwa aliyekuwa Mwenyekiti wake Mhe. Profesa Ibrahim Haruna Lipumba mnamo August 5, 2015. Aidha Mkutano Mkuu unaitishwa ili kufanya uchaguzi wa kujaza nafasi ya Makamu Mwenyekiti kufuatia aliyekuwa anashikilia wadhifa huo Mhe. Juma Duni Haji kuamua kujiuzulu na kujiunga na Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) hatimaye kuteuliwa kuwa mgombea Mwenza ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama hicho na hivyo kupoteza sifa za kuwa kiongozi wa CUF.
Zipo pia nafasi nne za Wajumbe wa Baraza Kuu la Uongozi la Taifa ambazo nazo zinapaswa kujazwa na Mkutano Mkuu huo zikiwa na mgawanyo ufuatao; Nafasi moja ya mjumbe kutoka Kanda ya Kusini, nafasi moja ya Mjumbe kutoka Kanda ya Kati, nafasi moja ya mjumbe kutoka Kanda ya Kaskazini na nafasi moja ya Mjumbe mwanamke kutoka Kanda ya Ziwa.
Kuwepo wazi kwa nafasi hizi kutokana na sababu zifuatazo: Mosi, kwa Kanda ya Ziwa nafasi ya Mjumbe mmoja mwanamke imetokana na Mjumbe wake wa awali Mhe. Mkiwa Adam Kimwanga kuhama chama na kuhamia ACT Wazalendo, Kwa Kanda ya Kati kumetokana na Mjumbe wake Mhe. Chief Lutalosa Yemba kufukuzwa uwanachama na Baraza Kuu la Uongozi la taifa, kwa Kanda ya Kaskazini kumetokana na Mjumbe wake Lebora P. Ndarpoi kujiuzuru wadhifa wake na kwa Kanda ya Kusini kumetokana na Mjumbe wake Mohamed Abdalah Khalifa kuhama Chama na kuhamia ACT Wazalendo.
Chama cha Wananchi CUF kinachukua nafasi hii kuwaomba wanachama wote wenye sifa na ambao wapo tayari kukitumikia Chama kuweza kujitokeza kuomba nafasi za uongozi kama zilivyotajwa hapo juu. Ieleweke tu kwamba nafasi ya Mwenyekiti wa taifa itagombewa na wanachama wa CUF wa upande wa Tanzania Bara tu na nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa Chama itagombewa na wanachama wa Zanzibar tu (Unguja na Pemba). Kwa nafasi za Ujumbe wa Baraza Kuu la Uongozi taifa zitagombewa na wajumbe wa Mkutano Mkutano Mkuu taifa wanaotoka katika Kanda hizo isipokuwa kwa Kanda ya Ziwa itaongezeka kwamba nafasi hiyo itagombewa na wajumbe wanawake tu.
Fomu za kuomba uongozi ndani ya Chama (UNC 1) zitapatika katika Ofisi za Makatibu wa wilaya zote nchini na kwamba Ada za malipo ya nafasi za uongozi ni kama zilivyo katika Kanuni ya Uchaguzi ndani Chama ya mwaka 2014. Mkutano Mkuu unatarajiwa kufanyika katika Ukumbi wa Hotel ya Landmark iliyopo Ubungo River side hapa Jijini Dar es salaam na kwamba wajumbe wote wa Mikoani wanatakiwa kuwasili tarehe 20 August 2016 Ofisi Kuu kwa ajili ya kujisajili na maelekezo mengine na kwa wale wa Dar es salaam wanaweza kufika moja kwa moja ukumbini tarehe 21 August 2016 saa mbili ya Asubuhi ila ni vema nao wakafika siku moja kabla kwa maelekezo mengine.
Chama cha Wananchi CUF kinapenda kuwahakikishia wanachama wake wote na watanzania kwa ujumla kwamba tumedhamiria kujipanga upya ili kurudisha uhai wa Chama na kwamba Nuru ya ukombozi wa taifa letu imekwishawaka kilichobaki kwa kila mmoja wetu kutimiza wajibu wake. Njooni tuimarishe taasisi yetu mapambano rasmi kuelekea Nuru ya Matumaini yaanze mara moja.
Mwisho CUF inapenda kuwatakia Waislamu wote wa Tanzania wakiungana na waumini wengine wa dini hiyo kote duniani, Mfungo mwema wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani na mwenyezi Mungu aweze kuwabariki sana katika Ibada yao hiyo.
Chama Imara, Uongozi Madhubuti, Nuru ya Matumaini: yanawezekana timiza wajibu wako.
Imetolewa na Kurugenzi ya Mipango na Uchaguzi Taifa,
Tarehe 5 Juni 2016.
MUNGU IBARIKI CUF, MUNGU IBARIKI TANZANIA.
Shaweji Mketo,
Kaimu Naibu Katibu Mkuu