Taarifa kwa umma kutoka CCM : Wazungumzia Kuhusu Mdahalo na Utafiti wa Twaweza

TandaleOne

JF-Expert Member
Sep 4, 2010
1,644
709
Chama cha Mapinduzi kinapenda kutoa taarifa kuhusu masuala kadhaa.

Mwenendo wa Kampeni

Kwa kifupi, Mgombea Urais, Ndugu John Pombe Magufuli na Mgombea-Mwenza Ndugu Samia Suluhu Hassan, wanaendelea vizuri na kampeni.

Kila mmoja anafanya mikutano na wananchi kati ya 8 hadi 11 kwa siku na kukutana na maelfu kwa maelfu ya wananchi. Tunawashukuru wananchi wanaokuja kwenye mikutano yetu. Tunawashukuru pia makada wa CCM wanaojitolea kwa hali na mali kukipigania Chama cha Mapinduzi na kumtafutia kura Ndugu Magufuli.

Tunaridhika sana na mwenendo wa kampeni yetu. Katika nusu hii ya pili ya kampeni tutaongeza kasi na msukumo wa kuwafikia wananchi wengi zaidi kwa mbinu na mikakati mipya.

Midahalo ya Wagombea

Tumeshangazwa na kauli ya Ndugu Kajubi Mukajanga, Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari Tanzania kwamba CCM haijathibitisha kushiriki mdahalo. CCM ilipokea mwaliko wa MCT na kuijibu kwa barua ya terehe 13 Septemba 2015 yenye kumbukumbu CMM/OND/M/190/132 iliyosainiwa na Ndugu Stephen Msami, Msaidizi wa Katibu Mkuu. Barua hiyo ilipelekwa na kupokelewa kwa Dispatch ambayo nakala yake tunayo. Baada ya hapo, Katibu Mkuu wa CCM, Ndugu Abdulrahaman Kinana, alifanya kikao na wawakilishi wa MCT katika ofisi ndogo ya CCM Lumumba ili kutaka kujua zaidi na kutoa maoni ya CCM kuhusu utaratibu mzima wa mdahalo. Katika kikao hicho, ambapo MCT iliwakilishwa na Afisa wake, Ndugu Allan Lawa, pamoja na Ndugu Tido Mhando, CCM ilithibitisha tena kushiriki mdahalo. Tatu, tarehe 16 Septemba 2015, CCM ilitoa kauli rasmi, iliyosainiwa, ikithibitisha kushiriki mdahalo. kauli ya Ndg Mukajanga inalenga kuwasaidia kisiasa wale ambao hawajathibitisha au hawana nia ya kuthibitisha kushiriki. Kwa msingi huu, tunaamini ni vyema mdahalo huu ukaandaliwa na ushirika wa taasisi mbalimbali zilizokuwa na nia ya kuandaa midahalo, (kama vile CEO Roundtable, UDASA, TWAWEZA) ili kuiondolea uwezo taasisi moja au kikundi cha watu wachache, kuhodhi na kuwa na ukiritimba kwenye jambo hili kubwa na muhimu.



CCM inapenda kusisitiza yafuatayo:

1. Ndugu Magufuli amekubali kushiriki mdahalo wa wagombea Urais

2. Mdahalo uwashirikishe wagombea wenyewe na sio wawakilishi wao.

3. Wagombea wote, hasa wa vyama vikuu, wawepo na washiriki. Tunapozungumzia mabadiliko katika nchi maana yake ni utayari wa kufanya mambo mapya yenye tija ambayo hayajawahi kufanyika, ikiwemo mdahalo wa wagombea Urais. Wanaohubiri mabadiliko huku wakiogopa kushiriki mdahalo wanahubiri mabadiliko hewa.

UTAFITI WA TWAWEZA

CCM haikushangazwa na matokeo ya utafiti wa taasisi huru ya Twaweza yaliyotangazwa jana ambayo yanatoa ushindi wa asilimia 65 kwa Ndugu John Pombe Magufuli dhidi ya asilimia 25 za Mgombea wa UKAWA. Hatukushangazwa na matokeo ya utafiti huu kwasababu tano:

1. Siku UKAWA walipomteua Ndugu Edward Lowassa kuwa mgombea wao ndio siku CCM ilipohakikishiwa ushindi katika uchaguzi wa mwaka huu. CCM hatukumteua kwasababu tuliamini hakuna namna ambapo Watanzania wengi watamchagua.

