tinna cute
JF-Expert Member
- Sep 22, 2013
- 4,630
- 2,317
'cute' nawe unajamba ?
Sana tena shuzi langu balaa hasa nikila ufuta nazalisha bomu.
'cute' nawe unajamba ?
Hahah,,ukijamba miaka 6 mfululizo unatoa ki2 cha atomic bomb,,duh! Af mkuu kikundu ndo nn?
Mambo Kumi ya Kushangaza Kuhusu Kujamba
11:35 PM | No comment
Kwanini tunajamba?kwanini "ushuzi" unanuka?Kujamba inaweza kuwa kitendo cha aibu kwa wengi wetu,lakini inaweza kukufanya ujisikie vizuri kujua kwamba ni tendo la kawaida sana kwa mwili wa binadamu kutenda.Kila mtu anajamba,hata Halle Berry nae hujamba.
1.Kujamba ni nini hasa?
![]()
Kujamba kunasababishwa na kubanwa kwa hewa,ambayo inaweza kutoka mwilini kwa njia nyingi.Baadhi ni hewa tuliyoimeza wakati wa kula au kunywa.Hewa ingine husababishwa na gesi kuingia kwenye utumbo wetu kutoka kwenye damu,na baadhi ya gesi huzalishwa na kemikali katika utumbo au bakteria.Kwa kawaida "ushuzi" unakua na asilimia 59 ya gesi ya nitrogen,asilimia 21 ni hydrogen,asilimia 9 ni carbon dioxide,asilimia 7 methane na asilimia 4 ni oygen. Asilimia moja tu ya "ushuzi" inaweza kuwa hydrogen sulfide na mercaptans,ambayo ndio ina sulfur ndani yake,sulfur ndo hufanya "ushuzi" utoe harufu mbaya Kujamba huambatana na sauti,hii ni kutokana na "vibration" katika njia ya haja kubwa.Ukubwa wa mlio wa kujamba hutegemea "presha" inayosukuma gesi itoke nje na pia ugumu wa misuli ya njia ya haja kubwa.
2.Kwa nini Ushuzi hutoa Harufu mbaya?
![]()
Harufu mbaya ya ushuzi hutegemea na ulaji wa mtu,vyakula vyenye sulfur kwa wingi ndio husababisha hili.Vyakula vyenye sulfur kwa wingi ni kama maharage,kabichi,soda na mayai.
3.Watu hujamba hadi mara 14 kwa siku
![]()
Mtu wa kawaida hutoa hata nusu lita ya ushuzi kwa siku.Inasemekana mtu akijamba mfululizo kwa kipindi cha miaka 6,anaweza kuzalisha nishati ya kutosha kutengeneza bomu la atomiki.
4.Ushuzi husafiri kwa mwendo wa futi 10 kwa sekunde.
![]()
Harufu ya ushuzi huanza kusikika sekunde 10-15 baada ya mtu kujamba,hiyo ni kwa sababu inachukua muda mrefu kwa harufu kufikia pua.
5.Kujizuia Kujamba Inaweza Kuhatarisha Afya Yako
![]()
Madaktari hawajakubaliana moja kwa moja kama kujizuia kujamba ni hatari kiafya.Baadhi ya wataalam wanafikiri kujamba ni sehemu muhimu katika mfumo wa mmeng'enyo wa chakula,hivyo kujizuia kujamba haitakuletea madhara.Wengine wanadhani kwamba kujizuia kujamba kunaweza kusababisha tumbo kujaa gesi,na pia inaweza sababisha kikundu(hemorrhoids).
6.Kwa Baadhi ya Tamaduni,Kujamba Sio Ishu
![]()
Wakati tamaduni nyingi zikichukulia tendo la kujamba lifanywe kistaarabu,kuna baadhi ya tamaduni hawaoni haya kujamba hadharani,na pia hufurahia tendo hilo.Mfano kabila la Yanomami huko America ya Kusini,kwao husalimiana kwa kujamba,na China unaweza kupata kazi ya kunusa ushuzi! Katika Roma ya zamani,Mfalme Claudius akihofia kwamba kujizuia kujamba inaweza kuwa hatari kiafya,alipitisha sheria kwamba ni ruhusa kujamba kwenye "banquets".
7.Ushuzi Unawasha Moto
![]()
Kama ilivyoandikwa hapo juu,methane na hydrogen inayozalishwa na ushuzi inaweza sababisha moto.
8.Mchwa Hujamba Kuliko Wanyama Aina Zote
![]()
Ni ngumu kuamini kuwa mchwa ndo anawajibika na matatizo yetu ya "Global Warming".Mchwa huongoza kwa kujamba kwa wanyama,na hiyo huzalisha gesi ya methane.
9.Ukiubana Ushuzi,Utakutoka Usingizini
![]()
Hata ujitahidi kuubana vipi,ushuzi utatoka mara utapokua umepumzika,hasa ukiwa umelala.
10. Watu Hujamba Hata Baada ya Mauti Kuwafika
![]()
Maiti huendelea kutoa gesi hadi masaa matatu baada ya mtu kufariki dunia,hii huambatana na milio ya kujamba.Hali hii husababishwa na misuli kusinyaa.
walimwengu
mkuu kama umesoma vizuri thread,kujamba husababishwa na kubanwa kwa hewa,nadhani hawa hawana "luxury" ya kujamba since wako wazi,hakuna hewa wanayoibana,km nimekosea nisahihishwe.
At last you have revealed what is in your mind,no wonder post zako huwa ziko namna zilivyo,kumbe umejaza hayo madudu kwenye brain yako.
Pole sana Faiza.
Asante kwa kujidhihirisha, utakuwa umewasaidia wengi waliokuwa wanajibizana na wewe.
kwanini hivi huwa unapenda kutusi sana?
nimejumlisha mada iliyotolewa na comment yako nimecheka mpaka machozi!Nimeuachia sasa hivi, duh! kumbe ndo ilivo!
hiyo namba sita hilo kabila naona siyo waislam , maana kila siku wangekuwa hawana udhukinacho nishangaza ni namna wenzetu walivyo kaa na kufanya utafiti na kuleta hizo data.
Swali?
1. Je kweli ya wanaume inanuka sana kuliko wanawake?
2. Je Rais hujamba akiwa katika gari lake au ndege?
...nasikia kwa ndugu zetu wahindi kujamba ni kitu cha kawaida kabisa na unaweza hata kupongezwa na uliokaa nao karibu ukitoa shuzi la sauti kubwa lililokwenda shule...!