MamaSamia2025
JF-Expert Member
- Mar 29, 2012
- 10,224
- 22,304
Ninawasalimu kwa jina la chama pendwa CCM.
Kama kichwa cha habari kinavyojieleza ni kwamba hili jambo limenitafakarisha sana. Tukumbuke mara baada ya uhuru waasisi wa taifa walipambana sana kujenga umoja wa kitaifa kwa mbinu nyingi na juhudi kubwa.
Kiswahili kilitumika na kinaendelea kutumika taifa zima la Tanzania. Ni nadra sana kukuta nchi ya kiafrika inaongea lugha moja. Tanzania tumeweza. Kutoka Mutukula hadi Mbamba Bay lugha ni moja KISWAHILI.
Waasisi hawakuishia kwenye lugha tu. Hata kwenye elimu na ajira walimtoa wa kaskazini nakumpeleka kusini na wa mashariki kwenda magharibi ili watu wachanganyike na kuzidi kuangamiza ukabila. Hili pia limefanikiwa sana.
Nyakati za uchaguzi hapa nchini huwa watu wanapigania vyama na ni ngumu kukuta mambo ya ukabila yanazungumzwa. Ni bahati mbaya kwenye utawala uliopita ndo kidogo karibia utuletee mambo ya ukabila Mungu akaepusha.
Lakini kwa bahati mbaya zoezi la watu wa makabila tofauti kuoana limeleta changamoto ya watu wengi kutojua lugha za makabila yao. Mojawapo ya mambo muhimu kwenye kulinda utamaduni wetu ni kuwarithisha vizazi lugha zetu za asili.
Vijana wengi kwa sasa hawajui tena lugha za makabila yao. Mtu ni mchaga lakini hawezi kuongea kichaga. Au Msukuma lakini hajui Kisukuma.
Binafsi napongeza waasisi kwa huu umoja wetu ila kama taifa tufikirie namna gani tunaweza linda lugha zetu zisipotee kabisa. Kwenye kizazi cha miaka ya 2000 wapo watu wachache wanaoweza zungumza lugha za makabila yao. Nadhani sisi wa 80's ndo angalau wengi tunajua lugha za asili zetu. JE, NINI KIFANYIKE?