2. Katika uchaguzi wa mwaka huu CCM tunafanya utafiti wetu wa ndani wa kisanyansi kila wiki kujua mwenendo na mwelekeo wa kampeni na maeneo yanayohitaji nguvu mahsusi. Tangu tuanze utafiti wetu mwishoni mwa mwezi Agosti, karibu kila wiki asilimia za ushindi wa CCM hazijawahi kushuka chini ya asilimia 60 na zimekuwa zinapanda.

3. Kazi kubwa anayofanya mgombea wetu, Ndugu John Pombe Magufuli, na mgombea-mwenza, Ndugu Samia Suluhu Hassan, kuzunguka nchi nzima kwa barabara na kuongea moja kwa moja na wapiga kura inazaa matunda. Wanawafikia wapiga kura wengi, hasa wa vijijini, na wapiga kura hao wanawaelewa.

4. Kampeni kubwa zinazofanywa na wagombea Ubunge na Udiwani wa CCM na makada na viongozi wa Chama katika ngazi zote nchi nzima kila siku kumuombea kura Magufuli nazo zinazaa matunda.

5. Tunaamini pia migogoro ndani ya UKAWA katika kipindi hiki cha uchaguzi iliyopelekea mitafaruku katika kuachiana majimbo na, baadaye, kutokana na uteuzi wa Mgombea Urais wa UKAWA, kupelekea kujiuzulu kwa viongozi wa muda mrefu na maarufu wa UKAWA, Profesa Ibrahim Lipumba na Dr. Wilbrod Slaa, na migongano ndani ya NCCR-Mageuzi, yote haya yamepunguza imani ya wananchi kuhusu uwezo wa vyama hivi kushika dola.

Lakini vilevile matokeo ya utafiti huu ni ishara kwamba Watanzania wamempokea na kumuelewa Ndugu Magufuli na wako tayari kumkabidhi nchi. Sisi kama CCM kuna baadhi ya mambo tumeyachukua katika utafiti huu na tutayafanyia kazi ili kujihakikishia ushindi. Tumeshangazwa na taharuki, hasa kutoka miongoni mwa wasomi na wanaharakati, kuhusu matokeo ya utafiti huu.

CCM ilitegemea kwamba jamii ya wasomi na wanaharakati ingefurahia utamaduni wa tafiti za kisiasa unaoanza kujitokeza hapa nchini ili siku zijazo tujikite katika kurekebishana kwenye kanuni za utafiti na ithibati na uhakiki wa ubora. Tunasikitika kwamba yanawekwa mazingira ya kutisha na kukatisha tamaa (atmosphere of intimidation) kwa watu wanaotaka kufanya tafiti za kisiasa nchini.

Utafiti ni sayansi. Matokeo ya utafiti hupingwa kwa matokeo ya utafiti mwingine, sio kwa kuponda tu au kwa matusi na vitisho. Ni vyema tukajifunza kupokea habari mbaya bila taharuki. Itakumbukwa kwamba, mwezi Agosti 2010, taasisi ya utafiti ya kimataifa ya Synovate ilitoa utafiti ikionyesha kwamba CCM itashinda Uchaguzi Mkuu wa 2010 kwa asilimia 61.

Baadhi ya wana-CCM hawakufurahishwa na matokeo ya utafiiti huo kwasababu waliamini kwamba ushindi wetu ulikuwa ni mkubwa zaidi. Wapinzani waliwalaani, kuwatukana na hata kutaka kuwashtaki Synovate. Kwenye matokeo halisi ya kura, CCM ilipata asilimia zilezile 61 zilizotabiriwa na Synovate.

Ni vyema kuweka akiba ya maneno kwenye masuala haya.

Imetolewa na:

January Makamba
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa Mjumbe wa Kamati ya Kampeni ya CCM

23.09.2015
 

Attachments

  • 2015 - JANUARI - PRESS - MWENENDO WA KAMPENI - 23.9.2015.pdf
    2 MB · Views: 157
Nimeona katika habari baadhi ya viongozi Wa ccm kusema imepunguziwa ushindi toka 69 hadi 65 ℅ .Kwa kweli ni mfano Wa kuporomoka elimu, tafiti hizi ni opinion polls zinazotumia cross section approach ,yaani Taarifa inayopatikana ni kweli Kwa wakati ilipofanyika tu na so wakati mwingine, ndiyo maana twaweza ilikuta hali tofauti baadae na Kama mwingine akifanya Leo anaweza kuta imeshuka tena. Kama wanapinga hilo hawajui maana ya cross section studies kiasi mtu anasema twaweza wametupunguzia ushindi? Nini maana ya kampeni kama si kushawishi watu wageuke, na unaweza geuza hata 95℅ mwishowe. Mtu asitudanganye ,waweke tafiti lakini swala la kugombea asilimia za ushindi ziwe zile zilizofanywa as point studies ni kutoelewa maana ya aina mbalimbali za tafiti na mbinu zake.
 
UTAFITI wenyewe walihonga, sasa wanajifanya eti hawakubali ili watz waseme kwamba ccm hawakuhonga ndiyo mana wanapinga matokeo. Watz wanaakili kuliko za ccm. Wasubiri Oct 25 ndiyo watajua watz wanampenda nani kura rais. Watajua kumbe watz wanampenda Lowasaaa!!!!!!!
 
Kwa kifupi, Mgombea Urais, Ndugu John Pombe Magufuli na Mgombea-Mwenza
Ndugu Samia Suluhu Hassan, wanaendelea vizuri na kampeni. Kila mmoja
anafanya mikutano na wananchi kati ya 8 hadi 11 kwa siku na kukutana
na maelfu kwa maelfu ya wananchi. Tunawashukuru wananchi wanaokuja
kwenye mikutano yetu.
Tunawashukuru pia makada wa CCM wanaojitolea kwa
hali na mali kukipigania Chama cha Mapinduzi na kumtafutia kura Ndugu
Magufuli.
Watu wanajitokeza kucheki shoo za bure za wasanii.
 
Musitusumbue. Kwani jk alipogoma kuna mtu alimlazimisha...lowassa haendi na mikumbo...hiyo midahalo kafanyeni na twaweza yy yuko bize na wananchi. By the way chaumma, tlp na act wamekubali. Mnaweza mkaenda mkafanya.
 
Wanataka kucheza na saikolojia ya watu tu hawa. Wanahamisha attention kutoka kwenye validity and reliability questions of the paper, ili muanze kujadili percentage za ushindi wa ccm. Wendawazimu huu.

HATUDANGANYIKI. HATUTARUHSU CCM IKAE MADARAKANI KWA GHARAMA YOYOTE, HILO WALIJUA KINA MAKAMBA NA WAHUNI WENZAKE.
 
MALAMBA umeahidiwa uwaziri nchi za nje mnataka mdahalo Na Wapumbavu na Malofa watasema kitu ganó zaidi ya kusubiri 25 october
 
Tandale one hivi uchaguzi unaofanyika nchi hii ni wa urais tu? Kwanini hamuongelei midahalo ya wabunge na madiwani? Tulijua tu lazima mtakuja na tulitegemea January Makamba ndiye atakimbilia kuhakikisha ule upuuzi ulioletwa na Twaweza unakubalika. Siku za hivi karibuni Janury Makamba amekuwa na kiherehere yeye na baba yake kwamba ndio wanajua sana watanzania wanataka nini. January Makamba anajua baba yake ndio alikataa midahalo tena kwa barua nchi nzima. Kama walikatazwa midahalo kuanzia urais, ubunge na udiwani kwa barua je wameshaandika barua kwa ngazi hizo kuwaruhusu?

Tunaangalia umbali toka tafiti ya kupikwa ya ccm na pamoja na Twaweza na ukaribu wa makada wa ccm akiwemo Janury Makamba na waandamizi wengine wa chama hicho kwenye taasisi hii. Matokeo haya ni dhahiri ni ya kupikwa hasa ukizingatia nguvu kubwa inayotumika na ccm kuhakikisha tafiti hiyo inakubalika.

Udhaifu wa wazi wa taarifa hii ni kwamba, hakuna uwiano wa muelekeo wa ccm kwenye kampeni hii zaidi ya sehemu kubwa kujikita kwenye kulazimishia yale yaliyoletwa na Twaweza jana. Ina maana ccm sasa hivi kampeni yao maelezo yake mengi yako kwenye ile taarifa ya jana ya Twaweza? Na ni kwanini January Makamba anayetuhumiwa kuwa karibu na twaweza ndio ajitokeze kutolea maelezo mengi ya Twaweza kama kipimo cha kampeni yao mpaka leo?

Sisi watanzania sio wajinga na kama ccm inataka kupata madaraka kwa kulazimisha ijiangalie sana. kwani hao akina January wamegeuza nchi hii ni mali yao hivyo wanataka kuanzia wazazi wao, wao wenyewe na familia zao wabaki watawala wa nchi hii hata kwa kumwaga damu. Hilo tunasema halitawezekana kamwe, na tuko tayari kwa mabadiliko amani. Tunataka kabla ya midahalo ya wagombea wa urais, tuanze na wabunge na madiwani. Na Janury Makamba atuambie ni nini kinachomfanya ajifanye anapenda demokrasia wakati kila siku anataka kupita bila kupingwa?

CC: Kitila Mkumbo, Zitto, John Mnyika, mwanadiwani, Mwigulu Nchemba, Godbless Lema, January Makamba
 
Sioni sababu ya kushiriki midahalo ya ubishi na kutoka povu.
Kama CCM walikataa Kikwete kushiriki mdahalo uchaguzi ulopita sioni sababu ya ukawa kujisumbua.

Nashauri ukawa endeleeni na kampeni badala kushiriki midahalo ambayo waongozaji ni CCM wenyewe.

Malofa wanawahitaji ndio wa kuongea nao!
 
Mdahalo lazima na Lowassa lazima aje atueleze kwa nini tumchague

Sio kutuletea wabunge wa viti maalum au ma dj
 
Katika hayo mi ntajibu matatu la kwanza umesema wasomi wengi wanabishia utafiti, ni kweli ukiona kitu wasomi wanatilia shaka nacho lazima kitakua na kasoro fulani hasa kama kitu chenyewe ni cha kisomi, pili suala la watu kujaa ktk mikutano yenu nashauri mara nyingi embu jaribuni kufanya mikutano yenu bila kuhusisha wasanii zaidi ya kikundi chenu cha TOT HAPO NDO MTAJUA JE MIKUTANO YENU INA MAUDHURIO KIASI GANI.

Zaidi ya hapo ni kujidanganya sababu wenzenu ukawa wanauwezo mkubwa kujaza uwanja wowote bilahata msanii yoyote sasa mjipime pia ktk hilo, la mwisho suala la mdahalo ni maamuzi ya chama au mgombea jiulize je kikwete ku mdahalo aliwai kuhudhuria?

Kwanini kwa mwingine iwe agenda..
 
Huyu January Makamba Ndio Amebaki kila Kitu ndani ya CCM.Utafiti ndani ya Chama yeye, Ndani ya Twaweza yeye..Duuh!! Mnajidanganya wenyewe.
 
Lowassa hatajiongezea idadi yoyote ya kura kwa njia ya midahalo; midahalo inaendeshwa na walionacho ambao tayari wameshajipambanua kuulinda mfumo uliopo ili waendelee kufaidi keki ya taifa kwa upendeleo.

Yaliyofanywa na twaweza ndio yatakayofanywa katika midahalo ku discredit upinzani na wala hakuna lofa atakayenufaika na midahalo hiyo inayoandaliwa kuwaumiza. Lowassa akitaka midahalo akaongee kwenye vyombo vya habari vya nje ya nchi sio hivi vinavyojulikana wazi vinampromote nani..
 
Ccm Kama Mna Akili Timamu Hamuwezi Kufanya Mdahalo Na Mbumbumbu,wapumbavu Na Malofa.Huu Ni Utani Jamani,jipangeni Upya.
 
Makamba tulishakuzoea, wew hata galanosi uliiba mitihani, so siasa za wizi wizi ni kawaida kwako, hapo mnakuja na siasa za ajabu ili kuuaminisha umma kuwa ccm inapendwa kumbe laa, toka lini wasomi wakaipenda ccm? vijana wenyewe waliojiandikisha wako takriban 15 Million ,wote wanataka mabadiliko, nyie mmekazania tafiti , pole sana.

Kuhusu mdahalo nendeni mkaongee, mabadiliko tunayohitaji sio mdahalo, ni mabadiliko ya mfumo na uongozi mbovu uliotufisha hapo. kama ccm mnadai mnataka mabadiliko na nchi mpya je mko tayari kubadili katiba? mpo tayari mawaziri wasitokane na wabunge? mko tayari wakuu wa mkoa na wilaya wachaguliwe na wananchi? mko tayari kuona tanzania mfumo wa mahakama, tume ya uchaguzi iwe huru na watumishi wake waweze kuteuliwa na bunge? mko tayari kuona spika wa bunge hatokani na chama chochote cha upinzani? hayo ni machache tunayoyahitaji wala sio mdahalo.
 
Back
Top Bottom